Tanzania Now Faces Sanctions & Diplomatic Crisis Over Iran

Status
Not open for further replies.
Waziri wa Znz yuko sahihi kusema yafuatayo:

1. Kuwa wao hawajavunja sheria yeyote kusajili meli hizo.
2. SMZ kwa kupitia ZMTA wako huru kusajili meli yeyote bila kushauriana na waziri husika wa muungano.
3. Na kwamba kwa kupitia agent wao Dubai (Philtex) ndio walisajili hizo meli.

Sawa lakini implication ya hilo ni kubwa nae kama haelewi basi kuna taabu hapa. Maana kwa kuanzia ile point yake kuwa hizo meli zinamilikiwa na raia wa uingereza kupitia virgin iland na seychelles si kweli, ama sivyo hawa jamaa(USA) wasingepoteza muda wao, hiyo ni katika namna ya Iran kukwepo vikwazo.

Pili tayari wameshajua meli hizi zimesajiliwa Znz kukwepa vikwazo na hii sasa haisaidii maana tayari wanazijua hivyo hazitapata bima kama walivyokuwa wanataka mwanzo.

Tatu kipato kikuu cha Znz ni utalii na hao watalii wengi Znz wanatoka mataifa hayo ya magharibi sio arabuni au Iran, hivyo hizo nchi zikiwashauri raia wao wasije Znz basi hilo pengo ni kubwa, na hata karafuu wakiamua kugomea kuziwekea vikwazo meli zao ndio mwisho wa Smz.

Hiyo yote ni kuwa na upeo mdogo wa kufikiri, kwa nini ujiingize kwenye mgogoro usiokuhusu, tena ilhali wewe mwenyewe uko goigoi na maskini bin taabani? Hivi US wakituwekea vikwazo au kutuvamia(sidhani kama watafanya hivyo) Iran wana ubavu au hata uwezo wa kuja kutusaidia? haya ndio mambo ya kufikiri kabla ya kuropoka tu bila kujua athari ya matendo yako.

Mwisho wa yote, nafikiri Znz watakubali kuwa walifanya kosa na si ajabu huyo Waziri au mkuu wa ZMTA wakaondolewa au kujiuzulu, hili si swala dogo kabisa.
 
Tanzania tunapaswa kuwa na uhuru wa kuamua ni nchi gani tunashirikiana nayo kidiplomasia, kiuchumi n.k. Lakini kimsingi uhuru huo hatuna kwa sasa kwani nchi tajiri na wahisani wanatuamria nani tushirikieane naye na nani tufarakane naye kwa kigezo cha utegemezi wetu kwao. Tunahitaji mabadiliko katika dira ya uongozi ili tuwe nchi yenye uhuru kamili.

Thubutu yenu mtatafutwa mpaka chini ya uvungu wenu
 
Ni vyema watu wakafahamu kwamba kwenye maritime law kuna uhuru wa meli/tanker kujisajili na kupepea bendera ya nchi yeyote....

Ni vema vile vile kujiuliza kama taifa hivi tutaburuzwa mpaka lini na hawa mabeberu.
Sawa, una uhuru wa kufanya unalotaka, lakini mfadhili wako amesema unachofanya kinamkera, anaamini unaikwepesha Iran vikwazo vya kimataifa. Hao sio mabeberu, hao ni mabwana misaada wetu, kama unataka kufanya unachofanya wamesema wanakata misaada.

Kwa maneno mengine, una uhuru wa kuchagu bwana yeyote yule, ila tu, chagua bwana mmoja, Marekani hataki kufanywa buzi la misaada halafu likikupa amri zake hutaki.

Pia, nilisema humu siku ile Kikwete alipohutubia Taifa kwenye Mei Mosi, Tanga, akitetea Iran na mradi wao wa umeme wa nuklia. Ile sina shaka baada ya zile comments za Kikwete kuna briefings zilifanyanyika kwenye ma "situation rooms" huko US, wakamaindi na kuanza kutuchunguza, matokeo yake ndio haya. Tusidhani balozi wa Marekani yuko hapa kufungua miradi ya visima tu, kazi kubwa ya balozi wa US popote pale ni kutuma nyumbani update za chochote kinachoendelea kuhusu interests za US.
 
