Tanesco yazidi kubanwa; Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu; lina Kesi 200 zisizoisha

Jasusi, Ndahani, Ame, Maundumula,



..hivi mnaichukuliaje hii kauli ya Prof.Muhongo kuhusu wizara ya fedha.

..je, waziri wa nishati ya madini anayo mamlaka ya kuzuia fedha zinazotokana na mapato ya gesi na mafuta zisiwasilishwe HAZINA??

..nina wasiwasi Prof.Muhongo anaweza kuingia ktk malumbano na Waziri wa Fedha.

NB:

..hapo bado Dr.Magufuli hajaanza kushinikiza kubomoa jengo la makao makuu ya Tanesco!!



Waliomzunguka ndio watamsumbua zaidi kuliko anavyodhani ingawa inawezekana ana nia ya kuonyesha yeye ni tofauti.
 
Jasusi, Ndahani, Ame, Maundumula,



..hivi mnaichukuliaje hii kauli ya Prof.Muhongo kuhusu wizara ya fedha.

..je, waziri wa nishati ya madini anayo mamlaka ya kuzuia fedha zinazotokana na mapato ya gesi na mafuta zisiwasilishwe HAZINA??

..nina wasiwasi Prof.Muhongo anaweza kuingia ktk malumbano na Waziri wa Fedha.

NB:

..hapo bado Dr.Magufuli hajaanza kushinikiza kubomoa jengo la makao makuu ya Tanesco!!


JokaKuu,'
Kwa kweli hapa sina jibu. Lakini nakubaliana na lengo lake kuwa kuna matobo mengi wizara ya fedha. Sasa sijui kama wataanzisha mfuko maalumu wa fedha za gesi, jambo ambalo IMF na World Bank walishinikiza Chad ifanye baada ya kugtundulika gesi huko.
 
Kiona, kajembe, Ndahani Jasusi, MR.PRESIDENT,

..kwa sisi tuliokula chumvi nyingi kidogo tunapendelea zaidi kuona matokeo, na siyo AHADI au NIA NJEMA.

..Mwaka 1994 nikiwa naive kama baadhi yenu nilivutiwa sana na hotuba ya bajeti ya Basil Mramba. Nilivutiwa kwasababu alikwenda bungeni akafoka sana kwamba Tanzania tunafuja fedha zetu kwa kuagiza vitu visivyo na maana. Mramba alikwenda mbali mpaka kutoa nyoka wa plastic ktk mkoba wake na huku akiwanyooshea wabunge kwamba badala ya ku-import vitu vya maana like machinery, tuna-import toys!!

..Sote tu mashahidi ya jinsi Mramba alivyobadilika na kuwa kitu kingine kabisa. Ndiyo maana nawaambia subirini kwanza mpaka muone kama atabadili hiyo mikataba, then we can celebrate.


Mkubwa umeongea point kabisa ila tatizo unafananisha moshi na upepo. Mramba aliongea na kuwajibika kama mwanasiasa. Waziri wetu bwana Mhongo yeye si mwanasiasa bali mwajiriwa. hawajibiki kwa mpiga kura yeyote kwa hivyo yeye yuko pale kuchapa kazi tu. Mramba alikwenda mrama Mhongo ni mhogo mchungu wala rushwa hawautafuni.
 
Mkubwa umeongea point kabisa ila tatizo unafananisha moshi na upepo. Mramba aliongea na kuwajibika kama mwanasiasa. Waziri wetu bwana Mhongo yeye si mwanasiasa bali mwajiriwa. hawajibiki kwa mpiga kura yeyote kwa hivyo yeye yuko pale kuchapa kazi tu. Mramba alikwenda mrama Mhongo ni mhogo mchungu wala rushwa hawautafuni.
Kiona,

..kwa taarifa yako, mawaziri wote ni wanasiasa.

..wataalamu ni makatibu wakuu na watendaji wengine wizarani.

..Prof.Muhongo ni mbunge wa kuteuliwa na Raisi, anatumikia serikali ya CCM, na anawajibika kwa wapiga kura wote wa Tanzania.

..Mawaziri wote, ikiwemo Prof.Muhongo, wanawajibika kwa wapiga kura wa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:


JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:22 NA ARODIA METER DAR ES SALAAM

*Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu
*Asema shirika hilo hivi sasa lina kesi 200 zisizoisha.
*Aitaka TPDC kupitia upya mikataba 26 ya gesi
*Akataa fedha ya mafuta na gesi kuingizwa Hazina
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kesi mbalimbali zinazokabili mashirika yaliyo chini ya wizara yake likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni kichaka cha ‘ulaji’ wa watu.

Profesa Muhongo pia ameonya kuwa mtumishi atakayeingia mkataba mbovu na kampuni yoyote ya kigeni au ya ndani atafukuzwa kazi na kushtakiwa.

Aliyasema hayo wakati wa akizindua bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency Dar es Salaam jana.

Fedha nyingi katika Tanzania zinapotea kwa njia ya mikataba mibovu na kesi nyingi zisizoisha mahakamani.

Alisema kwa mfano Tanesco peke yake kuna kesi zaidi ya 200 ambazo nyingi ni miradi ya watu wachache.

Waziri alisema baadhi ya watumishi wanashirikiana na makampuni ya sheria kuyaibia mashirika kwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka.

“Fedha nyingi katika nchi yetu zinapotea kwa kesi zisizoisha na mikataba mibovu… kesi hizo zinaifikisha bili zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka na kusababisha taifa kubaki katika ufukara.

“Nimekwisha kusema ni marufuku kampuni moja kurundikiwa kesi nyingine na kampuni itakayopewa kazi hiyo lazima ishinde kesi nane kati ya 10, tofauti na hayo inyang’anywe mara moja… na tabia hii ife,” alisema Profesa Muhongo.

Kuhusu Bodi ya TPDC

Akizindua boda ya TPDC, Profesa Muhongo aliwasimamisha wajumbe wapya wa bodi kila mmoja kwa dakika mbili akiwataka waeleze uzoefu wako na jinsi watakavyosaidia kuliinua shirika hilo.

Baada ya kujielekeza waziri aliwakabidhi wajumbe hao mkoba wenye mikataba 26 ya TPDC ili waipitie na kutoa mapendekezo yao ndani ya miezi mitatu.

Alisema Novemba 30 mwaka huu atakaa pamoja nao kujadili mkataba moja baada ya mwingine.

“Hapa tuna mikataba 26 baadhi yake ni mibovu, kazi yenu ni kuipitia upya ni lazima kila mkataba ufanyiwe auditing (ukaguzi).

“Nimeambiwa kisima kimoja kinalindwa kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 100 mpaka 150, kwa hiyo lazima bodi ipitie kwa makini suala hili ikiwezekana ulinzi huo ufanywe na jeshi letu ili fedha zibaki nchini.

“Tusije tukafanya tena mkosa kama tulivyofanya kwenye sekta ya Madani. Kampuni nyingi ni wajanja msiwaamini hata kidogo, haiwezekani mtu anachimba kwa miaka 10 bila kulipa kwa kisingizio cha fedha alizotumia.

Azuia mikataba mipya

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo amepiga marufuku mikataba mipya hadi ya sasa itakapopitiwa upya na kujiridhisha kwamba ipo kwa manufaa ya Watanzania.

“Kuanzia sasa sitasaini mkataba wowote hadi hii iliyopo tutakapojiridhisha kuwa iko salama kwa manufaa ya watanzania.” Alisema.

Fedha za gesi na mafuta kutoingizwa Hazina

Profesa Muhongo vilevile alisema fedha zote zitakazotokana na gesi na mafuta hazitaingizwa Hazina.

Alisema hatua hiyo itaepusha fedha hizo kuchangwa na nyingine na baadaye kuchakachuliwa na hivyo kushindwa kuonekana zimefanya jambo gani.

Waziri alisema fedha hizo zinapaswa kuonekana zimefanya kitu ambacho Watanzania watajivunia kuwapo kwa raslimali hiyo.

“Fedha za gesi na mafuta hazitakwenda Hazina kwa sababu huko kuna matobo mengi. Sitaki zikachanganywe na nyingine ambazo zikienda kwenye halmashauri mwishowe tutasikia dawati moja limenunuliwa kwa Sh milioni 10,” alisema.

Azungumzia malipo ya huduma (capacity charge)

Waziri Muhongo pia amepiga marufuku mashirika yote yaliyo chini ya Tanesco kuingia mkataba na kampuni unaotaka malipo ya huma (capacity charge).

Alisema malipo hayo ni bandia na wizi wa wazi, na mtumishi yeyote atakayeingia mkataba wa aina hiyo atafukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa.

“Ni marufuku kwa kampuni inayotaka kufanya biashara na sisi kuweka kipengele cha capacity charge, kampuni itakayotaka capacity charge ni ya kipuuzi.

“Katika sekta ya umeme kuna kampuni zinazolipwa hadi Sh bilioni mbili hadi saba kwa mwezi kutokana na malipo ya capacity charge.

“Yeyote atakayeingia na kusaini mkataba wa aina hiyo akaufute mara moja kabla haujanifikia, tutamfukuza kazi na atashtakiwa kwa sababu ni mwizi,” alisema.

Sera ya gesi na mafuta

Waziri alisema ili sera ya gesi na mafuta iweze kuandaliwa wananchi wanaoishi mikoa inayotoa raslimali hiyo wajulishwe waweze kutoa maoni yao nini kiingizwe kwenye sera hiyo.

“Tena nyinyi wataalam msiende na kuwabwagia tu hiyo draft na kuondoka, muipeleke wiki mbili kabla na baadaye mkutane nao ili waseme ni kitu gani wanataka kiingizwe kwenye sera hiyo,” alisema.

Mchango katika bajeti ya serikali

Waziri Muhongo aliyaagiza mashirika yote yaliyo chini ya wizara yake kujiandaa kuchangia bajeti ya serikali mwakani.

Alisema serikali kama mbia mkuu wa mashirika hayo lazima apatiwe gawio lake kila mwaka.

“Hata wale wanaopata hasara lazima waonyeshe kwamba katika kipindi fulani watakuwa wanatengeneza faida kwa hiyo gawio lake lazima lionekane, hatuwezi kuendelea kukusanya kodi katika viberti, bia, soda huku nyinyi mkiendelea kupokea fedha za serikali bila kurejesha gawio,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda alisema pamoja na mambo mengine wanatambua umuhimu wa kukamilika kwa Sera ya Gesi Asili na umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya utafutaji na uzalishaji mafuta ya mwaka 1980 kuondoa upungufu uliopo

Huyu ndiye alifaakuwa waziri mkuu au Raisi kabisa kuliko kuwa na genge la wezi wanaofilisi nchi hii ya Tanzania!!!Kasoro lichama lake linamwangusha si ajabu akatafutiwa mizengwe ili watu waendelee na ulaji wao!!!!

 
Prof big up komaa mpaka kieleweke hao wanaokupinga wana yao na wananufaika na ngawila za mafisadi
Ukiona wanakuletea zengwe kwenye utekelzaji wa yale unayoamini nimkwa manufaa ya nchi piga chini uwaziri kulinda heshima yako
Mkuu ni kweli badala ya kumkatisha tamaa kuwa hawezi kupambana na group linalo mzunguka tumtie moyo ili asonge mbele kutimiza azima yake ya kumkomboa Mtanzania aliye fanywa maskini kwa shinikizo la mafisadi!!!

 
Back
Top Bottom