Tanganyika na Zanzibar zinatumia kikokotoo gani kugawana fedha?

Ilipoanzishwa BOT - Pesa za Zanzibar zilizokuweko East Africa Community zilichukuliwa zikaanzishiwa hio BOT na Mpaka leo Zanzibar haipati mgawo wowote kutoka BOT- Nafikiri tungelianzia hapo na Tukaweka wazi kati ya Zanzibar na Tanganyika share zilikuwaje?
Unajua unachoandika?

1. 4.5% ya pato la Tanganyika inakwenda Zanzibar , unafikiri inatoka wapi?
2. Pitia bajeti ya Zanzibar, subsidy zinatoka wapi ?
3. Gharama za kuendesha muungano, pesa zinatoka wapi?
4. 21% ya ajira , gharama analipa nani?
5. Wizara ya mambo ya ndani, nje , muungano nani analipa gharama?
6. Madeni ya mikopo ya Zanzibar, nani analipa?
7. Wale Wabunge Dodoma nani analipa gharama?
8. Muuliza Salimin , Karume , Shein na Mwinyi, Mishahara ya SMZ inatoka wapi

Orodha inaendelea! Hesabu zikipigwa, hiyo pesa ya Bank kuu ni kama tone la maji baharini
 
Jeshi ni taasisi kubwa sana ikiwa na watumishi, zana n.k. Bajeti yake ni kubwa
Gharama za kuendesha jeshi letu zinalipwa na nani? Gharama zinatoka hazina na hakuna kumbukumbu za Zanzibar kuchangia mapato au matumizi ya muungano.

Siyo Marais wastaafu tu hata Wafanyakazi wa kawaida wa muungano na ajira za Tanganyika (21%) wanalipwa na Tanganyika. Wanposataafu malipo ya kustaafu na pensheni zao ni gharama za kodi za Watanganyika. Zanzibar haina mchango kwa mujibu wa Gavana Ndulu RIP.

Na hapa ndipo watu waelewe, kwamba, Wazanzibar wana ''special ajira 21%' iwe katika katika mambo ya muungano au yasio. Wanalipwa Mafao na mishahara kutoka kodi za Tanganyika.
Wanastaafu na kuhudumiwa kwa kodi za Tanganyika.

Wabunge wakimaliza miaka 5 wanalipwa na kodi za Tanganyika si SMZ
Lakini hao 21% si nao wanalipa Kodi inayoingia Tanganyika kwa kuwahudumia watanganyika? Wanalipa PAYE nk hukuhuku Tanganyika, kama ni hivyo wanastahili kulipwa mafao. Mfano, Kuna wazanzibar wanafundisha vyuo vikuu vya Muhimbili, UDSM, etc kufundisha watoto na WA Tanganyika.
 
Ilipoanzishwa BOT - Pesa za Zanzibar zilizokuweko East Africa Community zilichukuliwa zikaanzishiwa hio BOT na Mpaka leo Zanzibar haipati mgawo wowote kutoka BOT- Nafikiri tungelianzia hapo na Tukaweka wazi kati ya Zanzibar na Tanganyika share zilikuwaje?
Kwani mshahara wa Rais wa jmt analipwa na upande gani?
 
Kwaiyo ,ni silias kabisa kwamba gharama za muungano hazijulikanai? naona ni kama kama vile bara ndio wanaona muungano ni bora kwao ndio maana kuna vtu ata vikiwaumiza wanapuuzia au labda wanaona si jambo kubwa kwa maono yao
Huu muungano Kuna upande ulitumia ujanjaujanja kuufanikisha, inawezekana kulikuwa na mkono wa mabeberu kwenye huo mpango. Na hiyo ndiyo inayosababisha anaeupinga huu muungano atafanyiwa chochote bila wazungu kutoa lawama au kulaani.
 