Dear President Kikwete,

I am writing to express my deep dismay that Tanzania has permitted the National Iranian Tanker Company (NITC), to reflag at least 6 and as many as 10 of its vessels under the Tanzanian ship registry, allowing them to remain under NITC ownership and continuing to transport Iran’s crude oil exports. This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research programs and its support for international terrorism.

It is profoundly disappointing to me to learn that your government has acted in contravention of the broad international coalition that is working together to use peaceful means, including economic sanctions, to change the threatening behavior of the Iranian regime. The decision to accept the re-flagging of NITC vessels casts a shadow over Tanzania’s international reputation.

I respectfully request that Tanzania cancel the re-flagging of the NITC vessels. Given the close and cooperative relationship that our two governments now enjoy, it would be unfortunate if this action were permitted to stand.

It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord. However, your government should take note of President Obama’s Executive Order 13608, signed May 1, 2012, which provides for the imposition of sanctions on any entity worldwide, including foreign governments, that assists Iran in evading U.S. sanctions. In my view, reflagging Iranian oil tankers falls within the scope of sanctionable activity under that Executive Order. In addition, if Tanzania were to allow Iranian vessels to remain under Tanzanian registry, we in the Congress would have no choice but to consider whether to continue the range of bi-lateral U.S. programs with Tanzania.

Sincerely,

Howard Berman
Ranking Democrat, House Foreign Affairs Committee
Thus, spoke Zarathustra!
 
Hapa Marekani ataja singiziwa bure bure...Tayari nchi iko katika ukingo wa mabadiliko ya nguvu ya umma. Mgomo wa madaktari, Failed assasination plot ya Ulimboka, uvamimizi wa Oil Com (Rit 1) kwa nyumba za wananchi Tegeta, Bajeti inayodidimiza kabisa hata tumaini dogo kwa mtu wa kawaida kiuchumi, Matatizo ya bodi ya mikopo, Njama za watawala kumwua mbunge wa Ilemera, Scandal ya wizi wa fedha wizara ya mambo ya nje, meli za iran kutembea kwa hifadhi ya serkali ya Tanzania........Haya yote yatajatwikwa kwa Marekani lakini ni magonjwa ya kujitakia!!! EE Mungu tunasuru katika mikono ya watawala dhalimu watesaji na wauaji wa watu wao wenyewe!!!
 
...mmmmh, this saga gonna be an overwhelming stinker over "our TANKED marashi ya karafuu" and the union gov overall!!! 'Coz I don't see how serikali ya mapinduzi Zenj would back down na kuacha kusajili meli za nje, i.e Iran, knowing the ties between the two... But on the other hand, JMT nayo itakuwa katika songombinde just to protect her interests, i.e. misaada. Taking into consideration recent deals at the G8!! We heading towards collision...

Ni kuvunja muungano tu ndo soln. Kumbe sio kikwete ni serikali ya mapinduzi. Ndio juzijuzi nilisikia kuna baraza la usalama, mie nilifikiri ni kwa sababu ya Dr Uli, kumbe ni hili sakata.
 
Kikwete DHAIFU na Serikali yake DHAIFU wanastahili kuondoka madarakani si kwa kuwachokoza Marekani bali kwa kushindwa kuiongoza nchi na kuwaachia mafisadi wakiendelea kupeta huku maisha ya Watanzania walio wengi yakiendelea kuwa ya dhiki kubwa na ya kutisha.

angalikuwa lukuvi ni mod angekuambia toka nje.
na hali akijua usemalo ni kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaa udhaifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu ndio unaopeleka taifa pabaya
 
masikini watanzania tunadhani tuna serikali kumbe tuna sirikali tu zinazoendesha maisha yetu.
 
