Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Usifananishe mfumo wa mtu mmoja mmoja ,ukaulinganisha na Nchi mkuu..
Mfumo huletwa na watu, ambao ni wananchi - hivyo wananchi tukiwa asilimia kubwa tunawaza na kutegemea MCC ni hatariiiii sana ndugu yangu.
 
wakati mwingine ni bora hata tunyimwe hiyo misaada unajua mtu ukilala njaa ndo utajua siku inayofuata uamkie wapi au wapi umekosea mpaka umelala njaa!!!! na ikumbukwe kuwa hao wenyewe wanalipa kodi, haya mawazo tunayo toa baadhi yetu kwamba ni bora tungeupata huo msaada ni uoga wa kusimama wenyewe hii ni nchi yetu sote kila mtz alipe kodi.
 
Hiyo misaada ya MCC inakuja kwa sababu nyingine kabisa, sio siasa kama mnavyofikiria. Tulieni subirini jibu.
 
Mfumo huletwa na watu, ambao ni wananchi - hivyo wananchi tukiwa asilimia kubwa tunawaza na kutegemea MCC ni hatariiiii sana ndugu yangu.

Hapa tuna zungumzia umuhimu wa hizi pesa kwa taifa lipilosababishiwa umasikini na CCM toka zama zile kwa sababu za udikteta,sio wote tunawaza kusaidiwa katika kila jambo....
 
Lengo la kunyimwa msaada ni sehemu ya kutulazimisha tutii matakwa yao na tukijitia maskini jeuri watabana kila sehemu na mwisho wake hata mikopo watatunyima ukizingatia mashirika yote makubwa ya kifedha wamiliki ni wao.

Vikwazo vya kiuchumi visipofanya kazi wataanzisha fitina na kuzua uongo kupitia vyombo vyao vya habari

Wapi katika Afrika au hata katika Dunia kiongozi mzalendo akapendwa na kuthaminiwa na wazungu...? ni lazima uwe ndumilakuwili ili uende nao sambamba..
 
Hapa tuna zungumzia umuhimu wa hizi pesa kwa taifa lipilosababishiwa umasikini na CCM toka zama zile kwa sababu za udikteta,sio wote tunawaza kusaidiwa katika kila jambo....
unaufahamu udikteta au unaandika tu? Unaandika ili kuhalalisha utegemezi? Assume MCC isingekuwepo? Je wote waliopiga hatua wamefika hapo kwa ajili ya MCC? Nitajie nchi zingine zinazofaidika na MCC ambazo zimepiga hatua kiasi kwamba tusikitike kwa kukosa hio package ya MCC.
 
Baadhi ya mitanzania ni mijitu ya hovyo sana,hvi baba zima na miguvu yake linakaa linalilia kusaidiwa?me namshauri magu akaze kamba,hayo masharti yao ya kifedhuli hatuyataki..wakafie mbele na vijisent vyao.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Suala ni kwamba tumenyimwa kwa sababu gani?, tumenyimwa kwa sababu ya unkurunzinza wa huko zanzibar
tumetanguliza siasa za kijinga huku wanafunzi wanakaa chini,miundombinu mibovu, hispitali hazina Dawa nk, tukiitikia kibwege "hapa kazi tu"
 
Lengo la kunyimwa msaada ni sehemu ya kutulazimisha tutii matakwa yao na tukijitia maskini jeuri watabana kila sehemu na mwisho wake hata mikopo watatunyima ukizingatia mashirika yote makubwa ya kifedha wamiliki ni wao.

Vikwazo vya kiuchumi visipofanya kazi wataanzisha fitina na kuzua uongo kupitia vyombo vyao vya habari

Wapi katika Afrika au hata katika Dunia kiongozi mzalendo akapendwa na kuthaminiwa na wazungu...? ni lazima uwe ndumilakuwili ili uende nao sambamba..

Kwa hiyo viongozi wazalendo ni hawa wanao kandamiza haki za raia kama ilivyo tokea Zanzibar!!?.
Yaani una washutumu mabepari kwa uovu wao ,lakini uovu unaofanywa na viongozi wako wa Afrika unaupaka mafuta na kuuita ni wa kizalendo!?..
 
Ifike wakati tuthamini sana utu wetu dhidi ya haya mabepari.

Nachokiona hapa hata tukinyiwa huo msaada tukikomma vizuri tu tunaweza kutoka kabisa
 
Naombeni kuuliza swali ,Hivi Marekani inayotoa misaada kwa nchi nyingi duniani hivi yenyewe haidaiwi ???
inadaiwan na china tena pesa nyingi tu! mkuu hii yote ni sababu ya maswala ya kiuchumi.kama ulisikia **** miaka kama 3-4 iliyopita china alikuwa na budget surplus hii ni kutokana na export kubwa aliyoipata na FDI nchini mwake-tatizo la kiuchumi linakuja hiyo surplus ikiirudisha kwenye mzunguko wa kifedha ni lazima italeta matatizo ya kiuchumi tena kama inflaation kwa hiyo ni lazima aitoe kama grant au mkopo ndipo alipo ikopesha marekani
 
Nashukuru mkuu mimi sijui lolote kuhusu uchumi je hili la Tanzania kusema inapaswa iwe nchi ya kukopesha wengine ,maana yake ni kwamba sisi hatutakiwi kukopa ? ama kudaiwa ?? Tunapokataa mikopo kwa maneno na huku kwa vitendo hatuna namna ya kujisaidia kuna tija gani ?? Kwa vitendo nikiwa na maana ya Viwanda ,Mikataba ya hovyo inayo liumiza taifa ,ukwepaji wa kodi ,kutokua na vyanzo mbadala wa kuongeza wigo wa kodi nk nini hasa matarajio yetu kwenye hili ??
 
WaTanzania kwa kupenda misaada, mtu hasumbui akili katatizo kadogo tena kako ndani ya uwezo wake. Utasikia mpigie simu fulani asaidie, na ananunua vocha ya elfu kumi anampigia mtu asaidie elfu tano
tukomae kufanya kufanya kazi wakati viongozi wanakua majizi au kuna sheria gani za kuwabana?
 
tumetanguliza siasa za kijinga huku wanafunzi wanakaa chini,miundombinu mibovu, hispitali hazina Dawa nk, tukiitikia kibwege "hapa kazi tu"
Hasa siasa za kuzungusha mikono
 
maskini jeuri, hata ukiwa tajiri hela zile si za kuzipuuzia, zingefanya mengi, Mahiga tusaidie! Style ya kumuita Magu kule..
Kumbe mtumwa ni mtumwa hata kama wakikufungua pingu utataka kupeleka mikono yako ufungwe tena. Utajiri wote tulonao bado watu wanaomba kupewa misaada ? Gesi mpk Ruvu imegundulika bado watu wana mawazo ya misaada ? Magufuri una kazi kubwa, vichwa vya wabongo vingi vina urojo tuu
 
Bado hatujafikia kipindi cha kudharau msaada mkubwa namna hiyo wa 1 trillion TZS. Hapa tunaandaliwa tuu kisaikolojia ila ni pigo kubwa sana kwa watz na Magu pia.
Tunamshukuru Magufuli kwa kutufundisha kujitegemea ila kila kitu ni process. Tukishajijengea uwezo wa kukusanya kodi kubwa ya kutosha all expenditures hapo ndio tuseme no kwa vimisaada. Wewe mtu anakupa msaada ambao ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwezi mzima unadharau?
Anyway tutakaoteseka ni sisi maskini wa nchi hii wala siyo Magufuli na watu wake.
nakubaliana na wewe ila tuweke sheria ngumu za kuwabana viongozi wapunguze
wizi maana najua kuacha kabisa awawezi maana naona kama rushwa ni sera ndani ccm
 
Hatuwezi kuishi kwa kutegemea misaada ...LAZIMA MAANA YA UHURU WA KWELI IHESHIMIWE...HATUKUHITAJI UHURU WA BENDERA BALI UHURU KAMILI...Iko haja ya kuandaa mashtaka dhidi ya wote walioinyonya Tanzania kama koloni lao na pengine kupelekea hali hii tuliyonayo sasa.