Lakini hao 21% si nao wanalipa Kodi inayoingia Tanganyika kwa kuwahudumia watanganyika? Wanalipa PAYE nk hukuhuku Tanganyika, kama ni hivyo wanastahili kulipwa mafao. Mfano, Kuna wazanzibar wanafundisha vyuo vikuu vya Muhimbili, UDSM, etc kufundisha watoto na WA Tanganyika.
Kumbuka hiyo ni favor, hakuna tatizo la watu wenye sifa Tanganyika!
Kuna vijana wengi sana wa Tanganyika wanaozihitaji nafasi zao na wanaweza kuzitumikia

Vijana wangapi wanatembea na bahasha za khaki kwa nafasi zile zile walizozuiwa kwa 21%
In fact SMZ ilitakiwa ilipe mishahara ya 21% kwasababu Muungano unaajiri watu wao kuliko SMZ

Nafasi za ajira zinaweza kubaki 100% Tanganyika bila tatizo. 21% haijulikani hesabu zake ni favor kwa Wazanzibar. Kama wanadhani wanaonewa, waondoke warudi kuajiriwa na SMZ.

Taasisi na Wizara za muungano ni za Tanganyika kwasababu kuna mbadala Zanzibar!
21% ni ya ajira za Watanganyika, uwepo wa Wazanzibar ni favor tu kwa neno muungano.

Ikiwa unadhani PAYE wanalipa, SMZ iliwape wabunge wake Dodoma wabaki na PAYE !!
SMZ ilipe mishahara na wabaki na PAYE.
Kwasasa sivyo, SMZ inapata pesa za PAYE wanaolipa mishahara inayotoa PAYE ni Watanganyika.

Kwanini Baraza la Wawakilishi lina wajumbe wachache kuliko Wabunge wanaokuja Dodoma!

JokaKuu
 
Kwani mshahara wa Rais wa jmt analipwa na upande gani?
Unapoongelea malipo ya upande gani unakosea! Kwanza tueleze nani anachangia nini.
Huwezi kuwa na malipo kama huna chanzo. Tueleze kwanza chanzo cha mshahara ni kipi halafu tutajua nani anamlipa. Usizunguke zunguke, kabili hoja kama ilivyo!
 
Huu muungano Kuna upande ulitumia ujanjaujanja kuufanikisha, inawezekana kulikuwa na mkono wa mabeberu kwenye huo mpango. Na hiyo ndiyo inayosababisha anaeupinga huu muungano atafanyiwa chochote bila wazungu kutoa lawama au kulaani.
Hili ni tatizo la Watanganyika na Wazanzibar, Mabeberu ni kutafuta tu kukwepa ukweli

Jiulize leo Wazanzibar wako wapi? Leo hoja za Maalim kuhusu muungano zipo wapo
Wako wapi waliosimamia hoja ya muungano kama VP O.Masoud? Ukimya unaletwa na nini?
 
Unajua unachoandika?

1. 4.5% ya pato la Tanganyika inakwenda Zanzibar , unafikiri inatoka wapi?
2. Pitia bajeti ya Zanzibar, subsidy zinatoka wapi ?
3. Gharama za kuendesha muungano, pesa zinatoka wapi?
4. 21% ya ajira , gharama analipa nani?
5. Wizara ya mambo ya ndani, nje , muungano nani analipa gharama?
6. Madeni ya mikopo ya Zanzibar, nani analipa?
7. Wale Wabunge Dodoma nani analipa gharama?
8. Muuliza Salimin , Karume , Shein na Mwinyi, Mishahara ya SMZ inatoka wapi

Orodha inaendelea! Hesabu zikipigwa, hiyo pesa ya Bank kuu ni kama tone la maji baharini
Sasa kama hayo unayosema ni ya kweli, kwanza ifufuke hio Tanganyika. Halafu tuweke wazi matumizi na Mapato ya Muungano, ya Zanzibar na Ya Tanganyika ni yepi. Hapo ndio utajuilikana ukweli
 
