Tanesco yazidi kubanwa; Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu; lina Kesi 200 zisizoisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco yazidi kubanwa; Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu; lina Kesi 200 zisizoisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145


  JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:22 NA ARODIA METER DAR ES SALAAM

  *Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji' tu
  *Asema shirika hilo hivi sasa lina kesi 200 zisizoisha.
  *Aitaka TPDC kupitia upya mikataba 26 ya gesi
  *Akataa fedha ya mafuta na gesi kuingizwa Hazina
  WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kesi mbalimbali zinazokabili mashirika yaliyo chini ya wizara yake likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni kichaka cha ‘ulaji' wa watu.

  Profesa Muhongo pia ameonya kuwa mtumishi atakayeingia mkataba mbovu na kampuni yoyote ya kigeni au ya ndani atafukuzwa kazi na kushtakiwa.

  Aliyasema hayo wakati wa akizindua bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency Dar es Salaam jana.

  Fedha nyingi katika Tanzania zinapotea kwa njia ya mikataba mibovu na kesi nyingi zisizoisha mahakamani.

  Alisema kwa mfano Tanesco peke yake kuna kesi zaidi ya 200 ambazo nyingi ni miradi ya watu wachache.

  Waziri alisema baadhi ya watumishi wanashirikiana na makampuni ya sheria kuyaibia mashirika kwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka.

  "Fedha nyingi katika nchi yetu zinapotea kwa kesi zisizoisha na mikataba mibovu… kesi hizo zinaifikisha bili zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka na kusababisha taifa kubaki katika ufukara.

  "Nimekwisha kusema ni marufuku kampuni moja kurundikiwa kesi nyingine na kampuni itakayopewa kazi hiyo lazima ishinde kesi nane kati ya 10, tofauti na hayo inyang'anywe mara moja… na tabia hii ife," alisema Profesa Muhongo.

  Kuhusu Bodi ya TPDC

  Akizindua boda ya TPDC, Profesa Muhongo aliwasimamisha wajumbe wapya wa bodi kila mmoja kwa dakika mbili akiwataka waeleze uzoefu wako na jinsi watakavyosaidia kuliinua shirika hilo.

  Baada ya kujielekeza waziri aliwakabidhi wajumbe hao mkoba wenye mikataba 26 ya TPDC ili waipitie na kutoa mapendekezo yao ndani ya miezi mitatu.

  Alisema Novemba 30 mwaka huu atakaa pamoja nao kujadili mkataba moja baada ya mwingine.

  "Hapa tuna mikataba 26 baadhi yake ni mibovu, kazi yenu ni kuipitia upya ni lazima kila mkataba ufanyiwe auditing (ukaguzi).

  "Nimeambiwa kisima kimoja kinalindwa kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 100 mpaka 150, kwa hiyo lazima bodi ipitie kwa makini suala hili ikiwezekana ulinzi huo ufanywe na jeshi letu ili fedha zibaki nchini.

  "Tusije tukafanya tena mkosa kama tulivyofanya kwenye sekta ya Madani. Kampuni nyingi ni wajanja msiwaamini hata kidogo, haiwezekani mtu anachimba kwa miaka 10 bila kulipa kwa kisingizio cha fedha alizotumia.

  Azuia mikataba mipya

  Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo amepiga marufuku mikataba mipya hadi ya sasa itakapopitiwa upya na kujiridhisha kwamba ipo kwa manufaa ya Watanzania.

  "Kuanzia sasa sitasaini mkataba wowote hadi hii iliyopo tutakapojiridhisha kuwa iko salama kwa manufaa ya watanzania." Alisema.

  Fedha za gesi na mafuta kutoingizwa Hazina

  Profesa Muhongo vilevile alisema fedha zote zitakazotokana na gesi na mafuta hazitaingizwa Hazina.

  Alisema hatua hiyo itaepusha fedha hizo kuchangwa na nyingine na baadaye kuchakachuliwa na hivyo kushindwa kuonekana zimefanya jambo gani.

  Waziri alisema fedha hizo zinapaswa kuonekana zimefanya kitu ambacho Watanzania watajivunia kuwapo kwa raslimali hiyo.

  "Fedha za gesi na mafuta hazitakwenda Hazina kwa sababu huko kuna matobo mengi. Sitaki zikachanganywe na nyingine ambazo zikienda kwenye halmashauri mwishowe tutasikia dawati moja limenunuliwa kwa Sh milioni 10," alisema.

  Azungumzia malipo ya huduma (capacity charge)

  Waziri Muhongo pia amepiga marufuku mashirika yote yaliyo chini ya Tanesco kuingia mkataba na kampuni unaotaka malipo ya huma (capacity charge).

  Alisema malipo hayo ni bandia na wizi wa wazi, na mtumishi yeyote atakayeingia mkataba wa aina hiyo atafukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa.

  "Ni marufuku kwa kampuni inayotaka kufanya biashara na sisi kuweka kipengele cha capacity charge, kampuni itakayotaka capacity charge ni ya kipuuzi.

  "Katika sekta ya umeme kuna kampuni zinazolipwa hadi Sh bilioni mbili hadi saba kwa mwezi kutokana na malipo ya capacity charge.

  "Yeyote atakayeingia na kusaini mkataba wa aina hiyo akaufute mara moja kabla haujanifikia, tutamfukuza kazi na atashtakiwa kwa sababu ni mwizi," alisema.