Ni wakati wa wote waliopotelea ughaibuni kipindi cha Nyerere kurejesha ujuzi nyumbani kama ilivyokubalika....

Huu sio wakati wa kulamba viatu vya wakubwa....Ni wakati wa kukamuana kwenye kodi na kuhimizana kufanya kazi ili tuendelee...Asiyetaka akane uraia na aende kule anakohisi ataishi bila kulipa kodi au kwa kutegemea msaada.
Haya ni kwel lkn tambua viongozi ndo wana spend hela nyingi kuliko mtu mwingine yeyote na ujue anaetegemea pesa za nje kashazoea awez acha ata kidogo coz anajua utajir ndo anautolea uko toka ukoloni mwiz uokoka baada ya kupitia misukosuko au kudakwa kwaiyo ni kwa mawazo wanaoimba tuache misaada ni masikin wanaoona faida ya msaada au lugha halisi mkopo ni wapenda maendeleo kwa kasi ila wanaoimba mikopo kwa sauti ya juu ndo hao wanaochukua na kugawana na kurudi ulaya tena bila kupigiwa kulele na kujitapa wao ndo wazalendo wa kwanza kuliko mwingine
 
Lengo la kunyimwa msaada ni sehemu ya kutulazimisha tutii matakwa yao na tukijitia maskini jeuri watabana kila sehemu na mwisho wake hata mikopo watatunyima ukizingatia mashirika yote makubwa ya kifedha wamiliki ni wao.

Vikwazo vya kiuchumi visipofanya kazi wataanzisha fitina na kuzua uongo kupitia vyombo vyao vya habari

Wapi katika Afrika au hata katika Dunia kiongozi mzalendo akapendwa na kuthaminiwa na wazungu...? ni lazima uwe ndumilakuwili ili uende nao sambamba..
Heri kuwa maskini jeuri kuliko kutiwa vidole, wakati mwingine huwa nawaza hivi hawa akina:- Mtwa Mkwawa, Kinjekitile, Mirambo, Mangi Meli, Songea, Mputa walikuwa wa hovyo sana kuliko Chief Mangungo wa Msovero?
 
Jamani kwenye hii post nimegundua watu wengi uelewa wao ni mdogo sana hasa kwenye mabo ya uchumi na siasa.
1.kwa walewanaosema watu wafanye kazi na sio kuomba omba msaada ,naombeni ni waulize the end product ya kufanya kazi ni nini? maana kazi utazalisha ukizalisha kwa wingi ili upate kipato lazima uuze soko na kwa hao hao wanatoa hiyo mikopo-kumbuka kuna njia nyingi za kuzuia bidhaa yako isiuzike kwenye soko la dunia -maana hizo fedha watato subsidies kwa wakulima wao,haya mniambie hoyo GDP yetu itatoka wapi??
2.investment zote kubwa za madini,gasi na n.k zinahitaji technologia na ma expart , hivyo vyote hatuna na jua hizi investment ndizo zinazochagia kwenye pato la Taifa-na bado hazijaajiri watanzania wengi ndio maana unasikia pato la Taifa linakuwa lakini maisha yetu bado ni chini maana watanzania wengia hawajaajiriwa kwenye hizo sekata.sasa leo wakisema wajitoa hata kwenye uwekezaji tutafanya nini??

Jamani hamna anayependa misaada lakini hali yetu kama nchi bado tunahitaji tena sana ,huwezi ukaikataa misaada gafla athali zake ni kubwa sana kiuchumi,kijamii na kisiasa lazima tuweze kwanza kutengeneza mazingira ya kukikataa misaada,kwanza tuwe na tu import technologia ,tuanzishe viwanda vidogodogo,kutafuta allies wa kufanya nao biashara ambayo itakuwa equall
 
Back
Top Bottom