Tanganyika na Uhuru wa Zanzibar

Tanganyika na Uhuru wa Zanzibar

Zanzibar hawatakubali kwa sababu pakiwa na mfumo mmoja wa ushuru bei za bidhaa Zanzibar zitapandana na hivyo kuwaumiza wazanzibari.
Sijakuelewa. Zanzibar inakuwa nje ya Muungano ki vipi? Utasemaje sio nchi wakati ina Rais wake, bunge lake, serikali yake, mfumo wake wa kimahakama? Na akienda Rais wa JMT anakuwa mgeni wa Rais wa Zanzibar? Aidha, Zanzibar inaweza kutunga sheria ambazo zinamnyima au kumpunguzia haki mtu wa bara katika maeneo ya umiliki wa ardhi, ushiriki kwenye siasa, ajira n.k.? Kuna wakati machogo walikuwa wanalazimika kupata kibali maalum kabla ya kuoa binti wa kizanzibari. Zanzibar ni nchi bwana.

Amandla...
Je unaufahamu mfumo wa TANCIS?
 
Muungano finito. Inatakiwa pande zote mbili ziukubali. Ndivyo ilivyokuwa Czechoslovakia. Upande mmoja ulikataa, mwingine ulikubali wakagawana nchi. Kuwauliza wazanzibari peke yao kutaacha uwezekano wa hapo mbele kutokea watanganyika ambao watasema walilazimishwa tu.

Amandla...
Inaelekea nilikosea. Hapakuwa na referendum Czechoslavia bali wanasiasa walikubaliana kutengana ingawa wananchi wengi hawakutaka nchi igawanyike.

Amandla...
 
Hiki unachoongea sidhani kama kina ukweli sana, miaka ya 70,80 hadi 90 Zanzibar ilikuwa ni eneo ambalo bidhaa nyingi zilikuwa zinapatikana, akina mama kutoka bara walikuwa ndio wanatoka bara na kwenda kununua Zanzibar lakini kwasasa hali ni tofauti ambapo akina mama kutoka Zanzibar ndio wanaotoka Zanzibar na kwenda kununua bara hususan Kariakoo. Kinachonunuliwa Zanzibar sana sana ni vitu used labda na marashi pekee! Je unaliongeleaje hilo?
Nchini Zanzibar TRA wanasimamia kodi za customs, income na excise peke yake. ZRB wanasimamia nyingine. K.m. VAT Zanzibar ni 15% wakati bara ni 18%. Nadhani hii ndio inachangia bei kuwa chini Zanzibar.

Amandla....
 
Napenda sana niione ramani ya Tanganyika pekee na pia ramani ya Zanzibar pekee, then ramani ya Tanzania.
Hii itasaidia kuzielewa nchi zilizoungana kama zikitengana zitaonekanaje kiramani kwa jicho la kimataifa au hata kabla ya kuungana tarehe za nyuma ya April 26, 1964 ramani zao zilikuwaje?
 
Nchini Zanzibar TRA wanasimamia kodi za customs, income na excise peke yake. ZRB wanasimamia nyingine. K.m. VAT Zanzibar ni 15% wakati bara ni 18%. Nadhani hii ndio inachangia bei kuwa chini Zanzibar.

Amandla....

MKuu umeshawahi kufanya Biashara Zanzibar? TRA na ZRB wote wanabanana hapohapo, Kila mmoja anakuchomoa pesa
 
Suluhisho la matatizo yetu ni kugawana Mbao, Kila mmoja abaki na nchi yake, Muungano wa kinafiki sana
 
MKuu umeshawahi kufanya Biashara Zanzibar? TRA na ZRB wote wanabanana hapohapo, Kila mmoja anakuchomoa pesa
Sijawahi kwa kweli. Kwa hiyo Zanzibar mnalipa VAT mara mbili? Ya TRA na ya ZRB?

Amandla...
 
Sijawahi kwa kweli. Kwa hiyo Zanzibar mnalipa VAT mara mbili? Ya TRA na ya ZRB?

Amandla...
Nilikuulizia kuhusu mfumo wa TANCIS ambao unatumika na TRA kukusanya kodi, nakuomba kaupitie uusome kisha urudi hapa kwenye mada yako.
 