  Sera ya gesi na mafuta

  Waziri alisema ili sera ya gesi na mafuta iweze kuandaliwa wananchi wanaoishi mikoa inayotoa raslimali hiyo wajulishwe waweze kutoa maoni yao nini kiingizwe kwenye sera hiyo.

  "Tena nyinyi wataalam msiende na kuwabwagia tu hiyo draft na kuondoka, muipeleke wiki mbili kabla na baadaye mkutane nao ili waseme ni kitu gani wanataka kiingizwe kwenye sera hiyo," alisema.

  Mchango katika bajeti ya serikali

  Waziri Muhongo aliyaagiza mashirika yote yaliyo chini ya wizara yake kujiandaa kuchangia bajeti ya serikali mwakani.

  Alisema serikali kama mbia mkuu wa mashirika hayo lazima apatiwe gawio lake kila mwaka.

  "Hata wale wanaopata hasara lazima waonyeshe kwamba katika kipindi fulani watakuwa wanatengeneza faida kwa hiyo gawio lake lazima lionekane, hatuwezi kuendelea kukusanya kodi katika viberti, bia, soda huku nyinyi mkiendelea kupokea fedha za serikali bila kurejesha gawio," alisema.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda alisema pamoja na mambo mengine wanatambua umuhimu wa kukamilika kwa Sera ya Gesi Asili na umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya utafutaji na uzalishaji mafuta ya mwaka 1980 kuondoa upungufu uliopo

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ndio Uzuri wa kuteua Mawaziri ambao hawako kwenye SIASA za VYAMA wao ni KAZI kunufaisha TAIFA
   
 3. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na Ngeleja.
   
 4. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Aiseee!! Huyu Mh. Akiendelea na moto huu Watanzania tunaweza kuona mabadiliko na kunufaika na sekta husika.
  Big Up Prof. Muhongo..USIDANGANYIKE. Hazina imeoza na Ina matobo mengi sana.
  Kwa WALAFI na wanaofaidika na ufisadi kwa njia moja au nyingine wanaoita hizi ni NGUVU ZA SODA, all I can say is TIME WILL TELL. Muda wenu utafika wa kusaga meno.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mungu amjalie afya njema Waziri huyu ili atimize malengo yake.Mungu amlinde dhidi ya mafisadi.
   
 6. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ashughulikie basi na issue ya Symbion!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Muhongo anaenda vyema. Lakini sasa hili la kusema pesa zisiende hazina limekaaje? Atakuwa na bajeti ya wizara yake peke yake? Inabidi sheria ya fedha za umma ibadilishwe ili pesa za gesi ziwe na mfuko wake peke yake ambapo zitakuwa zinaingia na kutumiwa.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Katiba mpya inakuja, mawaziri watoje nje ya bunge (wasiwe wabunge) au wajumbe wa kamati za vyama vya siasa i.e NEC or CC. Anaweza kuwa mwanachama lakini asiwe mbunge or m-NEC. Pia kama wanasema wamesoma lazima kuwa na evidence ya elimu yao from a credible institution. Huu muda uliobakia hadi 2015 uwe ni ndio mwisho wa kuwa na cabinet ya magumashi.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu huyu atakimbia mwenyewe ngoja atakapokuja kujua kuwa madeal mengi ni ya mkuu wake ndo atakapo changanyikiwa na kujitafutia ka mrija kake!! Soon atakuwa kibogoyo huyu!!!
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  tunataka mawaziri wa ukweli kama huyu.!
   
 11. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wewe ni moja ya watz wachache walio wajinga zaidi. Mods toeni watu kama hawa humu jf.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Hata kesi ya Dowans ni chaka la ulaji wa DHAIFU, Rostam, Al Adawi na mafisadi wengine ndani ya Serikali na magamba.
   
 13. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ubarikiwe mara 7 sabini
   
 14. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kikubwa hapa akapate kikombe cha babu mapema kabisaaa, otherwise Appolo hospital in India inamsubiri, maaana kashikilia pabaya
   
 15. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Watu kama wewe ni wa kuogopa kama ukoma! unagopa kupambana kwa sababu ya kuwekewa sumu, pigana kidume!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  nampa muda,niote atasimamia kauli zake?
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,867
  Likes Received: 2,808
  Trophy Points: 280
  Yaani Mkuu nikipewa U-Mod naanza na watu wa aina hii!

  Kila kitu mashaka tu sijui kwa nini? Yaani yeyote atakayeponda mazuri yanayofanywa na mawaziri wa ukweli ni kulamba BAN tu mpaka wakome. Kama huyu sasa hivi ningekuwa nimeshamtandika BAN ya wiki 3!

  Huyu Prof atakuwa na akili sana MUNGU amlinde tuone anavyotutoa kwenye haya matatizo!
   
 18. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hivi W.E.H.U kama ninyi mnaomzodoa Mh. waziri mnataka afanye nini? Akiwa kama Ngeleja mnakuja juu, akiwa Muhongo halisi mnasema nguvu ya soda. Mnataka mpatiwe waziri wa aina gani? Au hadi muwe na waziri kama Nchimbi ndio mnafurahi? wabhongo bhana!
   
 19. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kumbuka hii ni Serikali ya Kikwete baya lolote linalofanywa na serikali yake tunamshambulia basi na zuri lolote lifanywalo chini ya serikali yake usisite kumpongeza ndo siasa komavu.
  Hongera Dkt Jakaya Kikwete kumteua Profesa kwa utashi wako bila ya kulazimishwa.Hongera Professa kumsaidia Ndugu Jakaya!
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280


  Anzeni na Jakaya Mrisho wa Kikwete.
   
Loading...