''...Tanzania haitakalika'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

''...Tanzania haitakalika''

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jan 20, 2009.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  “Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika

  Hayo ni maneno ya Machibya, aliyekuwa Rais wa iliyokuwa DARUSO. Maneno yake yanafanya nijiulize, hivi Machibya anaelewa maana ya maneno anayoyasema? Tanzania haitakalika, kwa hiyo watanzania wataenda wapi??? na nini kitafanya isikalike? Nani anampa huyu mwanafunzi kiburi cha kutishia maisha ya watanzania? Hizi lugha zisizo na busara zinaonyesha aina ya uongozi uliokuwepo DARUSO. Na sasa watanzania hawawezi kushangazwa na uamuzi wa kuifuta DARUSO iwapo huu ndio upeo wa viongozi wake.
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  alichokosea ni kuwa hata kwa sasa haikaliki....umeme shida, maji, mafuta hakuna, wakazi wa changanyikeni wamekuwa wakimbizi kwao kisa chuo kikuu Dar hawataki wapite... jamani kweli nchi haikaliki tena!!!!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Jiweke kwenye position ya mtanzania mwanafunzi wa UDSM asiyeweza kutimiza masharti hayo ya readmission kabla ya kulaumu hizo lugha 'zisizo na busara' aliyotumia.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo Tanzania kutookalika ndio better alternative?
   
 5. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mimi nilivyomwelewa ni kwamba tukiendekeza hayo matabaka anayoyataja kwa kuunga mkono sera zinazowagawa Watz katika makundi ya matajiri na maskini ni wazi Tanzania haitakaa iwe na amani (haitakalika). Kwa hiyo, wewe umesoma maandishi tu, hukuelewa maana!
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.
   
 8. E

  Edo JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivi ni Tanzania tu ndiyo yenye matabaka?, mbona zipo nchi nyingi zina matabaka hayo na zinakalika! na tangu lini unategemea nchi ikawa na watu sawa! Imeshindikana china itakuwa bongo?
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni sawa na yule kiongozi wa zamani wa daruso ambaye yuko chama cha upindzani inaelekea upinzani unapanga mambo haya kwa masilahi yao ya mbeleni
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  La hasha! A better alternative ni kutoendekeza sera zinazotugawa katika matabaka ya matajiri na maskini, etc.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa tathmini yangu ni kwamba hawa vijana wanatumiwa na watu fulani, ambao wameweza kuwamanipulate kutokana na kutokukomaa kwa wanafunzi hawa kifikra. Ndio maana migomo ya UD siku zote ni ya undergraduate students. Ingekuwa ni migomo genuine mature postgraduate students nao wangekuwa wanagoma.
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Jan 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Unbelievable!

  Labda mimi peke yangu ndiye sivioni.

  Lugha aliyotumia kijana ni ya Jazba ambayo ni kawaida kutoka vinywani mwa wengi. Ni matokeo ya kuchoshwa na kitu flani ambacho mhusika anakuwa hana control ya kauli dhidi ya kitu hicho tena.

  Katika hali ya kawaida sidhani kama angeongea hivyo... Kumbuka: Ni mwanafunzi (kwa maana bado anajifunza tu!)
   
 13. Vica

  Vica Member

  #13
  Jan 20, 2009
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ZeMarcopolo is in the house anatuchanganya,inaonekana hajaelewa vizuri na kama alisoma shule misamiati ilikuwa inampa tabu au anaweza akawa mtoto wa kigogo au mtoto wa mukandara,kwani sioni kama Huyo Rais wa zamani wa chuo kama amekosea kusema hivyo.kwani chuo kunakalika kwa sasa?
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sawa ni mwanafunzi, lakini ili ajifunzi ni wajibu wa wanaojua makosa anayoyafanya wakamkumbusha kuwa anakosea. Na yeye kama ana busara, ni wajibu wake kuomba radhi kwa makosa. Kwa sababu another fact ni kwamba pamoja ya kuwa ni mwanafunzi lakini ni mtu mzima tena ni kiongozi anayepaswa kuwa makini na maneno yake.
   
 15. Vica

  Vica Member

  #15
  Jan 20, 2009
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na Huyo shy asilete usista du hapa!Tukubali tukatae Rais Kikwete ameshindwa nchi!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Vica, with due respect sidhani kama chuoni hakukaliki. Kuna watu wengi tu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida pale chuo. Pili ,hali chuoni ndio hali ya tanzania???
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hawa wanaojiita viongozi wa daruso sijui kama wanaelewa kitu wanachokifanya achiliambali kile wanachokisema.
  Wanang'angania kwua serikali iwalipie asilimia 100 wanafunzi wote na kusisitiza kuwa sera inawanyanyasa wanafunzi kutoka familia masikini wakati sera yenyewe, msingi wake ni kuwasaidia zaidi wanafunzi wasio na uwezo. Hawa-appreciate the fact kwamba serikali, kwa kuona uwezo wake mdogo wa kugharamia elimu, imeamua kuwaangalia waanafunzi wasio na uwezo kupitia sera hiyo, ili wale wenye uwezo watoe nafasi kwa wasio na uwezo kulipiwa na serikali. Huu ni ubaguzi wa aina gani? Je, kutaka matajiri na masikini wote walipiwe 100% huko si kuwanyanyasa wasio na uwezo?
  Kwamba hawaelewi wanachokisema (pamoja na kuwa mkuu Inv. anasisitiza kwua wanajinfunza) kunaonekana kupitia katika matamshi na maandishi yao. wakumbuke kuwa katika hili wao wameshika makali, mwenye kushika mpini akiamua kuvuta kisu, wao ndio watakaoumia.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wakati USA, leo hii Obama anakuwa mtu atakayeifanya NDOTO ya Dr. King kuwa kweli na hivyo kuimaliza hizo ndoto, Tanzania tumeanzia kwa Obama na kwenda nyuma kwenye wenye nazo na wasio nazo. Matabaka yanazidi kutanda. Wengine wanafikiri matabaka kila sehemu yapo na Tanzania lazima yawepo. Ni kweli ila details ndiyo zinaleta shida siku zote. Wanasema "Demokrasia ni udikteta kwa walio wachache".
  Nchi zilizoendelea, matajiri na watu wa hali ya kati ni wengi kuliko masikini. Tanzania ni kinyume chake. Hii inapeleka kuwa na Watusi (10%) kuwatawala Wahutu (90%). Amini usiamini, siku moja mapanga yatatembea. Na wala hutajua yalianza-anzaje. Ila kama masikini ni 10%, hawawezi kutembeza mapanga kwa watu 90%.
  Haihitaji kuwa na akili sana au msomi sana ili kuelewa maneno ya kijana. Kama ni kijijini basi utasifiwa kuwa na wewe ni NABII kwani ulijua mapema kuwa hili litatokea. Ikumbukwe kuwa sisi hatupishani sana na Wakenya. Utalaani vyama vya upinzani weee lakini Mkenge umeutaka mwenyewe kuukalia.
   
 19. Vica

  Vica Member

  #19
  Jan 20, 2009
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe Marco Vipi!?Aombe msamaha kwa kosa ganikama ni mwanafunzi je ni viongizi wangapi wa siasa walokwenda shule amabo wamekuwa wakitoa kauli kali kama hizo na husemi lolote!
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
  Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!
   
Loading...