Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Wanabodi,

Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa nafsi yako yote na kuilinda na kuitetea kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, na kwa uwezo wako wote, na ikibidi kuipigania, uwe tayari kuutoa uhai wako kuifia nchi yako!

Uzalendo wa kweli hukaa ndani ya mtu, hauonekani kwa macho, bali hukaa moyoni, hivyo kuna watu ukiwaangalia kwa juu juu at face value kwa jinsi wanavyo onekana, wanaonekana kama ni wazalendo, lakini in reality sio wazalendo lolote wala uzalendo chochote, bali ni wapigaji, na baadhi yao ndio mafisadi wakubwa!. Wamejivisha ngozi ya kondoo ya uzalendo,Ila kwa ndani ni mbwa mwitu, fisi, Chui na Chatu kabisa!

Na kuna watu ni hohe hahe, masikini wa kutupwa, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, lakini wana moyo wa upendo wa dhati kwa taifa lao na ndio wazalendo wa kweli wa taifa hili, Mimi najihesabu ni mmoja wa wazalendo hawa, sinyamazi kusubiria wasifu ile siku, najitanabaisha wazi ili ikifika angalau nihesabiwe nilisema, niliandika na kutengeneza kipindi cha TV.

Ukiona kuna kitu serikali yako imeshindwa na wewe unaweza kusaidia, saidia tuu usingoje uombwe, na nilivyofanya huko nyuma, na ndicho ninafanya hapa.

Baada ya Tundu Lissu kushambuliwa na wasiojulikana, serikali yetu ilishindwa kuwapata, mimi ni miongoni mwa tuliojitolea kuisaidia serikali yetu kuwabaini wasiojulikana hawa, WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?

Kwenye ulinzi wa Rasilimali zetu, kwa muda mrefu Tanzania tumekuwa na kilio cha kufanywa shamba la bibi kwa manyang'au kutuibia Rasilimali zetu as if hazina mwenyewe!.

Tanzania tunaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?.
Wasalaam

Paskali​

Hata kwenye huu mjadala wa ubinashishaji wa Bandari yetu kwa kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, tunaendeleza uzalendo ili tusiendelee kufanywa shamba la bibi Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Hakuna. Mtanzania yeyote mwenye akili zake timamu anapinga maendeleo ya nchi yake, kinachotakiwa ni tumefanywa sana shamba la bibi, tusiendelee kufanywa shamba la bibi, let's negotiate a good deal
P
 
Hivi P ibara ya 6 na 13 unaionaje wewe kama wewe?? Ni deal nzuri au??
 
Hata kwenye huu mjadala wa ubinashishaji wa Bandari yetu kwa kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, tunaendeleza uzalendo ili tusiendelee kufanywa shamba la bibi Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Hakuna. Mtanzania yeyote mwenye akili zake timamu anapinga maendeleo ya nchi yake, kinachotakiwa ni tumefanywa sana shamba la bibi, tusiendelee kufanywa shamba la bibi, let's negotiate a good deal
P
Na huo ndio ukweli mchungu. !!
 
Tuwe kama China. Adhabu kifo. Uone kama watu wataiba mali ya umma..
Na huo ndio ukweli mchungu. ! Lakini kwanza Kabisa ni Katiba mpya bora ambayo itaifumua mifumo yote inayotakiwa itende haki kwa watu wote ili kusiwepo na uonevu au upendeleo wowote kwa yeyote yule !

Kisha mifumo isukwe ipasavyo !! Hata hao wachina mpaka wamefikia hapo wameshapitia changa moto nyingi kama zetu na kushinda zetu !!

Panapo na nia na njia ipo !! It can be done play your part !
In Mwalimu’s voice R.I.P 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom