Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Hauwezi kuona hoja hapa ,si unaona unavyopiga sarakasi na taulo .....yaani hamna hoja hapa !!!?
Hoja yangu ni utegemezi, tusiishi kwa kutegemea na hasa inapoonekana tunauwezo
 
Saa nyingine ni bora tunyimwe.
Hii misaada ndiyo inayo turudisha nyuma.
Tumepumbazwa na misaada.
Tanzania haijawahi kujitegemea tangu iumbwe , nyie endeleeni kufanya mchezo na wazungu , mnataka kuonja sumu !
 
nashukuru Mungu tumenyimwa ili sera ya hapa kazi tu ieleweke vizuri zaidi.
 
wakati mwingine ni bora hata tunyimwe hiyo misaada unajua mtu ukilala njaa ndo utajua siku inayofuata uamkie wapi au wapi umekosea mpaka umelala njaa!!!! na ikumbukwe kuwa hao wenyewe wanalipa kodi, haya mawazo tunayo toa baadhi yetu kwamba ni bora tungeupata huo msaada ni uoga wa kusimama wenyewe hii ni nchi yetu sote kila mtz alipe kodi.
Unayoyasema hata Wazimbabwe walidhani ni rahisi tu lakini sasa hivi wanajuta maana wamekuwa watumwa ktk nchi yao pesa yao haina dhamani tena Mugabe anaonekana kama anapendwa kumbe sivyo ila vyombo vya habari ya serikali ndo vinamtukuza ni hivi majuzi ameanza kurejesha mashamba kwa wazungu
 
Baadhi ya mitanzania ni mijitu ya hovyo sana,hvi baba zima na miguvu yake linakaa linalilia kusaidiwa?me namshauri magu akaze kamba,hayo masharti yao ya kifedhuli hatuyataki..wakafie mbele na vijisent vyao.
Ipo siku haya maneno yako utayakataa kwamba sio wewe uliye andika ngoja tuvute subira
 
Heri kuwa maskini jeuri kuliko kutiwa vidole, wakati mwingine huwa nawaza hivi hawa akina:- Mtwa Mkwawa, Kinjekitile, Mirambo, Mangi Meli, Songea, Mputa walikuwa wa hovyo sana kuliko Chief Mangungo wa Msovero?
Heri kuwa maskini jeuri kuliko kutiwa vidole, wakati mwingine huwa nawaza hivi hawa akina:- Mtwa Mkwawa, Kinjekitile, Mirambo, Mangi Meli, Songea, Mputa walikuwa wa hovyo sana kuliko Chief Mangungo wa Msovero?
Nyerere aliwahi kusema wazungu wasitupelekeshe, kama misaada na mikopo yao wakae nayo na alifikia Kuapa na kusema hatabadilisha msimamo akibadili msimamo basi awe nguzo ya chumvi mambo yalipombana akaamua kung'atuka
 
Nyerere aliwahi kusema wazungu wasitupelekeshe, kama misaada na mikopo yao wakae nayo na alifikia Kuapa na kusema hatabadilisha msimamo akibadili msimamo basi awe nguzo ya chumvi mambo yalipombana akaamua kung'atuka
Una records yoyote inayoonyesha kuwa Nyerere alistaafu kwa sababu ya masharti ya misaada ya wahisani ama mikopo ya taasisi za kifedha au mikopo kutoka nchi mbalimbali?
 
wanatoa tilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme unajua wanarudisha shilingi ngapi angalia miradi wanayopewa symbion wanachuma shilingi ngapi hakuna kitu cha bure
 
Kwa makusanyo ya kodi yaliyopo sasa. Inawezekana kwa serikali kuhifadhi kiasi cha 200bil kwa mwezi na ikatumia 1tril kwa mambo yake mengine (assuming kodi inakisanywa kufikia wastani wa 1.2tril). Kutumia 1tril ni sawa na kuongeza 200bil zaidi ya kodi iliyokusanywa kipindi cha jk.

Kwa miezi mitano itatosha kupata hiyo 1tril tutakayo ikosa huku kwa muda uliopo serikali ikaangalia namna ya kitafuta vyanzo mbadala ya mapato.

Bado inawezekana tukaishi bila hizo 1tril zao, ila hatuwezi sema kuwa hazina msaada.
 
Tatizo la Tz ni ushabiki wa kisiasa kuna baadhi ya watu wanadhani Magu hakosei na wala hajawahi kukosea.Jirani zetu kenya wako vizuri kiuchumi kuliko sisi lakini pesa kama hiyo wanaitaka je iweje sisi tuseme hatuzitaki kisa mtu mmoja ambaye hata akifa leo hakuna athari yoyote.nataka mnijibu hili swali je Shein ni bora zaidi kwa Watz kuliko hiyo pesa ya MCC?
 
Wote mnao shabikia na kujiona vidume kumbukeni tunanunua/tunaagiza sana bidhaa mbali mbali kutoka nje ya nchi yetu kuliko tunavyo zalisha ,hawa jamaa(mbepari)wakiamua tule nyasi tutakula na tutanyoosha mikono juu mapema sana..Hatuna uchumi ulio imarika kiasi tugomee misaada kisa CCM itawale milele,kwa sababu kinachoonekana sababu kubwa ni hali ya Serikali kukandamiza haki za raia hususani kwa yaliyo tokea Zanzibar (ref tamko la nchi wahisani kutotambua Uchaguzi wa marudio Zanzibar) plus Ufisadi kwa namna unavyo shughulikiwa na viongozi wa Serikali.

Niseme tu wakiamua kutuwekea vikwazo kidogo tu tutarudi kule tulitoka ,mfano wakiamua nchi wahisani wasifanye biashara na Tanzania haya magari tunayo yatumia kwa usafiri yaki haribika vipuri tuta pata wapi?

......
Akiri za mbayuwayu ww ? magari na vipuri tunanunua kwa pesa yetu ebo !
 
End on neo colonialisms
End of economic dependency

Nampongeza rais kwa kauli yake

Hakuna nchi iliyoendelea dunian kwa kutegemea mikopo ya kinyonyaji
 
Moja ya sababu zilizomfanya Nyerere anga'tuke na kuachia madaraka ni hiyo ya kukataa Sera zs wakubwa alikataa masharti aliyopewa akiwa Kigoma alitoa hotuba ya kuelezea msimamo wa kutokubaliana na sera za mashirika ya kifedha ulimwenguni na nchi ikafikia hali mbaya ya kiuchumi viwanda vikakosa vipuri ,hali ya usafirishaji wa mazao kutoka mashambani ikadorora miundo mbinu mingi ikafa Rais wa awamu ya pili Alli Hassan mwinyi alikubaliana na masharti yote ya IMF na World bank na uchumi ukapata ahuweni na Kidogo kidogo viwanda vikapata uhai tena.
 
wakati mwingine ni bora hata tunyimwe hiyo misaada unajua mtu ukilala njaa ndo utajua siku inayofuata uamkie wapi au wapi umekosea mpaka umelala njaa!!!!.
Chifu, siyo kwa akili za watanzania zilizodumaswa na serikali za CCM na mifumo yake. Si uliona wagogo walivyofanya baada ya njaa? Walikula viwavi!! Serikali za CCM kwa kuonyesha pale zinapotimiza wajibu wake na kuwadanganya wananchi kuwa hiyo ni misaada, hivyo wananchi washukuru, zimejenga utamaduni wa kutegemea misaada kwa wananchi wengi.
 
Tufanye kazi wapi
TRA, BOT, NSSF,UBUNGE,U-DC wapi?
Tujuze mwenzetu hata kulima utatupa shamba na pembejeo bure?
Fanya kazi hapo hapo unapofanyia sasa! Ila uongeze bidii! Lakini pia tuone fahari kulipa kodi! Suluhisho lipo katika: 1. Kufanya kazi kwa bidii kila MTU pale alipo 2. Kulipa kodi kwa fahari 3. Kutokomeza ufisadi
Tukifanikiwa hayo matatu, wazungu wataisoma namba!
 
Dubai yenye uchumi mzuri na imara hata zaidi ya mara 100 bado inapokea misaada. Tanzania nchi ambayo imeharibiwa na CCM kwa miaka kibao, Magu anadhani tunaweza kulala na kuamka na kubadilisha flow dynamics, badala ya misaada kutoka Marekani kuja Tanzania na kuanza kutoka Tanzania kwenda Marekani!
Inapokea misaada lakini haitegemei misaada! Tunachosema ni kwamba, na sisi tuachane kabisa kuombaomba misaada!
MTU kama anaona uhitaji wetu atusaidie bila kutushinikiza kwa masharti yoyote Yale!
Wazungu wanajua kuwa maendeleo yao hayawezi kuwa endelevu bila ubia na Africa!
 
Ni bora tunyimwe ili tusiendelee kulemaa, cha msingi watu wachape kazi na kulipa kodi, hizo hela tutapata tu
 
Kimsingi kama wataamua kutunyima hiyo misaada waathirika ni watu wa chini hao decision makers ambao kimsingi ndo chanzo cha matatizo yote haya hawapati athari yoyote, njia nzuri ilikuwa ni kuwawekea wao vikwazo vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao katika nchi husika na kuwapiga marufuku kuingia kwenye hizo nchi wahisani
 
Back
Top Bottom