Tanzania na Kilimo cha Mtandaoni: Je, Waziri Bashe anaifahamu jamii ya wakulima Tanzania?

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,

Leo nimeona sio mbaya kujadili mada hii,

NBS inaonesha karibia 65% ya Watanzania wanajihusisha na kilimo. Kilimo cha kujikimu na kiasi kidogo kubadilishia mboga. Tukichanganya ufugaji na uvuvi kama sehemu ya kilimo (maana karibu wate hawa ni wabangaizaji) basi ni 83%. Sasa maswali ninayojiuliza;

1. Je, hawa ndio Waziri anahangaika nao? Au yuko bize na wale vijana wa Kinondoni wanaosafisha ekari moja kwa milioni 15?

2. Je, hawa ndio Mh. Rais wetu mpendwa Mama Samia atakutana nao kesho? Au atakutana na wakulima wa Instagram, FB na WhatsApp?

3. Je, tunaelewa hili ndio kundi likiendelezwa linaweza kuzalisha ajira na kuongeza urali wa Biashara kimataifa kuliko kundi jingine lolote? Au tunawaangalia hawa wa WhatsApp waliojazana hapa viwanja vya Maonesho Mwakangale Mbeya?

4. Je, tumetekeleza kwa kiasi gani ASDP (Agricultural Sector Development Programme) huu ndio mpango wa kitaifa.

5. Je, hawa asilimia 65 ndio wataguswa na zile bilioni 360 za AFDB? Au zile zitaenda kwa hawa wa kinondoni?

Maswali ni mengi lakini naona Wizara inabangaiza, Serikali inabangaiza, pale Mwakangale wamejaa wasanii.

Turudie sera zetu. Tunaangamiza nchi.

Karibu Mbeya Rais wetu. Tupige picha na kukagua tembele na ng'ombe ambae huwezi jua anapatikana wapi Umasaini, Usukumani, au Ukuryani.
 
Kilimo cha instagram anashindwa kujiuliza Russia wanawezaje kugawa Grain Africa bure tena ya kutulisha Tanzania Mwaka mzima.
 
Wakulima wa WhatsApp wapo sana, hata huku kwangu kuna dada namfahamu kabisa! Alipewa tuzo ya kuwa kijana mkulima bora mwaka huu

🤣🤣🤣 kwanza hana shamba na hajui kushika jembe, lakini ndo aliyechukua tuzo ya kijana mkulima bora!
 
Kuna swali moja kwenye geography paper 2 linauliza prairies of canada are granaries of the world.Discuss. Nachotaka kusema hapa sioni mpango mkakati wa muda mrefu wa kuinua kilimo tz zaidi ya political propaganda. Wakajifunze huko texas au oklahoma au huko nevada, wisconsin na midwestern states za marekani jinsi kilimo kinavyofanywa siriazi.
 
Mkuu tumekuja kuonesha umahiri wako wa misamiati au kuchangia thread hii??
 
Mkuu tumekuja kuonesha umahiri wako wa misamiati au kuchangia thread hii??
Hapo nimechangia. sasa unataka kupanga mada ichangiwaje labda kwa mfano? Umeona nime mtukana mtu? Au kosa ni kuweka mifano?

Usikwazike na mambo madogo madogo. Anyway basi tuseme kama gavoo ina nia ya dhati kuwa siriazi na kilimo mojawapo ifufue mashamba yale ya ngano kule mbulu.
 
Karibu Mbeya Rais wetu. Tupige picha na kukagua tembele na Ng'ombe ambae huwezi jua anapatikana wapi Umasaini, usukumani, Ukuryani.
Nipo pamoja sana nawe katika andiko lako, kasoro pengine kwenye msisitizo wa mambo kadhaa wa kadhaa.

Kwa mfano, mimi ningewashukuru sana hawa akina Samia na Bashe, kama mkazo wao ungejikita zaidi kwa hao asili mia 65, ongeza na hawa uliowataja wa huko Usukumani, umasaini, Ukuryani, kuondokana na kufanya kazi zao kitamaduni, kwa mazoea.
Huyo mkulima anayejipinda kwenye eka yake moja au mbili aweze kuzalisha mara dufu ya anachozalisha sasa hivi.
Huyo mfugaji, wa kutangatanga kila sehemu kutafuta marisho, huyo siyo mfugaji endelevu; aelimishwe na apewe fursa ya kubadili namna ya ufugaji anaoufanya sasa hivi, huku akipata matokeo makubwa zaidi katika kazi yake hiyo, bila ya kuvuruga mazingira na kuleta athari nyinginezo zinazotokana na ufugaji unaofanyika sasa hivi.

Ninakubalaiana nawe, Samia na Bashe siyo viongozi wanaoweza kuleta mabadiliko ya aina hiyo, kwa sababu hawana uwezo wa uongozi wa kufanya hivyo.
 
Wakulima wa WhatsApp wapo sana, hata huku kwangu kuna dada namfahamu kabisa! Alipewa tuzo ya kuwa kijana mkulima bora mwaka huu

🤣🤣🤣 kwanza hana shamba na hajui kushika jembe, lakini ndo aliyechukua tuzo ya kijana mkulima bora!
Ungetuwekea picha ingependeza sana.
Nimejaribu sana kuichora hiyo picha kichwani mwangu, ikashindikana kabisa!
 
Wakulima wa WhatsApp wapo sana, hata huku kwangu kuna dada namfahamu kabisa! Alipewa tuzo ya kuwa kijana mkulima bora mwaka huu

🤣🤣🤣 kwanza hana shamba na hajui kushika jembe, lakini ndo aliyechukua tuzo ya kijana mkulima bora!
Kilimo cha Instagram kina mambo sana
 
Kuna swali moja kwenye geography paper 2 linauliza prairies of canada are granaries of the world.Discuss. Nachotaka kusema hapa sioni mpango mkakati wa muda mrefu wa kuinua kilimo tz zaidi ya political propaganda. Wakajifunze huko texas au oklahoma au huko nevada, wisconsin na midwestern states za marekani jinsi kilimo kinavyofanywa siriazi.
Dah!

Maswali ya namna hii bado yanaulizwaga enzi hizi?

Mkuu 'mcTobby' mifano yako ya Canada, Texas au Oklahoma au Nevada, siyo mifano halisi inayoweza kufanyika Tanzania.

Maeneo hayo yote uliyoyataja, sehemu kubwa zipo wazi kwa shughuli za kilimo cha kujitanua wapendavyo wakulima wenyewe.

Sisi hapa, kwa ujinga wetu, nasi bado tunadhani tunayo maeneo makubwa sana ya wakulima kujitanua kwa kilimo cha biashara kama kinavyofanyika huko.
Watu wanasahau kwamba hivi vieka tunavyogawiana sasa, miaka siyo mingi, kutakuwa na watu, tukibanana wenyewe kwa wenyewe, maana hata sioni mipango ya serikali kutupanga vizuri wengi wetu tukabanane mijini kupisha shughuli za kilimo na maswala mengine.

Lakini, pamoja na hayo niliyoandika hapo juu, mimi ningetumia mfano wa Israel, au Egypt, au hata China yenyewe; ya kwamba tunatumia eneo dogo tulilonalo la ardhi, na kulitumia vizuri zaidi ili tupate mafao makubwa kutokana na hicho kilimo.
Hili kwa hapa Tanzania tukijipanga vizuri, bado ardhi ya kutosha kabisa ipo.

Nikirudi kwenye swali lako la Jiografia: Huyo mwalimu aliyetunga swali hilo alikuwa ni mawlimu mvivu sana. Huyu ni mwalimu anayekaririsha wanafunzi wake watapike yale aliyowanywesha. Wakitoka tu nje ya mstari wake, na kutumia akili yao kufikiri, tayari atakuwa kishawanasa na kuwafelisha mtihani.
Ninajua ninachozungumzia hapa. Sibahatishi.
 
Back
Top Bottom