Hapa ninaona mambo mawili.
Kwanza ni uelewa wa wachangiaji kwenye neno re-flagging. hivi kweli wote wanaochangia wanalielewa neno hilo.
Re-flagging ninavyoelewa ni kubadilisha nationality ya kitu yaani kama utaifa. Hivyo, meli ilikuwa ya Tanzania, sasa ikiwa re-flagged Kenya inakuwa si ya Tanzania tena inakuwa ya Kenya.
Kama nimekosea nisahihisheni.
Kwa maana hii ni kwamba kilichofanyika ni meliza Iran sasa kuonekana na bendera ya taifa ililomo Zanzibar. Hapa kwenye RED mnivumilie kwanza maana imetumia neno taifa ililomo Zanzibar.
Sasa, tuje kwenye mambo ambayo tunapigizana kelele kila leo. Mambo ya muungano. Zanzibar kwa miaka mingi imekuwa ikipiga kelele kuwa na bandari yake. Ok, wana haki hiyo, hatuwezi kuwazuia.
Lakini biashara ya re-flagg maana yake bendera ya meli au ndege inabadilika inakuwa ya taifa jipya lililonunua meli.
Tuje tena kwenye yaleyale ya muungano. Kama ilivyolilia bandari ndivyo Zanzibar kwa siku nyingi imelilia kuwa na wimbo wa Taifa wake na bendera yake. Naamini hadi hapa hizi RED mbili zitaeleweka.
Kama Zanzibar ilijua inafanya biashara hii kwa kupitia bandari yake kwa nini isitumie Bendera ya Zanzibar kwa sakata kama hili.
Kama ilitumia Bendera ya Taifa la Jamhuri ya Muungano basi wawajibike haohao viongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Waliyataka wenyewe, hivyo mimi ninaiona hii ni sawa kabisa na moja ya plague au janga la matatizo ya muungano ambayo wengi wanaita ni kero kana kwamba ni sisimizi anakutekenya kumbe ni joka liko chumbani mwako.