Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Natambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha barabara zetu. Najua ni jukumu linalogharimu fedha nyingi sana.
Wazo langu la leo ni kuangalia jinsi gani tunaweza kuipunguzia mzigo huu serikali bila kuingia katika madeni yoyote. Huku ninapoishi niko kandokando ya barabara kubwa na kuna majumba yanayoonyesha wakazi wake ni watu wenye uwezo fulani ila cha kushangaza gharama kubwa zinatumika mara kwa mara kuikwangua tu na si kuiweka katika kiwango cha lami.
Wazo langu linasema, kwa nini serikali isiweke utaratibu ili mtu, kikundi cha watu au makampuni binafsi watakaotaka kujitolea kujenga barabara yoyote, waruhusiwe kufanya hivyo huku wakifuata taratibu zote ikiwemo za kutumia makampuni ya ujenzi yanayotambulika. Baada ya hapo, barabara hiyo ipewe jina atakalopendekeza huyo mtu/kikundi cha watu/kampuni labda kwa muda fulani, mfano kwa miaka 20. Kuwe pia na utaratibu maalumu unaoeleweka ili majina ya ajabuajabu yasije kuanza kutumika katika barabara hizo.
Tunaweza hata kuweka nyongeza ya unafuu fulani ya kodi kwa wale watakaotaka kufanya hivyo kwa sababu jina tu linaweza lisitoshe kuvutia wengi.
Kitu ambacho serikali inaweza kufanya kusukuma hili wazo ni kuzitambua barabara na mitaa ambayo ni kipaumbele na kutoa hiyo orodha katika tangazo rasmi. Kampeni kubwa ifanyike kwa matangazo ya televisheni, mabango, nk. ili makampuni na watu binafsi watambue fursa hii.
Wazo hili litasaidia sana kuharakisha ujenzi wa barabara hizi ambazo ki ukweli kuisubiri serikali itachukua muda mrefu sana.
Nawasilisha.