TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,649
Reaction score
4,756

FUNDI SANIFU WA UMEME (ELECTRICAL TECHNICIAN)​


Tunatafuta Fundi Sanifu wa Umeme mwenye ujuzi na uzoefu wa kufanya kazi za umeme katika majengo makubwa ya biashara, viwanda na nyumba za makazi.


Sifa za Mwombaji​


  • Awe na Cheti cha Ufundi (Certificate) au Diploma ya Umeme kutoka NACTVET (zamani NACTE) au VETA.
  • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2, unaoweza kuthibitishwa.
  • Awe na uwezo wa kusoma na kutafsiri michoro ya umeme (Electrical Drawings).
  • Awe na ujuzi wa Electrical Installation, Wiring, Testing, Commissioning, Maintenance na Fault Finding.
  • Awe na uwezo wa kufunga na kuhudumia mifumo ya taa, power outlets, distribution boards, MCCBs, MCBs, earth systems na vifaa vingine vya umeme.
  • Awe na uwezo wa kutumia vifaa vya kupimia umeme kwa usahihi.
  • Awe na uelewa wa kanuni za usalama kazini (Electrical Safety Standards).
  • Awe na uwezo wa kupanga kazi zake, kutekeleza kwa wakati na kufanya kazi bila kusimamiwa kwa karibu.
  • Awe na uwezo wa kuandaa taarifa fupi za kazi zilizofanyika na kutoa mapendekezo ya matengenezo.
  • Awe na uwezo wa kushirikiana vizuri na wateja pamoja na timu ya kazi.
  • Awe anaipenda kazi yake, ni mchapakazi, mwaminifu na mwenye nidhamu ya kazi.

Eneo la Makazi​


Mwombaji anatakiwa awe anaishi maeneo ya Tegeta, Wazo au maeneo ya karibu. Waombaji wanaotoka mbali wanakaribishwa iwapo watakuwa tayari kuhamishia makazi yao maeneo hayo.


Nyaraka za Kuambatanisha​


Maombi yaambatane na:


  • Barua ya maombi.
  • CV ya kina.
  • Nakala za vyeti vya taaluma na elimu.
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa unakoishi (makazi ya kudumu).
  • Majina na mawasiliano ya wadhamini watatu (3), ambao ni:
    1. Supervisor wa sehemu uliyowahi kufanya kazi.
    2. Mjumbe au kiongozi wa Serikali ya Mtaa unakoishi.
    3. Ndugu wa karibu au mzazi.

Namna ya Kutuma Maombi​


Tuma maombi kupitia:



Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 2 Agosti 2026 saa 6:00 usiku.


Waombaji wenye sifa zinazohitajika tu ndio watakaowasiliana kwa hatua zinazofuata za usaili.
 
Mfumo wa elimu ya bongo ni tatizo inatuaminisha kuamini vyeti na nyeti vyenyewe vinapatikana kwa kukariri tu unaf
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom