Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta

Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.

Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.

( last edit 30/1/2019 )
Safi sana. dikiteta wetu hana hata chembe ya "usomi" Ana PHD lakini utadhania Samaki. Samaki anaishi ndani ya maji lakini mchafu! Magu alipita tu kwenye mifumo ya elimu. utamjua kwa jinsi anavyojenga hoja zake. akiulizwa kwa nini hukutani na wapinzani, anasema wanataka kunikata kichwa!

Hapa anabomolea watu, kule anasema wasibomolewe ni wapiga kura wangu. hiyo ni dalili ya kukosa weledi na fikra.

mpaka hivi sasa anafanya mambo yanayoonekana wazi kwamba yatatugharimu, na kwa kweli tunagharimika. baadaye tutajifunza, baada ya kulipa gharama kubwa. Mkapa aliwakebehi waliohoji uwekezaji wa madini. leo kiko wapi? Magufuli naye kadhalika
 
Udikteta ni relative.

Kuna wengine wanaweza kusema hata wewe ni dikteta ndani ya ACT-Wazalendo kwa sababu cheo chako hakina tofauti na Supreme Leader of Iran. Sayyid Ali Hosseini Khamenei

Acheni kulisha wananchi matango ya kisiasa.

Udikteta upi unaosema katika mazingira ya kuweza kusema serikali ya sasa inaongozwa na dikteta!
1. kuongoza nchi kwa matamko badala ya utaratibu wa kawaida wa kiserikali. Ghafla tulitangaziwa kuhamia dodoma, tena kwenye podium ya uenyekiti wa ccm. hapa kuwa na michakato ya kiserikali ilivyo kawaida. tena bajeti ilikuwa imepita. wazo lenyewe lilishachina. yeye kaagiza tu.
2. Kutoa maagizo yanayovunja sheria na katiba. Ni rais wa kwanza kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, tokea mfumo uliporejea mwaka 1992. Hata Nyerere aliporudisha nchi kwenye chama kimoja, alileta mchakato wa kubadili katiba kwanza.
3. Kusababisha vurugu kubwa katika ngazi za juu. Huu mtifuano wa kijinga kati ya CAG na Spika Ndugai umetokea bila comment kutoka Ikulu. confidence ya Ndugai inatuonesha JPM ndiyo alieendesha hilo zengwe.
Hayo ni machache tu mengine baadaye
 
kuna watu wanajua ukweli kabisa kuhusu utawala huu wa mabavu lakini ndio wamekuwa mstari wa mbele ktk kutetea,
 
Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.

Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.

Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
Leo umeongea point kubwa sana. Adui wa watanzania ni CCM nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kama putin ni dikteta ambaye amemudu ushindani dhidi ya Marekani na Urusi iko juu kiteknolojia, bora na sisi tuwe na dikteta kuliko kuruhu kelele kila siku kwa kisingizio cha demokrasia.

Urusi ilipoteza ushawishi kipindi cha Mikhail Gorbachev ambaye alikuwa pandikizi la USA, ila baada ya hapo Putini ameisimamisha tena Nguvu ya Urusi duniani.

Hatutaki demokrasia za kila siku mikutano kulaghai wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ni kweli kwamba Urusi ilisambalatika kwasababu ya Mikhail Gorbachev kua "pandikizi la USA" au UJAMAA ndio ulishindikana? Kama alikua ni pandikizi wa USA, kwanini nchi zote (including China )UJAMAA/Ukominist ulianguka hata kwenye hizo nchi ambazo huyo pandikizi hakua mtawala!? Putin pamoja na kwamba anasifiwa hapa, nae hakuurudia UJAMAA, anaendesha nchi kibepari na sio UJAMAA aliokulia huko mwanzoni. But again, nambie kitu gani kipya walicho nacho Warusi leo kitecknolojia ambacho Putin kaleta kipya zaidi ya ile iliokua USSR? Technology ya silaha walio nayo leo Urusi ni kweli ipo advanced but ni mashindano yale yale yaliokuwepo Enzi za ile ilikua United Soviet wakishandana na USA!
 
Sasa kwa akili yako putin asingewekeza kwenye teknolojia na jeshi urusi ingeweza kushindana na Marekani?

USSR ilikuwa ni muunganiko wa nchi nyingi za kikomunisti huko Asia na Ulaya Mashariki na Hub kuu ilikuwa ni Urusi, baada ya kuingia Mikhail Gorbachev Urusi ilianguka na kuifanya USSR pia kuanguka.

Putin ni rais mwenye upeo mkubwa sana, na sijasema popote kuwa Putin anaendesha Urusi kwa misingi ya ukomunisti.
Hivi ni kweli kwamba Urusi ilisambalatika kwasababu ya Mikhail Gorbachev kua "pandikizi la USA" au UJAMAA ndio ulishindikana? Kama alikua ni pandikizi wa USA, kwanini nchi zote (including China )UJAMAA/Ukominist ulianguka hata kwenye hizo nchi ambazo huyo pandikizi hakua mtawala!? Putin pamoja na kwamba anasifiwa hapa, nae hakuurudia UJAMAA, anaendesha nchi kibepari na sio UJAMAA aliokulia huko mwanzoni. But again, nambie kitu gani kipya walicho nacho Warusi leo kitecknolojia ambacho Putin kaleta kipya zaidi ya ile iliokua USSR? Technology ya silaha walio nayo leo Urusi ni kweli ipo advanced but ni mashindano yale yale yaliokuwepo Enzi za ile ilikua United Soviet wakishandana na USA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni lazima utakuwa Mchaga wale wa chini kabisa, kifua kimekujaa chuki hata huoni mbele.
Ukabila unatoka wapi hapa ......... kwa taarifa yako Mimi ni Msukuma, same as Nyani na Pascal Mayalla.

By the way, hivi kuna mtu ana roho mbaya na chuki humu JF zaidi yako ...!!?
 
Sasa kwa akili yako putin asingewekeza kwenye teknolojia na jeshi urusi ingeweza kushindana na Marekani?

USSR ilikuwa ni muunganiko wa nchi nyingi za kikomunisti huko Asia na Ulaya Mashariki na Hub kuu ilikuwa ni Urusi, baada ya kuingia Mikhail Gorbachev Urusi ilianguka na kuifanya USSR pia kuanguka.

Putin ni rais mwenye upeo mkubwa sana, na sijasema popote kuwa Putin anaendesha Urusi kwa misingi ya ukomunisti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ambacho sikubaliani na wewe ni kuhusu eti huyu former USSR president kua ni pandikizi la USA, if that is true, kwanini UKOMINIST uanguke everywhere in the world na sio Urusi pekee yake? Still Putin, nasisitiza kaendeleza tu yale yaliokuwepo tokea Enzi za USSR ya ukominist kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama, remember Putin ni zao la KUG (hapa kwetu ni TISS) wakati wa huyo unae mwita "pandikizi la USA" so anajaribu kutembelea mule mule alimokulia but nyakati za aina ya siasa zile alizokulia ndio zimeshindikana, inabidi tu aimbe Kimarekani/Kimagharibi hata kama hataki.
 
Putin alikuwa agent wa KGB ( shirika la ujasusi USSR/Russia) na sio KUB,
Hebu weka sababu za kuanguka kwa ukomunisti duniani, naona una deny sababu kuu niliyoiweka mimi.
Ambacho sikubaliani na wewe ni kuhusu eti huyu former USSR president kua ni pandikizi la USA, if that is true, kwanini UKOMINIST uanguke everywhere in the world na sio Urusi pekee yake? Still Putin, nasisitiza kaendeleza tu yale yaliokuwepo tokea Enzi za USSR ya ukominist kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama, remember Putin ni zao la KUG (hapa kwetu ni TISS) wakati wa huyo unae mwita "pandikizi la USA" so anajaribu kutembelea mule mule alimokulia but nyakati za aina ya siasa zile alizokulia ndio zimeshindikana, inabidi tu aimbe Kimarekani/Kimagharibi hata kama hataki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais
Hapa zitto aliongea ukweli mtupu,yule baba wa Chato hakuwa akijua mahali Dunia ilipo
 
Back
Top Bottom