VAT ni VAT na ZRB ni ZRB
VAT = Value Added Tax
ZRB = Zanzibar Revenue Board
Kaupitie mfumo wa TANCIS ndipo uje uipitie tena mada yako.
 
Nimewasikia watu wakisema yafuatayo kuhusu Zanzibar:
1. Zanzibar inapaswa kupata uhuru kamili kutoka kwenye utawala wa Tanganyika.
2. Tanganyika ipate Katiba yake.

Ninachojiuliza ni kuwa Zanzibar itakuwaje nchi huru kamili ndani ya Muungano? Nchi zikiungana si kila moja zinapoteza sehemu ya uhuru wake na kuuweka kwenye Muungano wao? Watu wanasema kuwa lazima Zanzibar wawe na passport zao. Sawa, lakini hii si ina maana Zanzibar iwe na balozi zake na iwe na mamlaka kamili kuhusu uhamiaji? Ni nchi gani ambayo ni Federation ambayo constituent countries kila moja ina passport yake? Sijawahi kusikia passport za Scotland, Wales, Catalonia, Quebec n.k. Tukifikia hapo maana yake hamna Muungano.

Kuna watu wanakalamika kuhusu kodi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Kuwa mtu ukinunua kitu Zanzibar,ukikileta bara unatozwa kodi tena. Si ndivyo ilivyo kati ya nchi mbili huru? Hivi wanadhani serikali huru ya Tanganyika itakubali vitu viingie kutoka Zanzibar bila kutozwa ushuru?

Mimi binafsi sioni mantik na logic ya kuwa na nchi mbili huru ndani ya Muungano. Kwa vyovyote vile patatakiwa kuwa na serikali ya Muungano ambayo itachangiwa na nchi hizo mbili. Ingawa uchumi wa Tanganyika ni mkubwa sana ukilinganisha na Zanzibar, sidhani kama serikali yake itakubali kuchangia zaidi ya mwenzao bila kupata upendeleo fulani.

Nimesikia tena kuwa wazanzibari wangependa kuwa na serikali ya mkataba kama vile ilivyo EU. Wanachosahau ni kuwa EU sio nchi. Na sisi tukiwa na mfumo kama huo ina maana hamna Muungano kama nchi. Itakuwa bora kama nchi hizo zitashirikiana katika jumuia za nchi rafiki kama EAC, SADC n.k. Kwa msingi huo Zanzibar hawatastahili upendeleo tofauti ya ule wanaopata Kenya, Uganda na Rwanda. Vile vile Tanganyika haitapata upendeleo Zanzibar. Hii hali itakuwa rahisi kwa Tanganyika maana hali ilivyo watanganyika hawapati upendeleo wowote wakiwa Zanzibar wakati wazanzibari wana haki sawa na watanganyika wakiwa Tanzania Bara.

Inazungumziwa kupotea kwa identity ya Zanzibar wakisahau kuwa watanganyika ndio hawana identity yeyote. Na maana ya Muungano wa nchi ni kuwa identity zetu zinakuwa chini ya identity ya umoja wetu. Mscot anajivunia uscotish wake lakini anajua akitoka nje ya UK , identity yake kubwa ni ya ubritish. Mzanzibari anayesema kuwa haikubali identity ya utanzania ni kuwa hautambui Muungano.

Kuna malalamiko kuhusu maamuzi kuhusu mambo ya Zanzibar kufanyika Dodoma lakini wanasahau wabunge wa Zanzibar wana uwezo wa kuzuia bajeti ya wizara isiyo ya Muungano ambayo shughuli zake zinahusu Tanzania Bara peke yake. Hamna mtu wa bara ana nafasi ya kufanya hivyo katika Bunge la Zanzibar.

Maoni yangu ni kuwa hii hatua ya Chadema ya ku "pander" kwa wazanzibari ni misguided unless kama lengo lao ni kuvunja Muungano. Kuwageuza watanganyika kuwa oppressors wakati ni wao wenyewe waliochinjana baada ya Mapinduzi na uhuru wao ulibinywa sana chini ya utawala wa Karume ni kutowatendea haki watanganyika ambao kwa kusema kweli wamekuwa wavumilivu sana.. Wengi wa wazanzibari walikimbilia bara kuepuka mkono wa chuma wa utawala ule. Na walipokelewa bara bila masharti yeyote.

