Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.
ZeMarco,
Nyerere aliposhambuliwa kuwa enzi zake alikuwa anaweza mawaziri wote kwenye baraza lake la Mawaziri wa dhehebu la Kikristo, unajua alijibu vipi?
"....... wanasema mimi nilikuwa naweza WAKATOLIKI wenzangu kwenye baraza la mawaziri. Wakati huo Wakatoliki tuko watatu, mimi .... na ..... (jina nimesahau) na mwisho ni George Kahama ambaye alikuwa na wake 2.......".
Nafikiri DARUSO hawakuwa wajinga kugoma halafu leo hii walalamike kuwa hii system inasaidia tu wale walionazo. Jana nimesoma kuwa wale wasio na uwezo waandike barua kwa Waziri. Sasa barua ya nini wakati mambo ni mazuri kabisa kama wewe unavyoidai? Mbona umekaa na mambo ya kulazimisha tuamini jambo lenye utata? Duuu, Makatibu kata wengi dunia hii....