End on neo colonialisms
End of economic dependency
Nampongeza rais kwa kauli yake
Hakuna nchi iliyoendelea dunian kwa kutegemea mikopo ya kinyonyaji
"hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa kutegemea mikopo ya kinyonyaji" Hii kauli ni kweli. Lakini usipongeze kauli pongeza vitendo.
Hakuna nchi ya dunia ya tatu iliyoweza kukimbia makucha ya Neo colonialism na economic dependancy. Ukisema ipo unajidaganya mwenyewe, tena unasema kwa uhakika kabisa eti unapongeza kauli. Je kauli inaweza kututoa kwenye ukoloni mamboleo na uchumi tegemezi?
Kutoka kwenye ukoloni mamboleo na uchumi tegemezi kunahitaji maono na dira mpya itakayobadilisha sera zote za nchi na kuleta commitment ya hali ya juu kwa viogozi na wananchi kwa ujumla.
Kwanini nchi za dunia ya tatu haziwezi kujinasua na makucha ya ukoloni mamboleo na uchumi tegemezi? kujibu swali hili ina kupasa kuangalia matatizo yote yanayokabili hizo nchi pia kuangalia je matatizo hayo wanayatambua ? na kama wanayatambua wamefanya juhudi gani kuyatatua wenyewe pasipo mkono wa mkoloni mamboleo? Je ni kwa kiasi gani wananchi wapo aware na matatizo hayo? au wapo kiushabiki wa kisiasa tuu?
Tatizo la dunia ya Tatu ni kuigiza kuwa hakuna matatatizo na kama yapo ni madogo sana na yanaweza kutatuliwa kwa haraka zaidi kipindi wanapoomba kura kwa wananchi . Masikini sijui ni lini nchi dunia ya Tatu zitakapo kubali kuwa zina matatizo na kuazimia kuyatatua wenyewe badala ya kuhaidiwa ahadi tamu zisizo tekelezeka yani wananchi wamekuwa wakitegemea sugarcoated politics kutatua matatizo yao. Shida tuliyonayo wakazi wa dunia ya Tatu ni kuigiza kuwa hatuna matatizo kwa kuwa tunaishi kwa ushabiki wa kisiasa badala ya kuangalia maslahi ya mataifa yetu.
Baadhi ya Matatizo yanayo fanya nchi za dunia ya Tatu kuendelea kuwa watumwa wa wakoloni mamboleo kupitia uchumi tegemezi ni :-
1. Ukosefu wa uzalendo kwa viongozi wa dunia ya tatu. Bado dunia ya Tatu haijapata viongozi wazalendo hata hao wakina Mugabe sio wazalendo kwa Africa na nchi zao binafsi kwa kuwa wapo kimaslahi binafsi na ndiyo maana wanang'ang'ania. madaraka ili kutimiza maslahi yao binafsi.
2. Matumizi mabaya ya madaraka kwa nchi za dunia ya Tatu hususani kusini mwa jangwa la Sahara imekuwa ni chronic disease kwakuwa hakuna utaratibu rasmi ndiyo maana hakuna uwazi katika maslahi ya taifa ni urasimu tuu . Hivyo upelekea mikataba mibovu, Rushwa, ufisadi na wizi wa Mali ya umma. Na kwa kuwa kuna double standards hakuna hatua inayo chukuliwa kwa watu hao . Bado matumizi mabaya ya rasilimali yani dunia ya Tatu rasilimali zimekuwa laana badala ya NEEMA
3. Mifumo mibovu ya elimu inayoandaa watu kuajiriwa kwa kuwa wamefundishwa kufanya kazi badala ya kuwa wataalamu wenye kutumia taaluma zao kivitendo katika kutatua matatizo. Hivyo tumejikuta tuna lundo la wasomi wasiozalisha maana hawana kazi. Wakati nchi za dunia ya kwanza wamewekeza katika elimu ya vitendo ndio maana kila kukicha wanafanya uvumbuzi mkubwa wa kiteknolojia na wanaanzisha viwanda vinavyowezesha serikali zao kuneemeka kwa kulipa kodi.
4. Nchi za dunia ya tatu hazina viwanda hata kidogo yani zaidi ya 90% ya bidhaa zote zinatoka dunia ya kwanza. Sasa tutawezaje kuondokana na makucha ya mkoloni mamboleo bila uwezo wa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe na kuuza nje? Hata wachumi wanasema ili nchi iondokane na utegemezi ni lazima iweze kuexport zaidi kuliko kuimport (favorable balance of payment/ trade) . Dunia ya Tatu hakuna teknolojia, nishati ya uhakika, wataalamu wenye ujuzi wakivitendo ndiyo maana tunakuwa tegemezi wa kila kitu.
5. Migigoro ya kisiasa, kikabila inayochochewa na watu wa dunia ya kwanza kwa kutengeneza vibaraka wa kisiasa ili kutimiza mahitaji yao na kwa kuwa watu wa dunia ya Tatu sio wazalendo wanakubali kutumika.
6. Dunia ya Tatu imetengwa kwenye geopolitics, diplomasia ya kimataifa katika vyombo muhimu vya kufanya maamuzi yenye maslahi kwao na hakuna juhudi yoyote iliofanywa kuihusisha dunia ya Tatu, watu wa dunia ya kwanza wanasema vingozi wa dunia ya Tatu hawafuati kanuni za utawala bora na wanakiuka haki za binadamu na ndio maana The Hague imekuwa shubiri kwao.
Dunia ya Tatu haina veto power kwenye maamuzi makubwa kabisa ya dunia wala ushawishi kama wale wa P5+, G7,G8, G20 nk... pia haina nguvu kwenye mifumo ya fedha ya IMF na WB, pia katika WTO na WCC hadi kwenye michezo. Sasa kuondoka kwenye mifumo hii yenye kuifanya dunia ya Tatu kuwa hivi ilivyo inahitaji mtazamo mpya na utawala bora na commitment za ukweli zisizo na maslahi binafsi ya kisiasa.