Nadhani tuache uvivu wa kutembea, nendeni Zanzibar kama mnataka kwenda Zanzibar. Zanzibar ni Tanzania kabisa hakuna matata na watanganyika. Ukifika Zanzibar utawakuta wamasai wengu na lubega zao, kuna makabila yote ya Tanganyika yanafanya chochote mtaa wowote bila bughuza. Kama unazo hela nenda zanzibar ukafungue chochote kile hakuna bughuza hiyo watu tunayoisema na kuifikiria. UKienda Zanzibar fuata sheria na kanuni kama vile unavyokwenda ufipani, usukumani, umasaini, utangani, uarabuni, umarekani, nk baaasi. Mimi nilichokuwa nauliza ni kanuni ipi tunatumia tunapogawana kisungura chetu kwenye nchi yenye watu 37 mil ikiwemo Zanzibar, maana mikoa ya Tanganyika ni mikubwa sana na ina idadi kubwa ya watu waliotawanyika kwenye eneo kuuubwa kuliko mikoa, Wilaya na Kata za Zanzibar.

Mtu anaetutakia mema na kuutakia muungano hawezi kuhoji kuhusu muundo wa muungano, maana miungano yoote duniani hakuna uliokuwa shwari, hata marekani kuna majimbo yanayotamani kujitenga na kuwa nchi uhuru, kule Uingereza kuna mgogoro wa muunguno kule Ireland. Muungano ni kama ufupi na urefu, weusi na weupe tu, wazazi wako walikosea kuona wafupi na kuzaa mfupi na kupatia kuoana werefu na kuzaa mtoto mrefu kwaajili yako. Kazi yetu sisi ni kuuboresha muungano kwa kuuvalisha suti, kuupeleka salon, na kuupaka udi ili upendeze lakini sio kubadili ufupi na urefu wa mtu tena. Tuondoe kero tunazoziona kuwa ni za wazi kabisa. Mfano, mnaweza kuuboresha zaidi kwa kuunda serikali za majimbo na Zanzibar ikabaki kama ilivyo lakini ikahesabika kama jimbo mojawapo.
 
Articles za union, ziliweka Tume ya pamoja ya fedha. Zanzibar na Tanzania Bara, zilitakiwa kuchangia gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano.

Ili Zanzibar ichangie gharama za uendeshaji wa muungano, ni kwanza gharama hizo ziainishwe. Ili gharama za uendeshaji wa muungano ziainishwe, lazima tuwe na serikali 3. SMZ Zanzibar wajibebe, STB, Tanzania Bara wajibebe, na serikali ya JMT, hii ndio ichangiwe na SMZ na STB.

Kwa sasa ndani ya serikali ya JMT, there is no demarcation ya gharama za uendeshaji wa muungano kwa sababu serikali hiyo hiyo ya JMT ndio serikali ya muungano kwa wizara za muungano, at the same time ndio serikali ya Tanganyika kwa shughuli ambazo sio za muungano.

Zanzibar ina haki na uhalali wa kugomea kuchangia gharama zisizojulikana, as a result, ni Tanzania Bara pekee ndio inagharimikia gharama za uendeshaji wa muungano.
P
Zanzibar unaitamka kama Zanzibar,Tanganyika unaitamka kama Tanzania Bara-sasa Tanzania bara ndio Nchi gani???
 
Nadhani tuache uvivu wa kutembea, nendeni Zanzibar kama mnataka kwenda Zanzibar. Zanzibar ni Tanzania kabisa hakuna matata na watanganyika. Ukifika Zanzibar utawakuta wamasai wengu na lubega zao, kuna makabila yote ya Tanganyika yanafanya chochote mtaa wowote bila bughuza. Kama unazo hela nenda zanzibar ukafungue chochote kile hakuna bughuza hiyo watu tunayoisema na kuifikiria. UKienda Zanzibar fuata sheria na kanuni kama vile unavyokwenda ufipani, usukumani, umasaini, utangani, uarabuni, umarekani, nk baaasi. Mimi nilichokuwa nauliza ni kanuni ipi tunatumia tunapogawana kisungura chetu kwenye nchi yenye watu 37 mil ikiwemo Zanzibar, maana mikoa ya Tanganyika ni mikubwa sana na ina idadi kubwa ya watu waliotawanyika kwenye eneo kuuubwa kuliko mikoa, Wilaya na Kata za Zanzibar.

