Deshbhakt
JF-Expert Member
- Jan 22, 2008
- 375
- 189
Kwa niaba ya rafiki wangu huko Tanga na-share hii uzi
Barua wazi kwa mkuu wa mkoa tanga.
Mheshimiwa mkuu wa mkoa Tanga,
Ni kwa masikitiko makubwa tunakueletea malalamiko dhidhi ya club ya Ben Bistro hapa wilayani Tanga, kati ya mtaa wa Ekcenforde na ring - Guinea Street
Club hii iliyoanzishwa miaka miwili ilioypita inaendelea kututesa kwa kuleta mazingira ya mateso mengi sana kwa sisi tunaoishi kwenye maeneo haya! Tabia za kihuni kwa kucheza muziki hadi usiku wa manane pamoja na wateja wao kuhudumiwa pombe kwenye magari zao barabarani na kukutwa wamesinzia hadi asubuhi pamoja na kutoa huduma za shisha, wadada wanauza mwili zao pia wapo na kufanya mambo zao kwenye magari n.K asubuhi hukosi kuona machupa za pombe barabarani au kwenye mataro na ukuta zinanuka na mkojo.
Huo mtaa unatumika sana na wanafunzi wanaopita kuelekea mashule mengi zilizo jirani na huwa wanashuhudia haya mazingira kila siku. Pia kuna kanisa na misikiti mawili na waumini wengi nao wanashuhudia haya matatizo.
Siku ya jumamosi tarehe saba mwezi huu wamezuia mabarara nne za mitaa na kufunga jukwaa. Jumapili kuanzia saa 11 jioni wameanza tamasha ya bendi iliyoendelea hadi 12 alfajiri.
Mheshimiwa, sisi tulishindwa kupumzika kabisa maana kelele ilikuwa mkubwa mno na hadi vitu vya ndani, ufa n.K. Za manyumba zetu zilikuwa zinatetemeka.
Mara nyingi asubuhi waumini waonaoelekea msikitini wamekuta watu wameelewa na kulala juu ya meza, kwenye magari na chupa za pombe zimetupwa barabarani.
Mwenyekiti wa mtaa naye hataki kutusaidia na insemekana biashara zake ni kukodisha vifaa wa bendi na vilitumika siku hiyo. Mwenye hiyo biashara aitwaye beny nae inasemekana kuwa anafahamia na 'viongozi wa juu' na hakuna atakaemsumbua?
Je hii ni haki? Mtaa wetu miaka nenda nyuma ilikuwa na utulivu na heshima wa hali ya juu ila leo hii tunateseka sana.
Tafadhali angalia video hizi.
Mheshimiwa, tunakuomba utusaidie.