Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

shida ipo mtu kafia hospital mnamuamisha kwenda private mortuary
Mtu kufia hospitali haimaanishi kuwa ni lazima kwamba mwili wake uhifadhiwe hapo. Bado mnaweza kufanya taratibu mkaondoka na mwili na kisha kwenda kuuhifadhi kwenye a private mortuary kama mkitaka hivyo. Ila pia mkuu, kuna watu wengi tu wanafia kwenye hospitali/vituo vya afya ambavyo havina mortuary, hii pia huwa inatokea. Au mtu anafia hospitali yenye mortuary ila mnaambiwa kwa wakati huo imejaa, kwa hiyo mnaambiwa mchukue mwili labda muuepeleka mortuary ya Muhimbili au mortuary ya hospitali nyingine yoyote kubwa. Hapa sasa pia mnaweza kuamua kuupeleka mwili private mortuary.
Changamoto ambayo naiona itabidi kupambana nayo ni namna ya kuitangaza au kuifanya ijulikane... Maana kwa response niliyoiona hapa inaonekana Watanzania wengi wako so negative about this. Ila, mtu akianzisha na akapata namna tu ambayo ikafanya ikajulikana (mfano kwa kuestablish links na hospitali/vituo vya afya binafsi ambavyo havina mortuary, au kuingia mkataba nazo kwamba ikitokea mgonjwa amefariki, basi wanamleta kumhifadhi hapo kwako then wao wanapata percent fulani na wewe unapata percent fulani kulingana na makubaliano mtakayofikia, etc), kutusua ni rahisi.
 
Profesa Shaba ali import vifaa kabisa nadhani mpaka leo 30 years later bado viko bandarini.
Alipata upinzani na ukiritimba mkubwa sana kutoka serikali pendwa.
Duuhhh...!! Ukiritimba wa ajabu kabisa aisee!!
Hope sasa hivi labda mambo yatakua yamebadilika. Naendelea kufuatilia zaidi na kujifunza.
 
Zipo kuna sehem ilikuwepo wakahamia sehem flan hiyo nyumba hadi leo haipati wapangaji tetesi ni imeuzwa tena ilikua karibu na kituo kikubwa cha radio...

Ilikua ni mortuary na Pia wanafanya maandalizi ya msiba nk
Okaay.
Hii sijawahi kuisikia aisee. Funguka zaidi ipo maeneo gani au owner ni nani ili niweze kufuatilia zaidi.
 
Mtu kufia hospitali haimaanishi kuwa ni lazima kwamba mwili wake uhifadhiwe hapo. Bado mnaweza kufanya taratibu mkaondoka na mwili na kisha kwenda kuuhifadhi kwenye a private mortuary kama mkitaka hivyo. Ila pia mkuu, kuna watu wengi tu wanafia kwenye hospitali/vituo vya afya ambavyo havina mortuary, hii pia huwa inatokea. Au mtu anafia hospitali yenye mortuary ila mnaambiwa kwa wakati huo imejaa, kwa hiyo mnaambiwa mchukue mwili labda muuepeleka mortuary ya Muhimbili au mortuary ya hospitali nyingine yoyote kubwa. Hapa sasa pia mnaweza kuamua kuupeleka mwili private mortuary.
Changamoto ambayo naiona itabidi kupambana nayo ni namna ya kuitangaza au kuifanya ijulikane... Maana kwa response niliyoiona hapa inaonekana Watanzania wengi wako so negative about this. Ila, mtu akianzisha na akapata namna tu ambayo ikafanya ikajulikana (mfano kwa kuestablish links na hospitali/vituo vya afya binafsi ambavyo havina mortuary, au kuingia mkataba nazo kwamba ikitokea mgonjwa amefariki, basi wanamleta kumhifadhi hapo kwako then wao wanapata percent fulani na wewe unapata percent fulani kulingana na makubaliano mtakayofikia, etc), kutusua ni rahisi.
apa nimekuelewa
 
Dah hapana.
Kuchimba makaburi,kutengeneza masanduku na hyo unayosema
Inataka moyo
Kwa nini mkuu? Mbona ni huduma tu mkuu kama huduma zingine? Wote tutakufa, hilo wala si jambo la shaka.
Ni kama huduma ya wanaotengeneza na kuuza majeneza tu mkuu. Wanasaidia jamii (wahitaji), na pia wanapata namna ya kuendesha maisha yao. Kwa nini watu wengi mmekua na uoga sana juu ya hii huduma?
 
Wadau hivi Bongo ukiachana na Mortuary zilizopo ndani ya hospitali, Mbona hakuna Mortuary ambazo Mtu/Kampuni zinamiliki private? i.e high class/ VIP mortuary?

Mfano kwa wenzetu Kenya, hii fursa watu wameitumia kweli kweli na kuna private mortuaries nyingi tu watu wamezitengeneza, na wengi wanazitumia huduma hizo pale wanapofikwa na janga la msiba kwenye familia zao.

Kwa shida ya upungufu na ubora hafifu wa vyumba vya mortuary kwa hospitali nyingi ninayoiona kwenye hospitali nyingi za bongo, hii inaweza kuwa biashara nzuri tu bongo na ikalipa vizuri tu, kama watu wenye uwezo wakiwekeza huko.

Ni watu hawajaiona hiyo fursa au wabongo hawataweza kuzilipia?

Au taratibu zetu za kisheria haziruhusu? Kama sheria zetu haziruhusu, zifanyiwe marekebisho ziruhusu hilo, ni fursa nzuri sana. Watu watapata pesa na serikali itapata kodi.
Sidhani kama sheria haziruhusu, no WaTz wenyewe tu na uzito wetu wa kuchangamkia fursa.
 
Haitishi mkuu. Ni huduma inayohitajika, ukizingatia kuwa hospitali zetu kwa kweli hazikidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa ubora na wingi. Kenya iko regulated vizuri, na inafanya vyema tu.

Cheki hapa chini kwenye link, moja ya kampuni inayotoa huduma ya private mortuary Kenya huko. Very lucrative!

Mkuu tuanzishe funeral home yetu tutapiga hela balaa

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Unajua bei ya zile jokofu za 4 in one? Si chini ya 50,000,000 kaka
Halafu mkuu nimecheki hapa mtandaoni mbona hata sio expensive kihivyo? Naona bei zake hazijafika huko ulikosema wewe mkuu..... Au labda zina kodi kubwa sana? Ila no way zitafika huko. Nimecheki mfano la kabati 6 ni kama dola 2,000 ambayo ni around 5milion hivi (maximum). Cheki hizi screenshots. penadu

Screenshot_20210513-201920.png

Screenshot_20210513-201927.png
 
Nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
Fungu la10 tena duh hatari
 
Back
Top Bottom