Tanga; Mkoa uliokufa

Hujatembea kaka. Nenda kigima, mwanza, shinyanga, mara ukaone watu wanavyolala na mbuzi chumba kimoja. Wanasema nyumba za makuti, si afadhali wao wanalala kwenye tembe za nyasi hakuna kitu.

Watu wanataka wasikie taarifa za habari majambazi wameteka maduka wameua watu 8, wakazi wa mtaa fulani wamekatana mapanga ma mji haulaliki, mabomu ya.machozi daily, hayo kwao ndio maendeleo.

Ila ukikaa barazani huja endelea. Sasa huko kwengine nyumba mnajenga kama mahema ya UNHCR hiyo baraza yakukaa itatoka wapi jamani? Huwezi kuona watu wamekaa barazani manake risasi njenje saa kumi na mbili watu wamelela.

Njooni tanga 24/7 hakuna atakaye kuuliza wala kukukaba. Mji upo kimyaaaaa, malevi yamezoea kupiga mikelele wanaona tabu sana. Rudini kwenu lawama zenu tumezichoka.
Mkuu hiyo ya kulala na mbuzi umenichekesha mpaka watu wameshangaa, nikakumbuka watu wa Tanga hutumia neno "Mibwasha" Kuelezea watu wa namna hii kwa kukosa ustaarabu. Kuna rafiki yangu alihamishiwa Musoma kikazi idara ya polisi basi aliacha kazi kwa kuwaogopa watanzania wenzetu wa huko.
 
ila mikoa/ maeneo mengi yenye waislamu ni wavivu na hakuna maendeleo (mtanisamehe ila huo ndo ukweli) kila mtu atafute case study yake. dodoma cjui wanamatatizo gani
Umesikia Omba Omba wa kidogo? Au umesikia mabeki tatu wa kidogo.... Maeneo ya waislam hayana maendeleo lakuni nashangaa matajiri wengi ni waislam... Hii imekaaje?
 
Hivi ilikuwaje Tanga ikapewa hadhi ya Jiji..!!?
Mkuu Tanga ilitakiwa kuwa Jiji kabla ya majiji mengine
Katika historia Tanga ilipewa hadhi ya 'Manispaa' mwaka 1966 ikiwa ndiyo pekee baada ya Jiji Dar

Kama kasi ingelikuwa nzuri, Tanga ilitakiwa iwe Jiji miaka ya 1980.
Kitendo cha kuwa Jiji katika miaka ya karibuni ni kuchelewa achilia mbali kuuliza ilikuwaje

Kwa Taarifa, Tanga ndio mji wa kwanza kuwa na kitu kinaitwa gazeti mwaka 1919 kama sikosei
Wakati huo miji kama Arusha ilikuwa vituo tu vya kupita kama vimiji vingine tunavyoviona leo

Kudorora kwa Tanga kumechangiwa sababu kadhaa

1. Kiuchumi:
Tanga ilikuwa kiunganishi kizuri na miji kama Mombasa.
Baada ya kufunga mpaka na Kenya shughuli nyingi ziliathirika mwingiliano na biashara

2. Kudorora kwa uchumi wa nchi kuliathiri sana viwanda na bandari

3. Kuanguka kwa zao la mkonge lililokuwa tegemeo la uchumi nako kulichangia sana

Sababu ya Pili
Kijamii, Tanga na miji ya jirani kama Muheza ina wasomi wengi.
Utamaduni wa wasomi kutorudi makwao na kuwekeza umedumuza sana maendeleo

Katika mkoa masikini kwa rasilimali hasa ardhi, Kilimanjaro ni namba moja.
Hata hivyo umasikini hauonekani kwasababu wananchi hurudi na kuwekeza makwao.

Sababu ya Tatu
Wakazi wa Tanga wanategemea sana shughuli laini katika kutafuta kipato.

Tanga ina ardhi yenye rutuba kwa mazao ya aina nyingi.
Ukiona kilimo kinachoendelea sasa ni kutokana na wahamiaji hasa kutoka KLM

Hili linatokana na mazoea ya kuwa na uchumi wa huduma zaidi ya uzalishaji

Sehemu kubwa ya matatizo inachangiwa na waliokuwa na uwezo wa kifedha na kielim kuondoka na kutotaka kurudi kuwekeza nyumbani,kwa hisia za utamaduni wa mambo ya kishirikina

JokaKuu
 
Mleta mada karibu upunguze stress
e74a388409bd3059972992e702372acf.jpg
Tsh 300 tu,,,Tanga hapachoshi kabisa.
 
Kwa mnaoidharau Tanga kwa sababu yoyote ni mda tu mtakuja kukubali kwamba mnaongea theory,,,mkoa unarudi Kwenye track kwa kasi ya ajabu.Mkoa una plan,,umepangwa vizuri,,hewa nzuri na watu wenye hekma.Kuna sehemu za public kupumzika kwenye kivuli,,mkoa mzuri kabisa.
 
Baada uhuru tukaua nchi kwa udini..tukaiua Tanga pangani mtwara lindi bagamoyo ambazo tayari zilishapiga hatua.
Na kuamua mjii mkuu uhamie dodoma kwa sababu hizo...
Afadhali wakoloni hawakuangalia udini kwenye umuhimu wa miji na maendeleo yake....
 
Mtoa mada nakubishiia. Tan ga Ni mji mzuri na maendeleo yapo ,,Tanga ya zaman si sawa na ya Leo ,,we mwenyew tizama usiongee kwa kukejeri ....Tanga ya Leo maendeleo inayo ....mwendo Ni huu na tutafika
 
Tanga raha! Karibuni..acheni sanifu na mikoa ya watu
Huyu ni wa kumpuuza,na hiyo nairobi anayoizungumzia labda ya kibosho,tanga inakua kwa kasi sana,majumba ya kifahali,viwanda vipya,nk vinaongezeka kila leo,huyu mwanamke alieleta huu uzi atakua yuko
 
Back
Top Bottom