Kwa mawazo yangu, kabla hata ya kuzungumzia Katiba mpya kuna haja ya kuwa na referendum kuhusu Muungano wenyewe. Na raia wa pande zote mbili waulizwe kama wanautaka au la ( watanganyika nao waulizwe ili kuondokana na dhana kuwa suala hili ni la wazanzibari peke yao). Baada ya hapo pande zote katika hii debate zieleze faida na hasara ambazo kila upande zinapata katika Muungano. Na zitakazopatikana baada ya kutengana. Kama upande mmoja utakataa basi tutengane kiungwana kama walivyofanya Czech Republic na Slovakia.

Pande zote mbili zikikubali ndio Katiba Mpya iandikwe ikiainisha ni aina gani ya Muungano tuwe nao na mgawanyo wa majukumu uwekwe wazi. Hii kuambiana kuwa tunaweza kuwa na Muungano wa nchi mbili zenye uhuru kamili ni kudanganyana. Tukiungana kila nchi itapoteza uhuru wake kwa kiasi fulani. Hatuwezi kula keki na tukabaki nayo. Ndio ukweli wenyewe.

Amandla...
naunga mkono hoja
p
 
Nilikuulizia kuhusu mfumo wa TANCIS ambao unatumika na TRA kukusanya kodi, nakuomba kaupitie uusome kisha urudi hapa kwenye mada yako.
Tanzania Customs Integrated System inahusiana nini na mada hii? Ninavyojua inatumika ku track mizigo na imekudiwa kuboresha clearance ya mizigo. Sasa inahusiana nini na kodi kati ya Zanzibar na JMT?

Amandla....
 
VAT ni VAT na ZRB ni ZRB
VAT = Value Added Tax
ZRB = Zanzibar Revenue Board
Kaupitie mfumo wa TANCIS ndipo uje uipitie tena mada yako.
Samahani lakini naona unanipotezea muda maana haujui unacho ongelea. Tanzania Revenue Authority inatoza VAT Tanzania Bara ambayo ni 18% ya thamani ya transaction. Zanzibar Revenue Board inatoza VAT Zanzibar ambayo ni 15% ya thamani ya transaction. Tanzania Custom Integrated System inairuhusu TRA kutrack mizigo inayoingia Tanzania. Inahusiana vipi na masuala ya VAT?
Kwangu mimi mjadala umeisha. Baki na unachoamini na mimi nitabaki na ninachoamini.

Amandla....
 
Naona watu wamelalamikia sana kuhusu ushuru unaotozwa na TRA kwa bidhaa zinazotoka Zanzibar. Nitatumia tofauti ya VAT Tanzania Bara na Zanzibar. Tuseme mtu ni Mkandarasi ambae biashara yake iko Bara na haipo Zanzibar. Pasipokuwa na hiyo kodi ya ziada, mtu huyu anaweza kuisajili kampuni yake Zanzibar ambako sio tu VAT iko chini lakini mpaka ada za usajili ni chini. Huyu anaweza kutenda kwa ajili ya miradi bara kwa gharama ya chini sana kwa sababu VAT kwenye vifaa atakavyoagiza kwa ajili ya mradi huo atapitishia Zanzibar. Aidha overheads zake zitakuwa chini kwa sababu gharama ya kujisajili kama mkandarasi Zanzibar ni ndogo kuliko Bara. Hii haitaleta ushindani wa haki. Ndio maana TRA wamekuwa wakali.

Amandla...
 
Hayo yote yatajadiliwa wakati wa referendum kuhusu Muungano. Kama kuna maeneo unayoona yanakukwaza katika Muungano basi utakuwa ndio wakati wa kuwashawishi watu wakuunge mkono. Kama pande zote mbili zitakubali kuwa Muungano uwepo, basi hayo masuala yatapaswa yapatiwe ufumbuzi. Kama hayana ufumbuzi ni bora tutengane na kila mmoja achukue hamsini zake.

Amandla...
Refrendum ipi manayo taka.