Mtu anaetutakia mema na kuutakia muungano hawezi kuhoji kuhusu muundo wa muungano, maana miungano yoote duniani hakuna uliokuwa shwari, hata marekani kuna majimbo yanayotamani kujitenga na kuwa nchi uhuru, kule Uingereza kuna mgogoro wa muunguno kule Ireland. Muungano ni kama ufupi na urefu, weusi na weupe tu, wazazi wako walikosea kuona wafupi na kuzaa mfupi na kupatia kuoana werefu na kuzaa mtoto mrefu kwaajili yako. Kazi yetu sisi ni kuuboresha muungano kwa kuuvalisha suti, kuupeleka salon, na kuupaka udi ili upendeze lakini sio kubadili ufupi na urefu wa mtu tena. Tuondoe kero tunazoziona kuwa ni za wazi kabisa. Mfano, mnaweza kuuboresha zaidi kwa kuunda serikali za majimbo na Zanzibar ikabaki kama ilivyo lakini ikahesabika kama jimbo mojawapo.
Kama unaweza Fanya chochote zanzibar, basi njoo uchukue hela ukanunulie shamba hecta 50.Pia fungus makanisa angalau 10 kwenye mitaa tofauti tofauti.
 
x
chaajabu hata sherehe hzo za muungano pesa hutoka bara pekee! na endapo ikitokea sherehe zinaahirishwa wanataka mgawanyo sawa wa fedha ambazo zi getumika kwenye sherehe.... sion faida yao hawa wa baharini
 
Zanzibar unaitamka kama Zanzibar,Tanganyika unaitamka kama Tanzania Bara-sasa Tanzania bara ndio Nchi gani???
Viongozi wa Tanganyika wanalazimisha Zanzibar iitwe Tanzania visiwani lakini wenyewe hawalitaki hilo jina wanapenda iitwe Zanzibar yenye wimbo wa taifa na bendera.
 
Sasa kama hayo unayosema ni ya kweli, kwanza ifufuke hio Tanganyika. Halafu tuweke wazi matumizi na Mapato ya Muungano, ya Zanzibar na Ya Tanganyika ni yepi. Hapo ndio utajuilikana ukweli
Hivi ni kipi rahisi kati ya kuifufua Tanganyika au kuiondoa Zanzibar ili kuwe na Tanzania moja?
 
There's no first and hard rules, Zanzibar ni wenzetu, tunaweza kugawana hadi 50/50 na hakuna ubaya wowote, Ila uwiano wa kuwianika kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ni asilimia 4.5% kwa 95.5%.
P
Sawa ni wenzetu!..kwani hiki tunachogawana kinatoka wapi?..Je, ni msaada?..au ni kodi inayotoka KWA WATANGANYIKA lakini pia hatuwez kugawana 50/50 ili hali Tanganyika tunawazid kwa kila kitu!..hadi makusanyo ya kodi kwa sasa nauchukia muungano
Sisi huku mafuta ya kula tu ni balaa kipande cha sabuni ni 500/=...keki yetu inaliwa zanzimba
 
Sasa kama hayo unayosema ni ya kweli, kwanza ifufuke hio Tanganyika. Halafu tuweke wazi matumizi na Mapato ya Muungano, ya Zanzibar na Ya Tanganyika ni yepi. Hapo ndio utajuilikana ukweli
Hakuna cha mapato ya muungano, kilichopo ni mapato ya Tanganyika.
Hivi unajua Bajeti ya Zanzibar? Hivi unajua kuwa makusanyo ya kodi Zanzibar kwa siku au mwezi ni madogo kuliko baadhi ya Kampuni nchini.

