Tanga; Mkoa uliokufa

Tanga; Mkoa uliokufa

Umekaa wiki mbili tena umeishia huko uswahili a.k.a barabara za namba, halafu unakuja na jibu lako kama hilo? Acha kuwadanganya watu.

Mji umekufa lakini watu wanaishi na idadi yao inaongezeka kila siku.

Usafiri umeongezeka, mabasi yanaongeza ruti na ndege zimeongezeka pamoja na meli halafu unasema mji unakufa.

Viwanda vipya vya saruji (Sungura na Rhino) vimefunguliwa huku wachina wakitarajia kujenga kiwanda kikubwa cha saruji kuliko vyote ukanda wa Afrika Mashariki halafu unasema mji umekufa?

Site mpya za Mwahako, Neema, Kange, Kasera, Pongwe mpaka Machui umezitembelea? Kama huko ni mbali shuka kidogo na Karume road ukianzia Duga mwembeni mpaka Tanga Beach Resort uone makao mapya.

Nyumba chache za makuti zilizobakia hapo utakuta wengi wa wamiliki walishakufa na walioachiwa urithi wana migogoro nazo. Hata hvyo ujenzi wa makuti ni utamaduni lakini sio kiashiria cha umaskini.

Watu kukaa barazani kwenye mikeka wakicheza bao na kunywa kahawa sio kama hawana kazi, hapo wamebarizi baada ya kazi au wakisubiri waingie kazini jioni au usiku kwa wale wavuvi.

Ukumbuke wengi wa wanamji ni waislamu hivyo huwezi kuwakuta baa au vilabuni wao hukaa vibarazani mwao.

Fanya utafiti wako kisomi kisha uje tena.
Dah! Imemaliza eti masomoni nairobj mika 18. Hiyo tayari dosari.
 
Nimekujibu koz at least you deserve it.... Mkuu imagine you have left a place after 18 years unarudi unakuta nyumba za makuti in the middle of the town

Unakuta nyumba zimekatiwa umeme barabara 13 na14 kweli miaka hii watu wanashindwa kuendelea.....
Mkuu kila mji Tz kuna sehemu hasa za wenyeji hazijaendelea na kuna sehemu za makazi mapya zimeendelezwa. Uliza hapo Tanga ni sehemu gani zimeendelezwa na kuwa na majengo ya kuvutia. Nimeishi zaidi ya mikoa saba tofauti Tz nimegundua Mara nyingi wenyeji wa mji wanadharaulika au kushutumiwa kwa tabia za hovyo kwa sababu ukifika sehemu lazima utajua mapungufu ya wenyeji.
 
Mleta mada karibu upunguze stress
e74a388409bd3059972992e702372acf.jpg
 
Jamaa wanadai kwa nini MAGU ( DEREVA WA LORI) anataka kujenga vi-wonder Dodoma wakati alipokuja Tangamano aliwapa ahadi ya kufufua viwanda vifuatavyo

Kiwanda cha sabuni ya Mbuni
Matunda toka LUSHOTO
Mashamba ya Mkonge
Nk.......?
Na tangu awape ahadi hiyo hataki kukanyaga tena maana atadaiwa chenchi ya barabara ya tanga pangani!
 
Bwana kinawari kama ni kusoma huko nairobi ada yako imetoka hapa hapa tanga au umeamua kuua tanga mkajenge moshi maana naona mmejiwekeza vya kutosha!
 
Nmezaliwa tanga nmesomea huko na mpaka leo wazaz wng wako tanga lkn kiukweli ni kwamba ukiwa tanga huwez kuona kama ule mkoa umedoda mpaka utoke uende sehem zilizochangamka then ukirud tanga ndio utaona namna gan ule mkoa ulivyodorora...
.
Hata wanaotetea hawaon kama tanga ipo nyuma kimaendeleo labda mpaka nawao watoke kidogo wakajichanganye sehem nyngne ndio wataelewa namna ambavyo tanga yetu inaretarded growth
Hujatembea kaka. Nenda kigima, mwanza, shinyanga, mara ukaone watu wanavyolala na mbuzi chumba kimoja. Wanasema nyumba za makuti, si afadhali wao wanalala kwenye tembe za nyasi hakuna kitu.

Watu wanataka wasikie taarifa za habari majambazi wameteka maduka wameua watu 8, wakazi wa mtaa fulani wamekatana mapanga ma mji haulaliki, mabomu ya.machozi daily, hayo kwao ndio maendeleo.

Ila ukikaa barazani huja endelea. Sasa huko kwengine nyumba mnajenga kama mahema ya UNHCR hiyo baraza yakukaa itatoka wapi jamani? Huwezi kuona watu wamekaa barazani manake risasi njenje saa kumi na mbili watu wamelela.

Njooni tanga 24/7 hakuna atakaye kuuliza wala kukukaba. Mji upo kimyaaaaa, malevi yamezoea kupiga mikelele wanaona tabu sana. Rudini kwenu lawama zenu tumezichoka.
 
Hawa Wanaropoka ropoka.... Sasa hebu tumuulize mtoa mada ameona Tanga hapo... Wacheni mambo ya kibwege asubuhi asubuhi.
Hizo data mbichiiiiiii hawazioni hapo kabisa. Wamefunga tinted. Nakuho kwao kila mwaka mbolea ya ruzuku na njaa kama kawa kama dawa.
 
Tanga tumekaa sana

Watu wa tanga akili zao zote zinawaza dar na Arusha Pmj na kuwa Kuna ardhi nzuri ya kilimo

Tanga vijana wanaishi km wazee wanashinda kwenye kahawa
Mabint wakitanga wanavunga ni waarabu hawatak kujishughulisha,

Ila raha ya Tanga, Kuna samak I watamu sana

Na Mabint hawajui kukataa
Utalimaje wakati mbolea za ruzuku zinapelekwa bara kila siku? Ushawahi kusikia tanga wamepewa mbolea za ruzuku? Sasa walime kwa msaada wa serikali gani wakati serikali wanasaidia watu wa kwao wasife na njaa?

Na bado tanga haiyumbi. Chakula chakutosha na mengine mengi
 
Kange wamejenga watu wa kuja, mswahili wa Tanga kuhama kule uswahilin haitatokea yeye yupo tayar akae kwenye makut
Sasa kange akafuate nini? Mtu amejenga nyumba yake ya makuti fasi, umeme na maji ndani. Hakuna bugdha wala jekejeke, unataka aende kange akafanyeje? Hao wakuja ndio kiziri njia ya kwenda kwao hao unaowaita waswahili washafika hawana haja kwenda kukaa karibu na highway.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom