Tanzania Inajipanga Kuacha Kutumia Fedha za Kigeni Kuagiza Mafuta Nje ya Nchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI - TANZANIA INAJIPANGA KUACHA KUTUMIA FEDHA ZA KIGENI KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

SERIKALI imekutana na wadau wa kuzalisha Mafuta ya kupikia kwa ajili ya kujadili changamoto zinazosababisha kushuka kwa bei ya Mafuta ya Alizeti nchini.

Katika kikao kilichofanyika tarehe 23 Mei, 2023 kilichowakutanisha Mawaziri kutoka Wizara tatu; Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji; Waziri wa Kilimo, Mhe. Husssein Bashe na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.

Akifungua kikao hicho Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema lengo la kikao hicho ni kuongea kwa pamoja, kuboresha maisha, kuchangia Uchumi wa Taifa na hatimaye kuzalisha Mafuta ambayo yatajitosheleza na hivyo kuachana na kutumia fedha za kigeni kuagiza mafuta nje ya nchi.

Amesema kuwa kwa sasa Alizeti imeshuka kwa asilimia 50 na Mafuta ya kupikia kwa asilimia 17 jambo ambalo limepelekea wananchi hususani wakulima kuwa na malalamiko hivyo Serikali ikaona wajadiliane na kwenda pamoja .

"Tuna Viwanda 771 vinavyochakata Mafuta, tunazalisha Tani laki tatu na mahitaji yetu ni Tani laki tano na Sitini, hivyo Mafuta bado hayatoshi hali inayopelekea kuruhusu wenzetu welete kutoka nje ya nchi na kupitia hali hiyo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akaelekeza tuwe na Mikoa mitatu ya Kilimo cha Alizeti ndani ya Taifa letu ambayo ni Dodoma, Singida na Simiyu lengo ni kutafuta Malighafi ya kutosha" - Mhe. Dkt. Kijaji.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa ili kuondokana na changamoto hiyo kuna haja ya kutengeneza Sera ya kuwakuza kiuchumi na kwamba ndani ya miaka mitatu Serikali haitaagiza mafuta nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa wazalishaji wa mafuta wanapaswa kukutana wao kukaa kwa pamoja kuchagua uongozi mzuri ambao utawasaidia kuwaunganisha na serikali.

Aidha, washiriki hao akiwemo Nelson Mwakabuta Meneja wa Kampuni ya Mount Meru Millas na Fatuma Salum mzalishaji wamesema kuwa wamefurahishwa na kikao hicho na wana uhakika changamoto zilizowakabili ikiwemo upungufu wa Malighafi na Masoko yanaenda kupatiwa ufumbuzi.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.33.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.33.jpeg
    32.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.34(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.34(1).jpeg
    20.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.34(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.34(2).jpeg
    22 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.36.jpeg
    29.4 KB · Views: 3

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI - TANZANIA INAJIPANGA KUACHA KUTUMIA FEDHA ZA KIGENI KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

SERIKALI imekutana na wadau wa kuzalisha Mafuta ya kupikia kwa ajili ya kujadili changamoto zinazosababisha kushuka kwa bei ya Mafuta ya Alizeti nchini.

Katika kikao kilichofanyika tarehe 23 Mei, 2023 kilichowakutanisha Mawaziri kutoka Wizara tatu; Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji; Waziri wa Kilimo, Mhe. Husssein Bashe na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.

Akifungua kikao hicho Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema lengo la kikao hicho ni kuongea kwa pamoja, kuboresha maisha, kuchangia Uchumi wa Taifa na hatimaye kuzalisha Mafuta ambayo yatajitosheleza na hivyo kuachana na kutumia fedha za kigeni kuagiza mafuta nje ya nchi.

Amesema kuwa kwa sasa Alizeti imeshuka kwa asilimia 50 na Mafuta ya kupikia kwa asilimia 17 jambo ambalo limepelekea wananchi hususani wakulima kuwa na malalamiko hivyo Serikali ikaona wajadiliane na kwenda pamoja .

"Tuna Viwanda 771 vinavyochakata Mafuta, tunazalisha Tani laki tatu na mahitaji yetu ni Tani laki tano na Sitini, hivyo Mafuta bado hayatoshi hali inayopelekea kuruhusu wenzetu welete kutoka nje ya nchi na kupitia hali hiyo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akaelekeza tuwe na Mikoa mitatu ya Kilimo cha Alizeti ndani ya Taifa letu ambayo ni Dodoma, Singida na Simiyu lengo ni kutafuta Malighafi ya kutosha" - Mhe. Dkt. Kijaji.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa ili kuondokana na changamoto hiyo kuna haja ya kutengeneza Sera ya kuwakuza kiuchumi na kwamba ndani ya miaka mitatu Serikali haitaagiza mafuta nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa wazalishaji wa mafuta wanapaswa kukutana wao kukaa kwa pamoja kuchagua uongozi mzuri ambao utawasaidia kuwaunganisha na serikali.

Aidha, washiriki hao akiwemo Nelson Mwakabuta Meneja wa Kampuni ya Mount Meru Millas na Fatuma Salum mzalishaji wamesema kuwa wamefurahishwa na kikao hicho na wana uhakika changamoto zilizowakabili ikiwemo upungufu wa Malighafi na Masoko yanaenda kupatiwa ufumbuzi.
Huyu waziri sijawahi kumuelewa, naomba team yake mnisamehe
 
Yan sina hamu mwaka jana walituhamasisha kulima alizeti saana, ila saiv wameondoa kodi kwa waagizaji wa mafuta nje bei imeporomoka.........mkulima wa alizeti yeyote tanzania saiv ni kufukuzana na hasara tu

Bora wangesema wataondoa kodi za matajir wanaoagiza mafuta, ili tusingejichosha kulima alizeti. Kwa hali hii hakuna mkulima atakaerudi mwakani kulima alizeti, maana hasara ni kubwa mno na kama mtu alichukua mkopo kazi ipo

Ushauri wa haraka: serikali ipandishe kodi haraka kwa mwaka huu kunusuru hii hali

Cha mwisho na muhimu: kwa mkulima ukija kuona zao linahamasishwa kulimwa kwa nguvu na wanasiasa usijiloge ukaingia, utalia kilio cha mbwa koko
 
Kwahiyo kiongozi soko lilikuwepo lakini bei ikawa imeshuka kutokana Na kuingia kwa mafuta ya nje?
 
Yan sina hamu mwaka jana walituhamasisha kulima alizeti saana, ila saiv wameondoa kodi kwa waagizaji wa mafuta nje bei imeporomoka.........mkulima wa alizeti yeyote tanzania saiv ni kufukuzana na hasara tu

Bora wangesema wataondoa kodi za matajir wanaoagiza mafuta, ili tusingejichosha kulima alizeti. Kwa hali hii hakuna mkulima atakaerudi mwakani kulima alizeti, maana hasara ni kubwa mno na kama mtu alichukua mkopo kazi ipo

Ushauri wa haraka: serikali ipandishe kodi haraka kwa mwaka huu kunusuru hii hali

Cha mwisho na muhimu: kwa mkulima ukija kuona zao linahamasishwa kulimwa kwa nguvu na wanasiasa usijiloge ukaingia, utalia kilio cha mbwa koko
Nini kifanyike sasa mkuu
 
Back
Top Bottom