Unachosema ni kweli, tunaitaka Tanganyika ili isimamie shughuli zake za sasa kama Tanganyika.
Mambo ya Tanganyika ni ya muungano na Tanganyika haina kauli juu yake kwasababu hainonekani japo ipo.

Mfano; kuna mamlaka ya anga Tanzania (TAA) halafu mamlaka ya anga Zanzibar (ZAA)
Kuna sababu gani za Wajumbe wa bodi ya TAA kuwa na Wazanzibar?
Kwanini Wazanzibar wanashughulikia mambo yasiyowahusu! Je, hii ni kwa ajili ya ajira?

Orodha inaendelea
Mamlaka ya bandari Tanzania( TPA), Mamlaka ya bandari Zanzibar (ZPA)
Shirika la viwango Tanzania (TBS), shirika la viwango Zanzibar (ZBS)
Mamlaka ya chakula na Dawa(TDMA), Mamlaka ya Dawa Zanzibar (ZFDA)
Malaka ya usafiri Tanzania (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri Zanzibar
Taasisi ya kuzuia rushwa Tanzania(TAKUKURU), Mamlaka ya kuzuia rushwa Zanzibar
Bodi ya mikopo ya wanafunzi Tanzania( HESLB), Bodi ya mikopo Zanzibar (ZHESLB)
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya mawasiliano Zanzibar
etc

Hizo ni baadhi tu ya Taasisi, swali la kujiuliza hizi za Taasisi za Tanzania ni za nani kama si za Tanganyika? Ikiwa sivyo zile za Zanzibar ni za nani na zinasaidiaje muungano?

Kumbuka hakuna Mtanganyika anayeajiriwa katika taasisi za Zanzibar
Kuna asilimia 21 imetengwa kwa Zanzibar kwa Taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania

Lakini pia hizi Taasisi za Tanzania ambazo wamo Wazanzibar wengi kwa asilimia 21% zinagharamiwa na kodi za Watanganyika, Zanzibar haina mchango!

Hapo hazitajwa Wizara zinazogharamiwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania

Ikifika hapo Watanganyika na hasa vijana wakiwemo wa CCM wajiulize!
 
Mara nyingi huwa ninajihoji mwenyewe, maswali mazuri kama haya tunamuuliza nani ayajibu? Zanzibar haikuhusika hata kidogo na kuiua Tanganyika, ni watanganyika wenyewe ndio waliohusika, na mtu sahihi wa kuyajibu haya maswali angekuwa Nyerere, nae hayuko. Mwl. Nyerere lazima alikuwa na mpango wake mahususi wa kuiua Tanganyika, hakuwa zuzu yule. Lakini lazima wote tukubali kuwa huo mkakati wake (kama ulikuwepo) ulishindwa kama ilivyoshindwa Ujamaa na kujitegemea na Azimio la arusha. CCM Tanganyika ndo sasa iseme wahat next.
 
The formula ya kikokotoo cha mgao wa fedha kwa Tanzania Bara na Zanzibar, ni kutumia formula ya eneo, ambayo eneo la Zanzibar ni 4.5% ya eneo la Tanzania Bara.

Kila Mkoa ukipata wa Bara ukipata TZS 1.B jumla ni 26.B na Zanzibar 2.5B. Kufuatia Zanzibar kuwa na the minority status, it's usually gets a little bit more, hata kwenye ajira, kwenye mabalozi, kwenye Mawaziri, kwenye mikopo, kwenye scholarship na kwenye kila kitu.
P
Hapo kwenye ajira ndo kuna shida inabidi zile taasisi za muungano ndo iwe hivyo ila hizi tasisi zisizokuwa za muungano zibaki kwa wabara. Lakini saiv ni tofauti wazenji wameajiriwa mpaka halmashauri

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom