Tanganyika na Uhuru wa Zanzibar

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,940
6,854
Nimewasikia watu wakisema yafuatayo kuhusu Zanzibar:
1. Zanzibar inapaswa kupata uhuru kamili kutoka kwenye utawala wa Tanganyika.
2. Tanganyika ipate Katiba yake.

Ninachojiuliza ni kuwa Zanzibar itakuwaje nchi huru kamili ndani ya Muungano? Nchi zikiungana si kila moja zinapoteza sehemu ya uhuru wake na kuuweka kwenye Muungano wao? Watu wanasema kuwa lazima Zanzibar wawe na passport zao. Sawa, lakini hii si ina maana Zanzibar iwe na balozi zake na iwe na mamlaka kamili kuhusu uhamiaji? Ni nchi gani ambayo ni Federation ambayo constituent countries kila moja ina passport yake? Sijawahi kusikia passport za Scotland, Wales, Catalonia, Quebec n.k. Tukifikia hapo maana yake hamna Muungano.

Kuna watu wanakalamika kuhusu kodi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Kuwa mtu ukinunua kitu Zanzibar,ukikileta bara unatozwa kodi tena. Si ndivyo ilivyo kati ya nchi mbili huru? Hivi wanadhani serikali huru ya Tanganyika itakubali vitu viingie kutoka Zanzibar bila kutozwa ushuru?

Mimi binafsi sioni mantik na logic ya kuwa na nchi mbili huru ndani ya Muungano. Kwa vyovyote vile patatakiwa kuwa na serikali ya Muungano ambayo itachangiwa na nchi hizo mbili. Ingawa uchumi wa Tanganyika ni mkubwa sana ukilinganisha na Zanzibar, sidhani kama serikali yake itakubali kuchangia zaidi ya mwenzao bila kupata upendeleo fulani.

Nimesikia tena kuwa wazanzibari wangependa kuwa na serikali ya mkataba kama vile ilivyo EU. Wanachosahau ni kuwa EU sio nchi. Na sisi tukiwa na mfumo kama huo ina maana hamna Muungano kama nchi. Itakuwa bora kama nchi hizo zitashirikiana katika jumuia za nchi rafiki kama EAC, SADC n.k. Kwa msingi huo Zanzibar hawatastahili upendeleo tofauti ya ule wanaopata Kenya, Uganda na Rwanda. Vile vile Tanganyika haitapata upendeleo Zanzibar. Hii hali itakuwa rahisi kwa Tanganyika maana hali ilivyo watanganyika hawapati upendeleo wowote wakiwa Zanzibar wakati wazanzibari wana haki sawa na watanganyika wakiwa Tanzania Bara.

Inazungumziwa kupotea kwa identity ya Zanzibar wakisahau kuwa watanganyika ndio hawana identity yeyote. Na maana ya Muungano wa nchi ni kuwa identity zetu zinakuwa chini ya identity ya umoja wetu. Mscot anajivunia uscotish wake lakini anajua akitoka nje ya UK , identity yake kubwa ni ya ubritish. Mzanzibari anayesema kuwa haikubali identity ya utanzania ni kuwa hautambui Muungano.

Kuna malalamiko kuhusu maamuzi kuhusu mambo ya Zanzibar kufanyika Dodoma lakini wanasahau wabunge wa Zanzibar wana uwezo wa kuzuia bajeti ya wizara isiyo ya Muungano ambayo shughuli zake zinahusu Tanzania Bara peke yake. Hamna mtu wa bara ana nafasi ya kufanya hivyo katika Bunge la Zanzibar.

Maoni yangu ni kuwa hii hatua ya Chadema ya ku "pander" kwa wazanzibari ni misguided unless kama lengo lao ni kuvunja Muungano. Kuwageuza watanganyika kuwa oppressors wakati ni wao wenyewe waliochinjana baada ya Mapinduzi na uhuru wao ulibinywa sana chini ya utawala wa Karume ni kutowatendea haki watanganyika ambao kwa kusema kweli wamekuwa wavumilivu sana.. Wengi wa wazanzibari walikimbilia bara kuepuka mkono wa chuma wa utawala ule. Na walipokelewa bara bila masharti yeyote.