Zanzibar ni taifa huru ndani ya jamhuri ya muungano, haipaswi kuanzia rais wa muungano, wazir wa muungano na viongozi wengine wowote kuingilia zanzibar kwenye mambo yake kama imesajili meli ndio ni haki yake. mambo haya ya kuendeleza kuendeshwa na wakoloni yamepitwa na wakati, kwa ushaur ningependa kumskia rais wetu akitoa tamko kwa hili.

Taifa huru ni kweli, si wangeweka bendara yao, siku hizi si wanayo?
 
hii ndio serikali ya kikwete ya chama cha mapinduzi na hapa ndipo ilipofikisha taifa unaweza kupima kwa akili ya kawaida tu tunaelekea wapi
 
Kikwete avunje muungano, maana wazanzibar bila hivyo watampapasa pabaya.
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.

Kama tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao, kwa nini huo uamuzi usianze leo?
Pili, katika dunia ya leo Tanzania sio kisiwa - zipo kaida za kimataifa ambazo lazima izizingatie ipende isipende. Ni sawa na wewe leo hii huwezi kuamua kutembea uchi mbele ya hadhara kwa vile tu una uhuru wa kujiamulia ulitakalo!!!
 
Wakuu mambo yanasonga mbele. Mkulu kakaliwa kooni, naona safari za USA zinaota majani. Tumechoka na kodi zetu kutumiwa vibaya, hawakujua JK ni ndumilakuwili? Hataki DIASPORA wale huku na kule wakati yeye anakula na Iran na wamarekani? Tuone sasa nani mwenye nguvu, JK na mafisadi wake au wamarekani.... matonya sijui unanipta na bakuli lako?

********************************************

Dear President Kikwete,
I am writing to express my deep dismay that Tanzania has permitted the National Iranian Tanker Company (NITC), to reflag at least 6 and as many as 10 of its vessels under the Tanzanian ship registry, allowing them to remain under NITC ownership and continuing to transport Iran's crude oil exports. This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research programs and its support for international terrorism.

It is profoundly disappointing to me to learn that your government has acted in contravention of the broad international coalition that is working together to use peaceful means, including economic sanctions, to change the threatening behavior of the Iranian regime. The decision to accept the re-flagging of NITC vessels casts a shadow over Tanzania's international reputation.

I respectfully request that Tanzania cancel the re-flagging of the NITC vessels. Given the close and cooperative relationship that our two governments now enjoy, it would be unfortunate if this action were permitted to stand.

It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord. However, your government should take note of President Obama's Executive Order 13608, signed May 1, 2012, which provides for the imposition of sanctions on any entity worldwide, including foreign governments, that assists Iran in evading U.S. sanctions. In my view, reflagging Iranian oil tankers falls within the scope of sanctionable activity under that Executive Order. In addition, if Tanzania were to allow Iranian vessels to remain under Tanzanian registry, we in the Congress would have no choice but to consider whether to continue the range of bi-lateral U.S. programs with Tanzania.

Sincerely,

Howard Berman
Ranking Democrat, House Foreign Affairs Committee

Source
http://democrats.foreignaffairs.house.gov/press_display.asp?id=976
 
Kumbe huyu mcheza ngoma kawapa nembo yetu wa irani inasikitisha sana ila kwa agizo la wanaomfadhili atafyata mkia penda usipende, get well soon ulimboka
 
Tunapomwambia kaa chini tumia wataalamu wetu kwenye kuongeza pato la taifa,tunapomwambia acha kuuza madini yetu kwa bei za kutupwa,tunapomwambia pandisha kodi za madini huwa hasikii ,ona sasa anavyodharauliwa our head of state anaandikwa barua ya onyo kali na ofisa katika wizara na si Secretary of State kwa mfano Hilary Clinton,ghiriba zake za kutaka huku na huku zitamtokea puani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom