Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
na ni serikali hiyohiyo inayojenga barabara nchini kote, inajipinda kupeleka maji na umeme vijijini, imejenga shule kila kata, inatarajia kujenga zahanati kila kata huku ikipambana na wakwepa kodi... AMEN
Hi hiiiiii, unasema zile barabara zinazolipiwa na ******* wa EU? Hela za kodi za akina George Michael, ELton John, Freddy Mercury siyo? Wajukuu wa Hitler akina BMW, Audi, VW, BASF etc? Pesa za Tanzania zinatosheleza kulipa mishahara na matumizi ya serikali. Pesa zote za maendeleo zinatolewa na wadhamini ambao wengi ni European Union. Nyie mkiambiwa kujenga tu mnara wa Freddy Mercury na ******* waje kutalii na kuacha madola mnakuja juu. Ila wengine wakizikusanya hela zao na kuwapa nyie, mnakubali. Tuoene aibu na tukome kujisifu kwa kupitia migongo ya wengine. Mtanzania, unaona huku wanasema eti serikali inatoa hela wakati ni kodi yako unayolipa huko.
Kwa hiyo Tanzania kutookalika ndio better alternative?
Ushirombo mimi sikatai kuwepo kwa masikini, lakini ninakuhitaji na wewe utambue tofauti zilizopo. Kama uko Tanzania ukipata muda nenda kakae mtoni kwa aziz ali pembeni ya barabara. Angalia magari yanayopita na watu walioyapanda. Halafu nenda sarenda bridge, angalia magari na waliomo kwenye magari hayo. Labda hii itakusaidia kutambua kuwa kugoma ili kila mwanafunzi akopeshwa asilimia 100 kwa madai kuwa watanzania ni masikini sio jambo la busara.
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
Tehe tehe tehe tehe! Huyu mwanafunzi hapo juu ana hasira sana!!!! Na wala msimlaumu kwa kutumia lugha ya matusi!
Inafika wakati jazba inazidi busara! Zemarcopolo angalia sana!
Kwa hiyo Tanzania kutookalika ndio better alternative?
Serikali na Chuo wanatumia vigezo gani kujua kina nani wana uwezo na kina nani hawana uwezo?
Zemarco,
Umesema vizuri sana. Hili nakubaliana na wewe. Ukikaa maeneo hayo, utaona magari ya bei mbaya yakipita na ni mengi sana.
Nakuomba pia ukakae AIRPORT, uone watoto wao wakichukua MAPIPA (ndege) kwenda shule na wakati wa likizo wakirudi na masanduku yao ya SAMSONITE na kupokewa na wazazi na ndugu kwenye hayo magari..
xxxxxxx mkubwa we!! hujui maisha wanayopitia hao vijana, usijifanye kutaka kuleta hoja hapa, wakati umeshamaliza kusoma, unakula na unakitambi uhuji shid wanazopata watoto wa kike na wa kiume mlimani...................................
mmh naomba nisicomment juu ya hili!!!
1. Hakuna elimu ya juu ya bure na hizi sii enzi za ujamaa..ambapo wanafunzi vyou vikuu walikuwa wachache sana na serikali iliweza kuwagharamia bure!
Au na wewe ulisindikizwa nini? hihiiihiiii. Na mie nikiri nilisindikizwa. Ila ndugu zangu wengi wamesoma pale na wengine wanasoma. Mie na wao ni damu damu na shida zao ni zangu..............
Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika,
Hayo ni maneno ya Machibya, aliyekuwa Rais wa iliyokuwa DARUSO. Maneno yake yanafanya nijiulize, hivi Machibya anaelewa maana ya maneno anayoyasema? Tanzania haitakalika, kwa hiyo watanzania wataenda wapi??? na nini kitafanya isikalike? Nani anampa huyu mwanafunzi kiburi cha kutishia maisha ya watanzania? Hizi lugha zisizo na busara zinaonyesha aina ya uongozi uliokuwepo DARUSO. Na sasa watanzania hawawezi kushangazwa na uamuzi wa kuifuta DARUSO iwapo huu ndio upeo wa viongozi wake.
bold and red text quoted above makes me very sick!!!!!
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
Ninajali welbeing ya watanzania wote na nina ndugu wa hali mbalimbali kimaisha. Hivyo ninachochangia kina lengo la kuboresha nchi yetu na si kupendelea watu fulani. ningekuwa napendelea matajiri ningeunga mkono maoni ya kutaka 100% ya wanafunzi wapewe mkopo.Ila kwa vile natambua mahitaji ni mengi kuliko uwezo ndio maana napendelea sera ya kuwawezesha wanaohitaji zaidi.