Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

Tanzania imenyimwa msaada wa fedha za MCC?

nakubaliana na wewe ila tuweke sheria ngumu za kuwabana viongozi wapunguze
wizi maana najua kuacha kabisa awawezi maana naona kama rushwa ni sera ndani ccm
Wewe endelea kuzungusha mikono
 
kinachofuata ni baba wa familiya kutoa kodi kutokana na idadi ya watu kwenye familiya yake(kodi ya kichwa)
 
Kama ni kweli basi safi sana

Huwezi kujivuna kuwa una nyumba na familia ili hali unashindwa kuitunza na kutegemea jirani na marafiki wakutunzie familia yako!! You will have no intergrity na hilo nadhani ndilo analolisisitiza Magufuri. Ni hatari sana mke wa mtu kufadhiliwa na jirani!!!
 
unaufahamu udikteta au unaandika tu? Unaandika ili kuhalalisha utegemezi? Assume MCC isingekuwepo? Je wote waliopiga hatua wamefika hapo kwa ajili ya MCC? Nitajie nchi zingine zinazofaidika na MCC ambazo zimepiga hatua kiasi kwamba tusikitike kwa kukosa hio package ya MCC.

Mkuu hii pesa umeiona ni ndogo sana au kwa sababu amesema rausi wako Magufuli ndio unatetea hata kama tutapata athari sisi wananchi wa hali ya chini?.Hata hali ya maisha iwe vipi raisi bado ataishi mazuri,kazi ipo kwa sisi wa hali ya chini.

Tupunguze mapambio jamani ,kiongozi nae ni binadam anaweza kuteleza pia.
 
Hatuwezi kujitegemea huku Nchi ikiwa Na ukandamizaji wa Demokrasia,Katiba Mbovu, Fikiri kwa Upana Uongozi Wenyewe ndio huu wakina Chenge wamezibiti Bunge Tunajidanganya Mtu Anaharibu anapangiwa kazi Nyingine wakina Maswi Mtu anautoa Mfumo wa Jakaya anaweka watu wake Tunajidanganya anatumbua Majipu Kazi bure
 
Jamani kwenye hii post nimegundua watu wengi uelewa wao ni mdogo sana hasa kwenye mabo ya uchumi na siasa.
1.kwa walewanaosema watu wafanye kazi na sio kuomba omba msaada ,naombeni ni waulize the end product ya kufanya kazi ni nini? maana kazi utazalisha ukizalisha kwa wingi ili upate kipato lazima uuze soko na kwa hao hao wanatoa hiyo mikopo-kumbuka kuna njia nyingi za kuzuia bidhaa yako isiuzike kwenye soko la dunia -maana hizo fedha watato subsidies kwa wakulima wao,haya mniambie hoyo GDP yetu itatoka wapi??
2.investment zote kubwa za madini,gasi na n.k zinahitaji technologia na ma expart , hivyo vyote hatuna na jua hizi investment ndizo zinazochagia kwenye pato la Taifa-na bado hazijaajiri watanzania wengi ndio maana unasikia pato la Taifa linakuwa lakini maisha yetu bado ni chini maana watanzania wengia hawajaajiriwa kwenye hizo sekata.sasa leo wakisema wajitoa hata kwenye uwekezaji tutafanya nini??

Jamani hamna anayependa misaada lakini hali yetu kama nchi bado tunahitaji tena sana ,huwezi ukaikataa misaada gafla athali zake ni kubwa sana kiuchumi,kijamii na kisiasa lazima tuweze kwanza kutengeneza mazingira ya kukikataa misaada,kwanza tuwe na tu import technologia ,tuanzishe viwanda vidogodogo,kutafuta allies wa kufanya nao biashara ambayo itakuwa equall
Mkuu hapa unazungumzia export katika soko gani? la USA au global market?

Je unadhani kwa dunia ya sasa technolojia ipo moja tu na mzalishaji wake ni huyo huyo tu?
Anyway, tutaanza na wavietnam, wachina na hata wazimbabwe maana hakuna namna kuliko kutiwa vidole
 
Twasubiri matokeo ya MCC leo! Nafikiri wakati tunajipanga na kodi zetu,tupate hizo......zitusaidie zaidi
 
Nakubaliana na maneno ya Muheshimiwa Rais kua tusikubali misaada yenye masharti. Ila ni vizuri kama watayaweka hadharani hayo masharti yenyewe tujuwe ni kwa maslaha ya wafadhili au ya watanzania kama ni yetu jee serikali imeyahishimu au la na kwa faida ya nani.
 
Mh. Magufuri, hakikisha Tra inakusanya kodi toka bidhaa zote zilizomo nchini na zinazoingia. usilegeze uzi. nasema nje huku watu wanalipa kodi ya biashara hadi wakulima wadogo wadogo. iweje Tz tusilipe kodi na kuendelea kujidharilisha na vimisaada vya kihuni, kama mliweza kukusanya tril moja kwa kwa mwezi basi mkikaza buti kila mtu akafanya biashara halali na kulipa kodi tutaweza kuongeza ufanisi na weledi katika biashara maana watu wataongeza ubunifu katika bidhaa ili kuhakikisha,wanapata faida na kulipa kodi
 
Wanaopata shida ni wananchi sisi tunachotaka ni kutawala tu.Tutafika Kanaani
 
Naona ccm wanataka kiwadanganya watz kwamba misaada sio kitu wakati wanajua wao ndo wamevuruga! Tunanyimwa msaada kwasababu ya ccm kuvuruga democrasia sasa tunaomia ni wote hata ambao hatuna vyama, inauma sana.
 
ndio raha ya lumumba mkiambiwa ukweli mnakuja na hoja za kipuuuz
Hakuna hoja, and hoja haiwezi kuwa yenye nguvu hasa ya kuendekeza utegemezi, ila sishangai kwa sababu upande wenu ni waliberali
 
Jamani hii misaada siyo tu kwa sababu tu masikini bali ni kama watu mayajiri lakini pia wanakopa pesa kwenye mabenki. Haya ni mambo ya kuwezesha mambo ya maendeleo kufanyika ambapo mwisho wa siku ndunia nzima itafaidika
 
Ngoja tutakapoanza kuchapisha noti ya Trilion 10 kama zimbabwe, ndo tutauona umuhimu wa kufanya kazi kwa mikakati na vitendo badala yakurefusha mdomo kushabikia. Nchi maskin ya kipato na maarifa kama hii, huwezi kushindana na wazungu ukatoka salama, kwa vile watanzania huwa hatufikirii vizuri, yan kama CCM wanavyotumia vyombo mbali mbali kuwahujumu wapinzani wake kisiasa, ndo tools hizo hizo na zaidi wazungu wanazo kukomesha, watu wenye maneno mengi bila vitendo. Tusubiri.
 
tukomae kufanya kufanya kazi wakati viongozi wanakua majizi au kuna sheria gani za kuwabana?
Sasa hata MCC zikija viongozi watazila, bora watunyime tu wakae nazo maana hata zikija hatuzipati na bado tunakwekewa masharti. Bora nusu shari yani tuzikose tusiwe na masharti
 
Nakubaliana na maneno ya Muheshimiwa Rais kua tusikubali misaada yenye masharti. Ila ni vizuri kama watayaweka hadharani hayo masharti yenyewe tujuwe ni kwa maslaha ya wafadhili au ya watanzania kama ni yetu jee serikali imeyahishimu au la na kwa faida ya nani.
Mwambie avunje makubaliano waliyoyasign tokea zamani. Shida kubwa huwezi elewa iko sehemu gani. Makubaliano ya kimataifa hayavunjwi kirahisi. Tuna deni la zaidi ya Trillion 40 hivi wakisema tuzilipe leo utafanyaje? Development is a process mkuu muda wa kujitegemea utafika tu. Magufuli angekuwa na nia ya dhati angerudisha mikataba yote ya kinyonyaji bungeni, huwezi kupata 3% ya madini, 7 years ya gesi ni majaribio kwa wachina, IPTL azalishe asizalishe tumlipe..... ...mengi mkuu kukimbia hela za bure zaidi ya Trillion moja ni kuchelewesha kuunganisha mikoa huku wilaya hatujaanza kuzifikiria kuunganisha kwa lami.Makusanyo ya trillion moja kwa mwezi ni kidogo maana mishahara tu ni zaidi ya nusu ya trillion moja huku kuna mambo lukuki kuendesha nchi.Think big
 
Hakuna hoja, and hoja haiwezi kuwa yenye nguvu hasa ya kuendekeza utegemezi, ila sishangai kwa sababu upande wenu ni waliberali

Hauwezi kuona hoja hapa ,si unaona unavyopiga sarakasi na taulo .....yaani hamna hoja hapa !!!?
 
Misaada yenyewe midogo, sasa hiyo $472 million itasaidia nini! Kila mwaka wanatoa imesaidia nini hadi leo??
Mkuu unasema hiyo $472M ni ndogo tena kila mwaka wanatoa unasema haijasaidia kitu. Sasa kama imetolewa lakini haijatusaidia kitu huoni kuikosa kabisa ndiyo itakuwa na madhara makubwa sana? maana itakuwa leakage kubwa kwenye budget yetu ya FY2016/17 na sijui tutafidia vipi?

Waswahili wanasema ni maneno ya mkosaji. Kiukweli kama hawatatoa MCC kwenye FY2016/17 utakuwa mwaka mgumu sana kutakuwa na mdororo wa uchumi
 
Back
Top Bottom