TANROAD KUUZA ENEO LA KEEP LEFT SI SAWA

TANROAD KUUZA ENEO LA KEEP LEFT SI SAWA

Shetemba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2018
Posts
955
Reaction score
984
Hapa Mbezi Luis kwa Yusuf Kuna mzunguko ambao magari yote yanagawanyika,yanayotolka Kibaha, yanayotoka kinyerezi,yanayotoka Mpigi magoe yanayotoka stendi ya Magufuli yote yanakutania hapa,sasa sijui ni uroho au ulevi mtu anatoa kibali cha kuweka makontena ya biashara katika eneo hili, bila kujali kwamba eneo ili linapongoza kwa ajali za kila mara
 
Walikuwepo wakina manka hapo wanafanya biashara wakafukuzwa km mbwa, siku hizi manka yupo safar bar kwa nyuma
 
Kwahiyo mzunguko ndo keep left?
 
Mkuu Naomba unisaidie tofauti ya keep left na round about
Keep left ni instruction ya barabarani inayomaanisha ukae upande wa kushoto kutoka kwenye kizuizi kilichopo barabarani au kutoka ilipo alama ya mstari wa katikati ya barabara , au muda mwingine inachorwa mishale ili kusaidia kuongoza magari haya maelekezo yanatolewa kwa nchi zinazoumia upande wa kushoto wa barabara kama kwetu Tz.

Round about ni mzunguko maalum unaotengenezwa kwenye makutano ya barabara ambayo kazi yake ni kusaidia magari kubadilisha muelekeo wowote bila kusimama.

Kwahiyo round about ni mzunguko unaotengenezwa kwenye makutano ya barabara na keep left ni maelekezo namna gani utumie barabara, zipo nchi zinazunguka roundabout zikiwa upande wa kulia kwahiyo siyo sawa kuiita round about kuwa ni keep left
 
Back
Top Bottom