Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

WaTanzania kwa kupenda misaada, mtu hasumbui akili katatizo kadogo tena kako ndani ya uwezo wake. Utasikia mpigie simu fulani asaidie, na ananunua vocha ya elfu kumi anampigia mtu asaidie elfu tano
 
Kwahiyo kwa sababu tukikomaaa tunaweza kujitegemea basi Hamna haja ya kuiheshimu demokrasia eti Kwa Kua hatuhitaji misaada?
 
Hii ni wake up call!watu walipe kodi na watu wafanye kazi kwa bidii .nchi nyingi waliweza kujitegemea kwanini tushidwe??

Baadhi ya nchi nyingine zilifanikiwa kwa sababu ya nidhamu ya matumizi pamoja na kisimamia sheria za nchi kuhakikisha zinafuatwa na kila raia.Kwa hapa kwetu Tanzania tume wekeza sana kwenye matumizi kuliko kuwekeza ktk maendeleo.Tumewekeza kwenye kulindana hasa inapotokea wizi(Ufisadi)unao husisha chama chetu tukufu CCM....Tuna watetea wezi wa mali ya umma kwa kuwapa vyeo..Hatubwashitaki /hatuwafungi/hatuwafilisi mali walizo tuibia ,hivyo hata ungelipa kodi mpaka ufilisike nchi haiwezi kusonga kwa makando kando kama hayo niliyo yaainisha hapo juu.

Maendeleo huja kwa kasi lakini hakuna maendeleo kama hakuna demokrasia inayo dhihirika kwa vitendo,sahau sana tutakuwa tuna tembea mwendo wa mlevi hatua mbili mbele halafu hatua nne nyuma...

..
 
Bado hatujafikia kipindi cha kudharau msaada mkubwa namna hiyo wa 1 trillion TZS. Hapa tunaandaliwa tuu kisaikolojia ila ni pigo kubwa sana kwa watz na Magu pia.
Tunamshukuru Magufuli kwa kutufundisha kujitegemea ila kila kitu ni process. Tukishajijengea uwezo wa kukusanya kodi kubwa ya kutosha all expenditures hapo ndio tuseme no kwa vimisaada. Wewe mtu anakupa msaada ambao ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwezi mzima unadharau?
Anyway tutakaoteseka ni sisi maskini wa nchi hii wala siyo Magufuli na watu wake.
 
La msingi ni kuangalia tunanyimwa msaada huo ambao sie tulishauingiza kwenye bajeti yetu kwa sababu gani?
Kwa sababu ni ujinga kama ni itakuwa kwa vile serikali inakandamiza demokrasia. Huo mpango wa kutohitaji misaada ni mchakato unaopaswa kuandaliwa na sio kukurupuka na kudharau misaada bila maadalizi.
Hii ni nchi, na nchi haiendeshwi kama familia ya mtu
 
Ieleweke kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Milenia (MMC) inakaa kikao leo ili kuijadili Tanzania kama imetimiza masharti baada ya kuamua kutopigia kura mkataba unaopendekezwa kati ya MCC na Tanzania katika kikao cha mwezi desemba 2015 ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala iliyoyatilia shaka na ambayo yanaweza kuipotezea Tanzania sifa ya kuweza kupata msaada wa MCC.

Siku moja kabla ya kikao cha MCC tumemsikia Rais Magufuli wakati akiwa kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front akisema,

Ninaamini maneno ya Rais Magufuli hakuyatoa kwa bahati mbaya siku moja kabla ya bodi ya MCC haijaanza kikao chake kuamua kama itoe msaada wa $472 million (Nearly Sh1 trillion).

Tunaambiwa serikali ina macho, masikio na mkono mrefu. Kwa kutumia nyenzo hizi, serikali inaweza kufahamu matokeo ya kikao cha MCC kabla ya official statement.

Maneno ya Rais Magufuli ni telltale sign kuwa tumenyimwa msaada wa fedha za MMC na maongezi yake kanisani ilikuwa ni kutuandaa kisaikologia!

Kunyimwa kwa msaada kutafungua mdahalo mpana kuhusu faida au hasara ya kunyimwa msaada. Nini kifanyike ili kuzipa pengo la zaidi ya shilingi trillion 1 ambazo zilikuwa zinatakiwa zitumike katika ujenzi wa barabara na kusambaza umeme nchini.
Hatutaki mambo ya Dr Rutengwe, wakae na hela zao na MCC yao na sisi tutaanzia hapo tulipo.
 
ivi nawaza tuu kwa sauti,, haiwezekani kakaundwa ka kikosi flani kufatilia watu wanaonunua bidhaa bila kuomba risiti wakikukamata faini iwe mara tano ya gharama ulonunulia bidhaa?? waforce kwa sasa ili baada ya kama miezi sita huo utamaduni uwe umejijenga miongoni mwetu.. nawaza tu kama kwa sasa makusanyo ni karibu trilioni 1.5 kwa mwezi which means kwa mwaka tunakua na trilioni 18 wakati bado kuna wafanya biashara wengi tuu hawatoi risiti wauzapo inawezekana tukibanana vizuri tukaondoa watumishi hewa wote na matumizi hewa yote tunaweza kuishi na tusife ata tukiikosa hiyo pesa ya masimango ya mcc,, halaf pia sisi tuna ma rasilimali ya kutosha wengi wanayatolea macho, nashawishika kuamini wataileta iyo pesa ya mcc hata kwa mlango wa nyuma. ila tuu tusizidishe kiburi wasije kutupiga
 
....misaada kama hii huleta breath kwa nchi...../
TUNDAIWA TRILIONI 35+ KAMA DENI LA TAIFA PESA HIYO ILIFANYA NINI?? SI NDIZO WATU WAMEFICHA USWISS HUKU WANANCHI WAKITESEKA?? HUO MSAADA WA MCC WALA HAUNA MAANA YOYOTE UJE USIJE NI SAWA TUU
 
Safari moja huanzisha safari nyingine. Mara nyingi mtu akikunyima msaada anakuwa amekusaidia sana. Ila for time being unaweza sikitika na kusononeka
 
Tusidanganyane. Ni mjinga pekee yake anayeweza kukaa chini na kusema, 'hiyo pesa tunyimwe kwa kuwa tuna uwezo wa kujitegemea'. Hiyo pesa kwa Tanzania ni muhimu sana. Ni hela hiyo ya MCC ndiyo iliyojenga barabara nyingi mpya za lami na madaraja wakati wa JK, pamoja na miradi mikubwa ya umeme intondelea. Leo karibia miradi yote ya ujenzi imesimama.

Dola karibia milioni 500 ni hela nyingi sana kwa nchi kama Tanzania ambayo pesa hiyo ni sawa na makusanyo yote ya kodi kwa mwezi. Ebu jiulize, hivi unaweza kukubali kiurahisi kuwa ukose mshahara wako wote wa mwezi unaoitegemeza familia yako?

Magu asijidanganye, tunatakiwa kujitegemea lakini siyo kwa namna anayoifikiria. Kwa sasa ni wakati wa kukusanya nguvu zote, iwe ni misaada, mikopo, makusanyo ya kodi kwaajili ya kupata nguvu za kuweza kujitegemea mbeleni. Tanzania kwa makusanyo yake ya pesa ya madafu trilioni 1, haina uwezo wa kujitegemea ghafla kutoka kwenye dependence ya 40%.

Magu asitupeleke iliko Zimbabwe ambako kiburi cha Mugabe kinawatesa Wazimbabwe balaa. Madaktari, manesi na walimu Wazimbabwe wameishia kuwa waiters SA. Ni aheri kuwa waiter SA kuliko kuwa daktari Zimbabwe.

Mwalimu naye aliwahi kujitahidi kutaka kufanya haya ya Magufuli, waliokuwepo wanajua. Hata sabauni za kufulia, mafuta ya kupikia na chumvi viliadimika.

Kumbukeni kuwa hiyo 470 milioni ni pesa ya kigeni, na ina impact kubwa kwa Tanzania. Kwa nini Watanzania wachelewe kupata maendeleo au wateseke kwa mambo ambayo ni rahisi kutekeleza? Afadhali tungenyimwa huo msaada kwa kutetea mambo ya msingi, mambo yenye faida kwa Taifa. Hapo tungesema tunalinda uhuru wa Taifa. Lakini sasa tutanyimwa kwa mambo ya kipumbavu, kutetea udikteta uliofanyika Zanzibar!

Hii ni sawa na mtu ambaye ni mchafu, hana choo, hafui nguo zake, anapikia chakula kwenye mazingira machafu. Halafu anatokea jirani anakuambia kuwa nitakujengea nyumba ambayo itakuwa na choo kizuri ndani, itakuwa haina vumbi kwa sababu nitakuwekea tiles LAKINI ili nikufanyie hayo kwanza nataka unioneshe unauchukia uchafu, uache kujisaidia kwenye upenu wa nyumba yako. Halafu wewe unasimama na kusema unaingilia uhuru wangu, kama ni hivyo ni aheri usinipe huo msaada. Naenda kufyeka msitu, nikapande michungwa baada ya miaka 5 nitaweza kujenga mwenyewe kwa sababu nina uwezo.

Kwanza masharti ya MCC siyo kwa faida ya USA, ni kwaajili yetu wenyewe. Yaani udikteta uliofanyika Zanzibar kwa manufaa ya Shein na CCM, udikteta ambao umemwudhi kila mtu mstaarabu Duniani, ndiyo sisi utufanye kuonekana ni wetu wenye msimamo? Kama huo ndiyo msimamo basi ni msimamo wa mtu mjinga.

Juzi Magufuli wakati anazindua mradi wa umeme mradi wa Kinyerezi alisema wazi kuwa hatuwezi kuacha hela ya bure tuliyopewa na Japani kwa sharti la kuchangia 15% ya gharama ya mradi. Pesa itakayotolewa na Japani kwa mradi wa Kinyerezi ni ndogo kuliko hiyo ya MCC. Ya Japan ni mkopo nafuu, ya MCC ni ya msaada, 100% free money, gharama yake ni kudhibhirisha tu kuwa tunaheshimu maamuzi ya wananchi wetu kwa vitendo.
 
Hatutaki mambo ya Dr Rutengwe, wakae na hela zao na MCC yao na sisi tutaanzia hapo tulipo.

Usifananishe mfumo wa mtu mmoja mmoja ,ukaulinganisha na Nchi mkuu..
 
Dubai yenye uchumi mzuri na imara hata zaidi ya mara 100 bado inapokea misaada. Tanzania nchi ambayo imeharibiwa na CCM kwa miaka kibao, Magu anadhani tunaweza kulala na kuamka na kubadilisha flow dynamics, badala ya misaada kutoka Marekani kuja Tanzania na kuanza kutoka Tanzania kwenda Marekani!
 
Tusidanganyane. Ni mjinga pekee yake anayeweza kukaa chini na kusema, 'hiyo pesa tunyimwe kwa kuwa tuna uwezo wa kujitegemea'. Hiyo pesa kwa Tanzania ni muhimu sana. Ni hela hiyo ya MCC ndiyo iliyojenga barabara nyingi mpya za lami na madaraja wakati wa JK, pamoja na miradi mikubwa ya umeme intondelea. Leo karibia miradi yote ya ujenzi imesimama.

Dola karibia milioni 500 ni hela nyingi sana kwa nchi kama Tanzania ambayo pesa hiyo ni sawa na makusanyo yote ya kodi kwa mwezi. Ebu jiulize, hivi unaweza kukubali kiurahisi kuwa ukose mshahara wako wote wa mwezi unaoitegemeza familia yako?

Magu asijidanganye, tunatakiwa kujitegemea lakini siyo kwa namna anayoifikiria. Kwa sasa ni wakati wa kukusanya nguvu zote, iwe ni misaada, mikopo, makusanyo ya kodi kwaajili ya kupata nguvu za kuweza kujitegemea mbeleni. Tanzania kwa makusanyo yake ya pesa ya madafu trilioni 1, haina uwezo wa kujitegemea ghafla kutoka kwenye dependence ya 40%.

Magu asitupeleke iliko Zimbabwe ambako kiburi cha Mugabe kinawatesa Wazimbabwe balaa. Madaktari, manesi na walimu Wazimbabwe wameishia kuwa waiters SA. Ni aheri kuwa waiter SA kuliko kuwa daktari Zimbabwe.

Mwalimu naye aliwahi kujitahidi kutaka kufanya haya ya Magufuli, waliokuwepo wanajua. Hata sabauni za kufulia, mafuta ya kupikia na chumvi viliadimika.

Kumbukeni kuwa hiyo 470 milioni ni pesa ya kigeni, na ina impact kubwa kwa Tanzania. Kwa nini Watanzania wachelewe kupata maendeleo au wateseke kwa mambo ambayo ni rahisi kutekeleza? Afadhali tungenyimwa huo msaada kwa kutetea mambo ya msingi, mambo yenye faida kwa Taifa. Hapo tungesema tunalinda uhuru wa Taifa. Lakini sasa tutanyimwa kwa mambo ya kipumbavu, kutetea udikteta uliofanyika Zanzibar!

Hii ni sawa na mtu ambaye ni mchafu, hana choo, hafui nguo zake, anapikia chakula kwenye mazingira machafu. Halafu anatokea jirani anakuambia kuwa nitakujengea nyumba ambayo itakuwa na choo kizuri ndani, itakuwa haina vumbi kwa sababu nitakuwekea tiles LAKINI ili nikufanyie hayo kwanza nataka unioneshe unauchukia uchafu, uache kujisaidia kwenye upenu wa nyumba yako. Halafu wewe unasimama na kusema unaingilia uhuru wangu, kama ni hivyo ni aheri usinipe huo msaada. Naenda kufyeka msitu, nikapande michungwa baada ya miaka 5 nitaweza kujenga mwenyewe kwa sababu nina uwezo.

Kwanza masharti ya MCC siyo kwa faida ya USA, ni kwaajili yetu wenyewe. Yaani udikteta uliofanyika Zanzibar kwa manufaa ya Shein na CCM, udikteta ambao umemwudhi kila mtu mstaarabu Duniani, ndiyo sisi utufanye kuonekana ni wetu wenye msimamo? Kama huo ndiyo msimamo basi ni msimamo wa mtu mjinga.

Juzi Magufuli wakati anazindua mradi wa umeme mradi wa Kinyerezi alisema wazi kuwa hatuwezi kuacha hela ya bure tuliyopewa na Japani kwa sharti la kuchangia 15% ya gharama ya mradi. Pesa itakayotolewa na Japani kwa mradi wa Kinyerezi ni ndogo kuliko hiyo ya MCC. Ya Japan ni mkopo nafuu, ya MCC ni ya msaada, 100% free money, gharama yake ni kudhibhirisha tu kuwa tunaheshimu maamuzi ya wananchi wetu kwa vitendo.
Asante kwa ufafanuzi Mzuri
 
Asijidanganye tutarudi enzi zile za Unga manjano na shida chungu nzima mwenzake enzi hizo alijifanya kiburi na maskini jeuri akatuketea wananchi wake shida na njaa kila kitu hakuna. Katizameni Zimbabwe halafu mtajua mkishiba hamjui shida
 
Labda ieleweke kuwa hii pesa ya MCC siyo msaada kama ile inayopatikana kwa kutembeza bakuli na kulazimishwa kufuata masharti. Hii pesa inatolewa (siyo mkopo) kwa nchi kushindanishwa kwa kutumia vigezo vya demokrasia na utawala bora. MCC ni sawa tu na hile tuzo la Mo Ibrahim kwa viongozi wastaafu Afrika. Tukiikosa hiyo pesa kwa sababu tu ya upuuzi uliofanyika Zanzibar ni sawa na kujitakia maradhi. Ukitaka kufahamu thamani ya hiyo pesa jaribu kuangalia miradi iliyofanyika kutokana na pesa tuliyopata ya MCC1: ujenzi wa barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Songea-Mbamba Bay pamoja na miradi mingi ya umeme vijijini. Miradi hii ya barabara ilifanyika wakati Magufuli akiwa waziri wa ujenzi na urefu wa hizi barabara ni kati alizokuwa anakariri mara kwa mara wakati wa kampeni kama mafanikio ya serikali ya CCM! Asiyeona thamani ya miradi kama hii kiuchumi na kijamii na eti bora tuikose kwa kulazimisha aliyeshindwa uchaguzi Zanzibar atawale kwa nguvu hana uzalendo wowote kwa hii nchi.
 
Huyo fala mwengine Google eti $472 itasaidia nini jiulize babako anazo? Sisi waafrika ni kama manyumbu tu hatujijui hatujitambui tunaenda tu kila kitu sisi ni shida tuuu.
 
Asijidanganye tutarudi enzi zile za Unga manjano na shida chungu nzima mwenzake enzi hizo alijifanya kiburi na maskini jeuri akatuketea wananchi wake shida na njaa kila kitu hakuna. Katizameni Zimbabwe halafu mtajua mkishiba hamjui shida
Hawa jamaa ni mabingwa wa mikakati ya kudhoofisha nchi maskini, inatakiwa kwenda nao taratibu lakini tukijifanya vichwa ngumu tutatengenezewa zengwe na kusambaratishwa tuione dunia chungu.
 
Back
Top Bottom