Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Wadau hivi Bongo ukiachana na Mortuary zilizopo ndani ya hospitali, Mbona hakuna Mortuary ambazo Mtu/Kampuni zinamiliki private? i.e high class/ VIP mortuary?

Mfano kwa wenzetu Kenya, hii fursa watu wameitumia kweli kweli na kuna private mortuaries nyingi tu watu wamezitengeneza, na wengi wanazitumia huduma hizo pale wanapofikwa na janga la msiba kwenye familia zao.

Kwa shida ya upungufu na ubora hafifu wa vyumba vya mortuary kwa hospitali nyingi ninayoiona kwenye hospitali nyingi za bongo, hii inaweza kuwa biashara nzuri tu bongo na ikalipa vizuri tu, kama watu wenye uwezo wakiwekeza huko.

Ni watu hawajaiona hiyo fursa au wabongo hawataweza kuzilipia?

Au taratibu zetu za kisheria haziruhusu? Kama sheria zetu haziruhusu, zifanyiwe marekebisho ziruhusu hilo, ni fursa nzuri sana. Watu watapata pesa na serikali itapata kodi.
Mbona Corona wana mortuary yao?
 
Mi wazo zuri Sana maana mortuary ni zaidi ya kuhifadhi maiti kuna huduma za uchunguzi,utafiti, maandalizi yamazishi hata mafunzo pia itaongeza uwanja wa ajira or medical examiners
 
Hahahahaha!

Hii nayo ni point nzuri mkuu. Ila mtanilaliaje? Kuingiza mwili hadi mtoe pesa, sio bure bure tu.

Mtu anaweza kuanzisha huduma hii aka target middle income eaners maeneo ya mjini kama Dar- Na akaweka huduma na bei ambazo ni za katikati (sio za juu sana). Anaweza kupata mid-income eaners wengi wafanyakazi na wafanyabiashara wa kati ambao watapenda kuhifadhi wapendwa wao kiheshima zaidi.

Au pia anaweza kutarget high income eaners wale matyta wa mjini hapa. The likes wanaotibiwa Aga Khan na zinazofanana na hizo.
Sio kwamba kitu kama hii mtu akajenge Sitimbi
Hii fursa mnaijadili hapa naamini kuna mtu ataifanyia kazi muda si mrefu.au inawezekana kuna mtu yupo tayari kwenye process ya kuifanyia kazi

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hahahahahahaha!

Sio ubepari mkuu. Ni huduma tu ya kawaida. Unajua kuhifadhi mwili ni gharama sana mkuu? Kuna treatment mwili unatakiwa kufanyiwa ili usioze, unatakiwa uwekwe sehemu baridi pia (refridgerator), vyote hivi ni gharama, usitegemee iwe ni huduma ya bure mkuu.
Tena unaweka na solar system unapata faida iliyonyooka kbsa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mi wazo zuri Sana maana mortuary ni zaidi ya kuhifadhi maiti kuna huduma za uchunguzi,utafiti, maandalizi yamazishi hata mafunzo pia itaongeza uwanja wa ajira or medical examiners
Ni kweli kabisa mkuu... Umeiweka vizuri haswa!
Hata huduma za autopsy, post moterm, cadaver preparations, etc.
ni uwanja mpana haswa!
 
Ni wazo zuri ila kuna mambo yasiyofaa yatafanyika huko, tujifunze kutoka kwenye ubinafsishaji mwingine uliofanyika huko nyuma, possibly wawekezeji namba moja watakuwa ni hao wafanyakazi wa mochuari wa sasa
Sio lazima wawe wao unaweza ukaanzisha ukawaajiri km part time yaani anafanya kazi hospital akitoka anaunganisha shift nyingine kwenye ofisi yako km madaktari wanavyofanya

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hii fursa mnaijadili hapa naamini kuna mtu ataifanyia kazi muda si mrefu.au inawezekana kuna mtu yupo tayari kwenye process ya kuifanyia kazi

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Nakubaliana na wewe asilimia 100.
Kuna kipindi fulani nilikua nimewaza na kufanyia utafiti kuhusu fursa ya kuwekeza kwenye uuzaji wa maji kwenye eneo fulani ambalo lilikua na shida sana ya maji.Sema nilikua sijakaa vizuri financially, kwa hiyo sikua na huo mtaji, na ni idea ambayo ilihitaji kiasi kama cha milioni 7 minimum kuitekeleza. Nikawa najipanga sasa nichukue mkopo sehemu fulani nianze utekelezaji.
Ndani ya muda wa miezi mitatu, kuna jamaa akaja kutekeleza yaani karibu kila ambacho niliwaza kuhusu ile idea kwa asilimia 90. Jamaa hadi sasa anaendelea na mradi fresh tu, anakula vichwa balaa!! Nikasema kweli ukiwaza kuhusu idea fulani usidhani kuwa peke yako ndo umewaza hilo.
 
Sio lazima wawe wao unaweza ukaanzisha ukawaajiri km part time yaani anafanya kazi hospital akitoka anaunganisha shift nyingine kwenye ofisi yako km madaktari wanavyofanya

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Sawa kabisa mkuu. Na pia kinachotakiwa ni kuweka standards tu na usimamizi wa kutosha (CCTV cameras, monitoring visits, uwepo wa miongozo ya ufanyaji kazi kwa weledi, etc).
Hii itahakikisha kuwa kila kitu kinafanyika kwa weledi mkubwa, na iwapo kunatokea uvunjwaji wa maadili na miiko ya kazi basi hatua stahiki zinachukuliwa kwa haraka.
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100.
Kuna kipindi fulani nilikua nimewaza na kufanyia utafiti kuhusu fursa ya kuwekeza kwenye uuzaji wa maji kwenye eneo fulani ambalo lilikua na shida sana ya maji.Sema nilikua sijakaa vizuri financially, kwa hiyo sikua na huo mtaji, na ni idea ambayo ilihitaji kiasi kama cha milioni 7 minimum kuitekeleza. Nikawa najipanga sasa nichukue mkopo sehemu fulani nianze utekelezaji.
Ndani ya muda wa miezi mitatu, kuna jamaa akaja kutekeleza yaani karibu kila ambacho niliwaza kuhusu ile idea kwa asilimia 90. Jamaa hadi sasa anaendelea na mradi fresh tu, anakula vichwa balaa!! Nikasema kweli ukiwaza kuhusu idea fulani usidhani kuwa peke yako ndo umewaza hilo.
True chief

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom