Je, Mkoa wa Tanga ni Jamhuri inayojitegemea?

DolphinT

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
1,308
1,828
Naomba kuuliza suala hili kwa Afande IGP, RPC wa Tanga na DTO wa Tanga je Mkoa wa Tanga ni Jamhuri inayojitegemea?

Katika kujitafutia maendeleo watanzania wanafanya kazi usiku na Mchana Ili kuweza kupambana na ugumu wa maisha na kupata mahitaji Yao ya kila siku.

Ni dhahiri kwamba katika harakati hizo watanzania wanatakiwa kuhakikishiwa ulinzi na Usalama hii ikiwa ni kazi na jukumu la jeshi la polisi na vyombo vingine vya Usalama.

Msingi wa hoja yangu ni kwamba ajali za barabarani hazichagui muda Sahihi wa kutokea, huwa zinatokea wakati wowote iwe usiku au Mchana Asubuhi au jioni.

Kwa kipindi Fulani palitokea ajali kadhaa wakati wa usiku katika mkoa wa Tanga hasa wilaya ya Korogwe ikihusisha magari yanayosafiri usiku hasa Coaster za zinazobeba abiria wengi wao wakiwa wafanyabiashara wanaotoka mkoa wa Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha na wengine kuelekea nchi Jirani ya Kenya.

Kundi kingine ni kundi la watu wanaosafirisha wapendwa wao walioaga Dunia kwenda kuwapumzisha katika mikoa niliyoitaja.

Kwa bahati mbaya sana baada ya kutokea ajali hizo jeshi la polisi mkoani tanga lilipiga marufuku magari hayo kupita mkoa huo isipokua kabla ya saa sita usiku.

Hali kadhalika Mkoani dar es salaam katika vituo bubu vya kupakia abiria hao Askari polisi wamegeuza magari hayo kuwa mtaji kama njia ya kuzuia watu kusafiri usiku;

Wakati zuio Hilo likiendelea mikoa mingine mathalani nyanda za Juu kusini watu wanasafiri kama kawaida bila bugudha yote

Sambamba na Hilo wanaosafirisha misiba hawajakumbwa na zuio Hilo huko Mkoani Tanga.

Sasa swali langu je Tanga ni Jamhuri inayojitegemea hivyo inaweza kujiamulia mambo yake ambayo kwa namna nyingine yanaleta athari kwa wananchi?

Way forward:
Kwakua Jeshi la polisi Lina jukumu la kuhakikisha Usalama wa raia na Mali zao, ni vyema kama wanavyofanya nyakati za usiku kuona namna Gani wanavyoweza kusimamia sheria na Usalama wa magari yanayotembea usiku!

Kwani kuzuia coaster na kuacha malori magari ya misiba na gari binafsi kutembea usiku ni uvivu wa kufikiri kwani vyombo hivyo havijiendeshi Bali huendeshwa na watu.

Kitendo Cha kuzuia magari kupita mkoa wa Tanga kabla ya saa sita za usiku unafanya madereva waendeshe magari kwa mwendo Kasi ZAIDI kuliko kawaida Ili kuwahi barrier Msata au Segera! Hii inawaweka abiria hatarini kuliko ambavyo wasingezuia.

Serikali ifanye utaratibu kwa kupitia mammlaka husika, itunge sheria na Ione utaratibu wa mabasi kutembea usiku kucha na Huku Jeshi la polisi likitakiwa kusimamia utaratibu huo. Na sio polisi kulala usiku wakati walichagua kazi ya ulinzi!

Hata wale wenzangu na Mimi wanaotoroka kazini Ijumaa jioni waendelee kunufaika kwa kurudi jumapili.

Wasalam.
 
Nenda ukaishi huko nyanda za juu uendelee kusafiri usiku.
Timechoka ajali za kizembe.
 
Kuna maamuzi yakishapitishwa huwa na hasi na chanya kwenye matokeo yake
Nakubaliana na ww mtani, lakini pia negatives yafaa ziepukwe zaidi sababu kila maamuzi yanalenga kumpa nafuu Mwananchi katoka shughuli zake za kila siku anapojitafutia riziki! Sasa kwanini maamuzi ya kuzuia jambo Fulani yafanyika katoka sehemu Moja TU ya nchi huku sehemu nyingine ya nchi jambo Hilo Hilo liendelee kufanyika na kwa utaratiibu ule ule? Hapa ndio nikauliza je? Mammlaka hiyo hiyo yaweza kukataza jambo Hilo Hilo katoka nchi hiyo hiyo na kuruhusu jambo Hilo Hilo katoka nchi hiyo hiyo?
 
Asante Madam speaker kwa kuliona Hilo ingawa Uzi wangu ulikumbana na kejeli!
 
Back
Top Bottom