Kwa upande wa zanzibar vyama upinzani havitaki muungano huu na kwenye uchaguzi kihalali ndivyo vinavyo shinda.
Inaonesha kuwa wazanzibari walio wengi hawautaki muungano huu uliopo.
Mashekhe wa uamsho walitiwa ndani kwa sababu ya kuelezea watu kuhusu ubovu wa muungano huu tulokuwa nawo.

kuna mambo mengi tuu.
kuna mgawo wa 4.5% , tangu 1964 mpaka leo zanzibar haikupata share yake.
Shirika laposta haiipi zanzibar share yake
Na mengineyo mengi tuu.
 
Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo? Badala ya kusema tu wazanzibari wengi hawautaki Muungano, referendum itatoa uhakika kuwa kweli hawautaki. Vile vile kwa upande wa bara. Ingawa imani ni kuwa watu wengi wa bara wanautaka Muungano unaweza kukuta hata wao hawautaki.

Hayo ya 4.5% yatazungumzwa wakati tunafunga hesabu za Muungano. Kiasi gani Zanzibar walitakiwa wapewe na kiasi gani walitakiwa kuchangia kwenye shughuli za Muungano. Hata hilo la shirika la posta la kulipa dividends litajadiliwa ingawa sitashangaa kukuta Zanzibar inadaiwa kutokana na lilivyokuwa linapata hasara kila mara.

Referendum kwa pande zote za Muungano ndio itakata mzizi wa fitna. Na hiyo itakuwa heri kwetu sote.

Mwisho sidhani kama kilichofanya mashehe wa uamsho kilikuwa ni wao kuzungumzia mabaya ya Muungano peke yake. Ninavyojua mimi ni kuwa baadhi ya mihadhara yao ilikuwa ya kichochezi na ingejenga chuki baina ya raia wa Tanzania.

Amandla...
 
Kwa wale wanaosema kuwa mashehe wa uamsho waliwekwa ndani kwa sababu ya kuelezea ubovu wa Muungano watafute clip ya Sheikh Amir Farid akisisitiza kuwa Zanzibar haikupatikana kwa makaratasi kwa hiyo kero za Muungano hazitatatuliwa mpaka tuchinjane. Na akaelezea jinsi Quran Tukufu ilivyotoa miongozi ya namna ya kuchinja. Aidha akawaambia wazanzibari wakiona askari amemuua musilamu ( kwake yeye hamna mzanzibari mkristu) wamsome sura, wamtafute mahali wamkate shingo. Na yote hayo baada ya kuwaita viongozi wa JMT kuwa ni washenzi tu. Vile vile akawaambia wasikilizaji kuwa waliowaua wazanzibari wakati wa Mapinduzi ni watanganyika na sio wazanzibari. Sasa kama haya sio kuchochea umwagaji damu ni nini? Sisi machogo chuki ya namna hii hatuna. Ndio maana sitatoa chozi kama matokeo ya referendum yatapelekea Muungano uvunjike.

Amandla...
 
CCM hawakubali referendum za huo wanaouita muungano kwa sababu alizotoa Lukuvi

Nimewasikia watu wakisema yafuatayo kuhusu Zanzibar:
1. Zanzibar inapaswa kupata uhuru kamili kutoka kwenye utawala wa Tanganyika.
2. Tanganyika ipate Katiba yake.

Ninachojiuliza ni kuwa Zanzibar itakuwaje nchi huru kamili ndani ya Muungano? Nchi zikiungana si kila moja zinapoteza sehemu ya uhuru wake na kuuweka kwenye Muungano wao? Watu wanasema kuwa lazima Zanzibar wawe na passport zao. Sawa, lakini hii si ina maana Zanzibar iwe na balozi zake na iwe na mamlaka kamili kuhusu uhamiaji? Ni nchi gani ambayo ni Federation ambayo constituent countries kila moja ina passport yake? Sijawahi kusikia passport za Scotland, Wales, Catalonia, Quebec n.k. Tukifikia hapo maana yake hamna Muungano.

Kuna watu wanakalamika kuhusu kodi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Kuwa mtu ukinunua kitu Zanzibar,ukikileta bara unatozwa kodi tena. Si ndivyo ilivyo kati ya nchi mbili huru? Hivi wanadhani serikali huru ya Tanganyika itakubali vitu viingie kutoka Zanzibar bila kutozwa ushuru?

Mimi binafsi sioni mantik na logic ya kuwa na nchi mbili huru ndani ya Muungano. Kwa vyovyote vile patatakiwa kuwa na serikali ya Muungano ambayo itachangiwa na nchi hizo mbili. Ingawa uchumi wa Tanganyika ni mkubwa sana ukilinganisha na Zanzibar, sidhani kama serikali yake itakubali kuchangia zaidi ya mwenzao bila kupata upendeleo fulani.

Nimesikia tena kuwa wazanzibari wangependa kuwa na serikali ya mkataba kama vile ilivyo EU. Wanachosahau ni kuwa EU sio nchi. Na sisi tukiwa na mfumo kama huo ina maana hamna Muungano kama nchi. Itakuwa bora kama nchi hizo zitashirikiana katika jumuia za nchi rafiki kama EAC, SADC n.k. Kwa msingi huo Zanzibar hawatastahili upendeleo tofauti ya ule wanaopata Kenya, Uganda na Rwanda. Vile vile Tanganyika haitapata upendeleo Zanzibar. Hii hali itakuwa rahisi kwa Tanganyika maana hali ilivyo watanganyika hawapati upendeleo wowote wakiwa Zanzibar wakati wazanzibari wana haki sawa na watanganyika wakiwa Tanzania Bara.

Inazungumziwa kupotea kwa identity ya Zanzibar wakisahau kuwa watanganyika ndio hawana identity yeyote. Na maana ya Muungano wa nchi ni kuwa identity zetu zinakuwa chini ya identity ya umoja wetu. Mscot anajivunia uscotish wake lakini anajua akitoka nje ya UK , identity yake kubwa ni ya ubritish. Mzanzibari anayesema kuwa haikubali identity ya utanzania ni kuwa hautambui Muungano.

Kuna malalamiko kuhusu maamuzi kuhusu mambo ya Zanzibar kufanyika Dodoma lakini wanasahau wabunge wa Zanzibar wana uwezo wa kuzuia bajeti ya wizara isiyo ya Muungano ambayo shughuli zake zinahusu Tanzania Bara peke yake. Hamna mtu wa bara ana nafasi ya kufanya hivyo katika Bunge la Zanzibar.

Maoni yangu ni kuwa hii hatua ya Chadema ya ku "pander" kwa wazanzibari ni misguided unless kama lengo lao ni kuvunja Muungano. Kuwageuza watanganyika kuwa oppressors wakati ni wao wenyewe waliochinjana baada ya Mapinduzi na uhuru wao ulibinywa sana chini ya utawala wa Karume ni kutowatendea haki watanganyika ambao kwa kusema kweli wamekuwa wavumilivu sana.. Wengi wa wazanzibari walikimbilia bara kuepuka mkono wa chuma wa utawala ule. Na walipokelewa bara bila masharti yeyote.

Kwa mawazo yangu, kabla hata ya kuzungumzia Katiba mpya kuna haja ya kuwa na referendum kuhusu Muungano wenyewe. Na raia wa pande zote mbili waulizwe kama wanautaka au la ( watanganyika nao waulizwe ili kuondokana na dhana kuwa suala hili ni la wazanzibari peke yao). Baada ya hapo pande zote katika hii debate zieleze faida na hasara ambazo kila upande zinapata katika Muungano. Na zitakazopatikana baada ya kutengana. Kama upande mmoja utakataa basi tutengane kiungwana kama walivyofanya Czech Republic na Slovakia.

Pande zote mbili zikikubali ndio Katiba Mpya iandikwe ikiainisha ni aina gani ya Muungano tuwe nao na mgawanyo wa majukumu uwekwe wazi. Hii kuambiana kuwa tunaweza kuwa na Muungano wa nchi mbili zenye uhuru kamili ni kudanganyana. Tukiungana kila nchi itapoteza uhuru wake kwa kiasi fulani. Hatuwezi kula keki na tukabaki nayo. Ndio ukweli wenyewe.

Amandla...

Huu Si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar.

Nyerere aliivamia Zanzibar Na kumkamata Waziri Mkuu wake pamoja Na baraza la mawaziri waliochaguliwa Na wananchi Na kuwafunga katika jela Za Tanganyika kabla Huo uvamizi kupewa jina la muungano hapo April 26 ,1964
 
Back
Top Bottom