Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Profesa Shaba ali import vifaa kabisa nadhani mpaka leo 30 years later bado viko bandarini.
Alipata upinzani na ukiritimba mkubwa sana kutoka serikali pendwa.
Nilishasikia hii kitu. Mpaka mwekezaji aliyekua patna na shaba akaondoka nchini akasusa na project yenyewe. Sijui kama kuna ukweli au la
 
Kuna mji fulani hospitali haina hiyo watu wakifa mait inalazwa chini au ipelekwe umbali wa zaid kilomita 25 kuifadhiwa kisha ifuatwe cku ya mazishi sasa nikamshauli mdogo wangu afanye biashara hiyo alikataa na hata alipowaambia watu ktk familia walikataa kabisaaa
 
Wabongo tuna uoga fulani wa ajabu hivi...!!
Wakati ni kitu kizuri kabisa, tena kwa wale waamini unapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu, maana unashiriki kitu muhimu sana katika kuupatia hifadhi na heshima inayostahili mwili wa binadamu mara baada ya roho kuachana na mwili. Haina ubaya wowote. Basi tu mawazo ya watu.
 
Zipo kuna sehem ilikuwepo wakahamia sehem flan hiyo nyumba hadi leo haipati wapangaji tetesi ni imeuzwa tena ilikua karibu na kituo kikubwa cha radio...

Ilikua ni mortuary na Pia wanafanya maandalizi ya msiba nk
Karibu na mawingu?
 
Wadau hivi Bongo ukiachana na Mortuary zilizopo ndani ya hospitali, Mbona hakuna Mortuary ambazo Mtu/Kampuni zinamiliki private? i.e high class/ VIP mortuary?

Mfano kwa wenzetu Kenya, hii fursa watu wameitumia kweli kweli na kuna private mortuaries nyingi tu watu wamezitengeneza, na wengi wanazitumia huduma hizo pale wanapofikwa na janga la msiba kwenye familia zao.

Kwa shida ya upungufu na ubora hafifu wa vyumba vya mortuary kwa hospitali nyingi ninayoiona kwenye hospitali nyingi za bongo, hii inaweza kuwa biashara nzuri tu bongo na ikalipa vizuri tu, kama watu wenye uwezo wakiwekeza huko.

Ni watu hawajaiona hiyo fursa au wabongo hawataweza kuzilipia?

Au taratibu zetu za kisheria haziruhusu? Kama sheria zetu haziruhusu, zifanyiwe marekebisho ziruhusu hilo, ni fursa nzuri sana. Watu watapata pesa na serikali itapata kodi.
Mbonq mortuary zipo nying sana za jumuiya nje ya government kama dar misikiti mikubwa karibu yote zina mortuary temeke kina masjid alqadiria kariakoo kuna manyema mtoro upanga kuna maanur town kuna masjid jabir bin zaid na magomen pia kuna masjid nying zina huduma hizo ilala pia
 
Pale Himo, Moshi nimewahi kuona Private hospital moja ina mortuary yake nzuri tuu na huduma safi kabisa,sema siyo kubwa sana.
 
Mleta mada wewe ni katili. Nyinyi ndo watu mnaomba kila wakati watu Wafe biashara zenu zichanganye
Mkuu vipi tena kuniita katili hata hunijui?
Kwa hiyo wauza majeneza nao ni makatili? Wao wanapata faida pale watu wanapofariki na kutoa huduma ya majeneza.
Na madaktari wa binadamu pia ni makatili? Maana wao watu wanavyoumwa ndo wao wanapata faida.
Mawakili je? Wao nao makatili, maana watu tusipoibiwa, tusipotapeliwa, tusipobakwa watapata wapi faida?
Mkuu ukiangalia maisha kwa namna hiyo basi watu wengi sana hapa duniani ni makatilil.
Look at it this way: Mtu anatoa huduma ya mortuary ili kuwezesha pale ambapo mtu amefariki basi aweze kuhifadhiwa kwa heshima na kwa stahiki inayotakiwa.
 
Mbonq mortuary zipo nying sana za jumuiya nje ya government kama dar misikiti mikubwa karibu yote zina mortuary temeke kina masjid alqadiria kariakoo kuna manyema mtoro upanga kuna maanur town kuna masjid jabir bin zaid na magomen pia kuna masjid nying zina huduma hizo ilala pia
Ok. Hii nilikua sijui mkuu kiukweli. Kumbe misikiti mikubwa Dar wana mortuary zao kabisa ambapo wanai-treat na kulaza miili ya marehemu? Nitajaribu kutembelea kwenye msikiti mmojawapo nijifunze pia.
Shukrani.
nanawoo
 
Pale Himo, Moshi nimewahi kuona Private hospital moja ina mortuary yake nzuri tuu na huduma safi kabisa,sema siyo kubwa sana.
Yeah, kwenye hospitali mortuary zipo... Sema ndo hivyo hazikidhi mahitaji kama ulivyosema hiyo ambayo umeitaja ni ndogo. Ndio maana nikawaza kuwa na kitu cha private kwa huduma hiyo tuu! (siyo hospitali, bali mortuary room tu).
 
Back
Top Bottom