Kwa mawazo yangu, kabla hata ya kuzungumzia Katiba mpya kuna haja ya kuwa na referendum kuhusu Muungano wenyewe. Na raia wa pande zote mbili waulizwe kama wanautaka au la ( watanganyika nao waulizwe ili kuondokana na dhana kuwa suala hili ni la wazanzibari peke yao). Baada ya hapo pande zote katika hii debate zieleze faida na hasara ambazo kila upande zinapata katika Muungano. Na zitakazopatikana baada ya kutengana. Kama upande mmoja utakataa basi tutengane kiungwana kama walivyofanya Czech Republic na Slovakia.

Pande zote mbili zikikubali ndio Katiba Mpya iandikwe ikiainisha ni aina gani ya Muungano tuwe nao na mgawanyo wa majukumu uwekwe wazi. Hii kuambiana kuwa tunaweza kuwa na Muungano wa nchi mbili zenye uhuru kamili ni kudanganyana. Tukiungana kila nchi itapoteza uhuru wake kwa kiasi fulani. Hatuwezi kula keki na tukabaki nayo. Ndio ukweli wenyewe.

Amandla...
 
Naomba unijibu yafuatayo;
1. Nitajie eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
2. Nitajie mambo ya Muungano
3. Kwanini kwenye kodi/ushuru wa forodha Zanzibar mnaitoa nje ya Tanzania?
4. Bidhaa yoyote ikiingia Zanzibar hailipiwi TRA? Sasa kama inalipiwa kwanini bidhaa ile ile ikiingia Bara ambalo bado ni eneo laJamhuri ya Muungano wa Tanzania inatakiwa ilipiwe kodi wakati bado ipo kwenye eneo la Muungano?
5. Kwanini bidhaa inayoingia Dar es salaam baada ya kulipiwa kodi hata ikiingia Morogoro hailipiwi kodi kwa vile bado ipo kwenye eneo la Jamhuri ya Muungano?
 
Kuwe na referendum kwenye pande zote mbili kuhusu muungano?

Modalities za hiyo kura zitakuwaje?
 
Naomba unijibu yafuatayo;
1. Nitajie eneo la Tanzania?
2. Mambo ya Muungano
3. Kwanini kwenye kodi/ushuru wa forodha Zanzibar mnaitoa nje ya Tanzania?
Hayo yote yatajadiliwa wakati wa referendum kuhusu Muungano. Kama kuna maeneo unayoona yanakukwaza katika Muungano basi utakuwa ndio wakati wa kuwashawishi watu wakuunge mkono. Kama pande zote mbili zitakubali kuwa Muungano uwepo, basi hayo masuala yatapaswa yapatiwe ufumbuzi. Kama hayana ufumbuzi ni bora tutengane na kila mmoja achukue hamsini zake.

Civics form wani hii
 
Rudia kusoma tena nimeongezea! Pia katika huu Muungano kuna mmoja analalamika kuhusu kuubeba mzigo wa gharama za matumizi ya Muungano lakini kwanini hata upande wa pili wakionesha kutaka kujiengua wanalazimishwa?!
 
Kuwe na referendum kwenye pande zote mbili kuhusu muungano?

Modalities za hiyo kura zitakuwaje?
Kama ilivyofanyika former Czechoslovakia.a Watu wa vote simply kama wanautaka Muungano au hawautaki. Watanganyika waulizwe na wazanzibari waulizwe. Pasiwe na dhana ya kuwa hamna haja ya kuwauliza watanganyika kwa sababu bila shaka wanautaka. Na watu wafanye kampeni za wazi za pro na against Muungano. Czechoslovakia upande mmoja ulikataa na nchi yao ikawa history.
Tuulizwe tuu maana maneno yamekuwa mengi

Amandla...
 
Rudia kusoma tena nimeongezea! Pia katika huu Muungano kuna mmoja analalamika kuhusu kuubeba mzigo wa gharama za matumizi ya Muungano lakini kwanini hata upande wa pili wakionesha kutaka kujiengua wanalazimishwa?!
Ndio maana nimesema pawe na referendum. Upande utakaotaka kujiengua utasababisha Muungano uvunjike. Mzizi wa fitna kuwa kuna upande mmoja ni king'ang'anizi utakatwa.

Amandla...
 
Kama ilivyofanyika former Czechoslovakia.a Watu wa vote simply kama wanautaka Muungano au hawautaki. Watanganyika waulizwe na wazanzibari waulizwe. Pasiwe na dhana ya kuwa hamna haja ya kuwauliza watanganyika kwa sababu bila shaka wanautaka. Na watu wafanye kampeni za wazi za pro na against Muungano. Czechoslovakia upande mmoja ulikataa na nchi yao ikawa history.
Tuulizwe tuu maana maneno yamekuwa mengi

Amandla...
Upande mmoja ukiukataa muungano na upande mwingine ukaukubali, hapo inakuwaje?
 
Kila president anayeingia anajitahidi/hataki muungano ufie mikononi mwake
Tujifunze kwa Biden. Kila Rais wa Marekani hakutaka kuonekana kuwa vita ya Afghanistan imemshinda. Biden akasema mimi najitoa.
Hivyo hivyo tunahitaji Rais atakaesema ngoja niondokane na hili tatizo. Muungano ukivunjika tutasikitika na maisha yataendelea. Na kama tunaona Muungano una faida basi ni wajibu wetu kuwashawishi watu wakubaliane nasi badala ya kukataa kukabaliana kwa hoja na wale ambao hawautaki.

Amandla...
 
Upande mmoja ukiukataa muungano na upande mwingine ukaukubali, hapo inakuwaje?
Muungano finito. Inatakiwa pande zote mbili ziukubali. Ndivyo ilivyokuwa Czechoslovakia. Upande mmoja ulikataa, mwingine ulikubali wakagawana nchi. Kuwauliza wazanzibari peke yao kutaacha uwezekano wa hapo mbele kutokea watanganyika ambao watasema walilazimishwa tu.

Amandla...
 
Rasim ya katiba ya mzee Warioba imeeleza kila kitu kuhusu muungano kwa kukusanya maoni ya wananchi wa pande zote mbili bara na visiwani, hatuna haja ya kukusanya maoni mengine, katiba mpya ndiyo suluhisho ya mambo yote, Viva Mbowe Viva Mbowe
 
Muungano finito. Inatakiwa pande zote mbili ziukubali. Ndivyo ilivyokuwa Czechoslovakia. Upande mmoja ulikataa, mwingine ulikubali wakagawana nchi. Kuwauliza wazanzibari peke yao kutaacha uwezekano wa hapo mbele kutokea watanganyika ambao watasema walilazimishwa tu.

Amandla...
Lakini upande ambao utaukubali muungano, endapo muungano utavunjwa kisa upande mmoja umeamua kuukataa, utakuwa umelazimishwa kuuvunja muungano ambao bado unataka uendelee.
 
Rudia kusoma tena nimeongezea! Pia katika huu Muungano kuna mmoja analalamika kuhusu kuubeba mzigo wa gharama za matumizi ya Muungano lakini kwanini hata upande wa pili wakionesha kutaka kujiengua wanalazimishwa?!
Unakimbilia details. Kuna ushuru ambao Zanzibar waliushusha na hivyo kufanya bidhaa zao kuwa na bei ya chini kiasi cha kufanya wakina mama waende wakanunue huko na kuzileta Dar. Wenye viwanda upande wa pili wakalalamika na serikali ya JMT ikaona inapoteza kiasi fulani cha mapato hivyo wakasema ile tofauti ya ushuru ilipwe vitu vinapoingia Tanganyika kutoka Zanzibar.
Kulinganisha Morogoro na Zanzibar ni kusemq kuwa Zanzibar kuwa ni mkoa wa JMT. Hiyo sio kweli.

Amandla...
 
Lakini upande ambao utaukubali muungano, endapo muungano utavunjwa kisa upande mmoja umeamua kuukataa, utakuwa umelazimishwa kuuvunja muungano ambao bado unataka uendelee.
Huwezi kulazimisha ndoa na mtu asiyekutaka kwa sababu tu unampenda. Kwa sababu hii itawekwa wazi basi itabidi akubali tu.

Amandla...
 
Unakimbilia details. Kuna ushuru ambao Zanzibar waliushusha na hivyo kufanya bidhaa zao kuwa na bei ya chini kiasi cha kufanya wakina mama waende wakanunue huko na kuzileta Dar. Wenye viwanda upande wa pili wakalalamika na serikali ya JMT ikaona inapoteza kiasi fulani cha mapato hivyo wakasema ile tofauti ya ushuru ilipwe vitu vinapoingia Tanganyika kutoka Zanzibar.
Kulinganisha Morogoro na Zanzibar ni kusemq kuwa Zanzibar kuwa ni mkoa wa JMT. Hiyo sio kweli.

Amandla...
Hiki unachoongea sidhani kama kina ukweli sana, miaka ya 70,80 hadi 90 Zanzibar ilikuwa ni eneo ambalo bidhaa nyingi zilikuwa zinapatikana, akina mama kutoka bara walikuwa ndio wanatoka bara na kwenda kununua Zanzibar lakini kwasasa hali ni tofauti ambapo akina mama kutoka Zanzibar ndio wanaotoka Zanzibar na kwenda kununua bara hususan Kariakoo. Kinachonunuliwa Zanzibar sana sana ni vitu used labda na marashi pekee! Je unaliongeleaje hilo?
 
Na bei ilikuwa chini kwa sababu ushuru ulikuwa chini sana Zanzibar kuliko Bara. TRA walipoanza kudai ile tofauti ya ushuru ndio biashara ya Darajani ikaanguka. Wewe haujiulizi kuwa itakuwaje gari linunuliwe Dubai lakini likipitia bandari ya Zanzibar liwe na bei ya chini kuliko likipitia Dar? Lakini hili jambo lilizungumzwa kati ya nchi hizo mbili zikafikia huo muafaka. Ila kama bado unaona ni dhulma basi labda Muungano ukivunjike hali itakuwa nzuri zaidi na biashara ya Darajani itashamiri tena.

Kwanini TRA wasiwe na mfumo mmoja tu wa ukusanyaji kodi ndani ya Tanzania nzima na badala yake ukiingiza bidhaa Zanzibar wanakata lakini bidhaa hiyo hiyo ukisafirisha kuiingiza bara wanakata tena ikiwa eneo lote ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Au labda unadhani shida iko wapi ikiwa TRA ile ile iliyopo Zanzibar ndiyo iliyopo Bara?
Siongelei vitu kama magari bali niko kwenye bidhaa ndogo ndogo.
Sidhani kama ulishawahi kutafiti hilo lakini nijuavyo ndani ya Muungano Zanzibar si nchi ila nje ya Muungano Zanzibar ni nchi na hiki ndicho kinachotumika kuwachapa mijeledi wafanyabiashara wadogo wanaoingiza bidhaa bara kwa vile wametoa Zanzibar hivyo inachukuliwa ni nje ya Muungano.
 
Zanzibar hawatakubali kwa sababu pakiwa na mfumo mmoja wa ushuru bei za bidhaa Zanzibar zitapandana na hivyo kuwaumiza wazanzibari.
Sijakuelewa. Zanzibar inakuwa nje ya Muungano ki vipi? Utasemaje sio nchi wakati ina Rais wake, bunge lake, serikali yake, mfumo wake wa kimahakama? Na akienda Rais wa JMT anakuwa mgeni wa Rais wa Zanzibar? Aidha, Zanzibar inaweza kutunga sheria ambazo zinamnyima au kumpunguzia haki mtu wa bara katika maeneo ya umiliki wa ardhi, ushiriki kwenye siasa, ajira n.k.? Kuna wakati machogo walikuwa wanalazimika kupata kibali maalum kabla ya kuoa binti wa kizanzibari. Zanzibar ni nchi bwana.

Amandla...
 
Back
Top Bottom