Kamawewe
JF-Expert Member
- Jan 16, 2013
- 531
- 505
Mkuu hiyo ya kulala na mbuzi umenichekesha mpaka watu wameshangaa, nikakumbuka watu wa Tanga hutumia neno "Mibwasha" Kuelezea watu wa namna hii kwa kukosa ustaarabu. Kuna rafiki yangu alihamishiwa Musoma kikazi idara ya polisi basi aliacha kazi kwa kuwaogopa watanzania wenzetu wa huko.Hujatembea kaka. Nenda kigima, mwanza, shinyanga, mara ukaone watu wanavyolala na mbuzi chumba kimoja. Wanasema nyumba za makuti, si afadhali wao wanalala kwenye tembe za nyasi hakuna kitu.
Watu wanataka wasikie taarifa za habari majambazi wameteka maduka wameua watu 8, wakazi wa mtaa fulani wamekatana mapanga ma mji haulaliki, mabomu ya.machozi daily, hayo kwao ndio maendeleo.
Ila ukikaa barazani huja endelea. Sasa huko kwengine nyumba mnajenga kama mahema ya UNHCR hiyo baraza yakukaa itatoka wapi jamani? Huwezi kuona watu wamekaa barazani manake risasi njenje saa kumi na mbili watu wamelela.
Njooni tanga 24/7 hakuna atakaye kuuliza wala kukukaba. Mji upo kimyaaaaa, malevi yamezoea kupiga mikelele wanaona tabu sana. Rudini kwenu lawama zenu tumezichoka.