Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Ieleweke kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Milenia (MMC) inakaa kikao leo ili kuijadili Tanzania kama imetimiza masharti baada ya kuamua kutopigia kura mkataba unaopendekezwa kati ya MCC na Tanzania katika kikao cha mwezi desemba 2015 ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala iliyoyatilia shaka na ambayo yanaweza kuipotezea Tanzania sifa ya kuweza kupata msaada wa MCC.

Siku moja kabla ya kikao cha MCC tumemsikia Rais Magufuli wakati akiwa kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front akisema,
‘’Sisi Watanzania kwa umoja wetu kila mmoja katika eneo lake tukiamua kufanya kazi, Tanzania haitakuwa nchi masikini. Wala hatutahitaji misaada yoyote kutoka nje, wala hatutabembeleza misaada ya masharti tunayopewa. Tanzania ni nchi yenye neema, Tanzania ina kila kitu, Tanzania imependelewa, lakini tukisimama katika umoja wetu na kila mmoja akatimiza wajibu wake, Tanzania inaweza kuwa miongoni mwa nchi ambazo zitakuwa zinatoa misaada kwa nchi nyingine’’.

Ninaamini maneno ya Rais Magufuli hakuyatoa kwa bahati mbaya siku moja kabla ya bodi ya MCC haijaanza kikao chake kuamua kama itoe msaada wa $472 million (Nearly Sh1 trillion).

Tunaambiwa serikali ina macho, masikio na mkono mrefu. Kwa kutumia nyenzo hizi, serikali inaweza kufahamu matokeo ya kikao cha MCC kabla ya official statement.

Maneno ya Rais Magufuli ni telltale sign kuwa tumenyimwa msaada wa fedha za MMC na maongezi yake kanisani ilikuwa ni kutuandaa kisaikologia!

Kunyimwa kwa msaada kutafungua mdahalo mpana kuhusu faida au hasara ya kunyimwa msaada. Nini kifanyike ili kuziba pengo la zaidi ya shilingi trillion 1 ambazo zilikuwa zinatakiwa zitumike katika ujenzi wa barabara na kusambaza umeme nchini.

Kuna wengine wanasema utegemezi wa misaada unapingana na dhana ya proverb inayosema, give a person a fish: you have fed the person for today. Teach a person to fish: you have fed the person for a lifetime.”

Tunatakiwa pia tukumbuke,there's no such thing as a free lunch in this world. Huu sio msaada per se bali ni manunuzi ya influence/power katika meza ya maamuzi ya nchi kwenye siasa, uchumi na kijamii!

Vile vile tukumbuke kuwa MCC=Symbion power!
 
Trillion 1 kwa maisha yetu ni pesa nyingi sana, wangeitumia effectively Kwny ma project ya barabara ni pesa ndefu sana, ila ndo hivo tena hata hio hela tukipewa haionekanagi inaenda wapi na kufanya nini?
 
Hatuwezi kuishi kwa kutegemea misaada ...LAZIMA MAANA YA UHURU WA KWELI IHESHIMIWE...HATUKUHITAJI UHURU WA BENDERA BALI UHURU KAMILI...Iko haja ya kuandaa mashtaka dhidi ya wote walioinyonya Tanzania kama koloni lao na pengine kupelekea hali hii tuliyonayo sasa.

Ni wakati wa wote waliopotelea ughaibuni kipindi cha Nyerere kurejesha ujuzi nyumbani kama ilivyokubalika....

Huu sio wakati wa kulamba viatu vya wakubwa....Ni wakati wa kukamuana kwenye kodi na kuhimizana kufanya kazi ili tuendelee...Asiyetaka akane uraia na aende kule anakohisi ataishi bila kulipa kodi au kwa kutegemea msaada.
 
Nchi haiwezi kuinvest ktk kuombaomba!
Yes we need that money, lkn sio kusimamisha maisha yetu kwa kutolea macho pesa za watu! Ni vema tukizipata, lkn tukizikosa pia maisha yasonge mbele!
Ukitumia principles za asili za wanyama, maisha Hayawezi kuwa magumu!
Mamba huwa anamiss targets zaidi ya a third ya attempts zote anazozifanya, cheetah yeye more than 50% na the king (lion) more than a third of all attempts made! Hata siku moja hawakai chini kuhuzunikia misses zilizotokea instead wanaandaa ambush nyingine ili maisha yasonge!
Pesa ya MCC ikigoma, tutarejea kwa kodi, kazi na majipu! Tutapata tu trillion moja nyingine kwa njia mbadala!
 
mwenye kaya nae anatuongopea kwa nyenzo zipi tutajitegemea? kama mali asili za taifa kagoma kupitia mikataba yake(madini,gesi na nk) yeye anapambana na watumishi hewa hivi kwa taifa kama hili ambalo lina changamoto kibao kwa mapato yapi tujitegemee?
Nigeria pamoja na uchumi mkubwa bado ni tegemezi iweje sisi ambao kutwa kuchwa ni ufisadi tu.
Pitia mikataba yote ya madini na gesi na fuatilia fedha zote zilizopotea kizembe BOT na hapo tunaweza angalau kupunguza utegemezi sio hizi ngonjera za majipu tu
 
Back
Top Bottom