Tanzania tunapaswa kuwa na uhuru wa kuamua ni nchi gani tunashirikiana nayo kidiplomasia, kiuchumi n.k. Lakini kimsingi uhuru huo hatuna kwa sasa kwani nchi tajiri na wahisani wanatuamria nani tushirikieane naye na nani tufarakane naye kwa kigezo cha utegemezi wetu kwao. Tunahitaji mabadiliko katika dira ya uongozi ili tuwe nchi yenye uhuru kamili.
Mkuu, nakubaliana na wewe hususan hapo kwenye wekundu.
Lakini kilichofanyika hapo kuhusu hizo meli kubwaa za mafuta siyo uhuru tena ni uhuni.
Haiwezekani kama nchi, mkakubali kubadilisha majina ya meli zisizowahusu na kuzipa bendera ya nchi yenu kupeperushwa ilhali dunia yote inajua nchi ya Iran ina ugomvi na karibu dunia nzima kuhusu matumizi ya vinu vya nishati ya nyuklia.
Mimi ninaamini kabisa kwamba serikali haijui lolote kuhusu huo uhuni, kwani inajua madhara yake. Bali kuna wahuni wachache ambao wameutumia mwanya fulani uliokuwepo kutekeleza uhuni huo.