Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Kwa Prof. Muhongo hatimaye naona mwanga angavu kabisa wa matumaini. Huyu bwana siyo mwanasiasa. Ni mtendaji. Hataki utani wala ubabaishaji. Anachotaka ni outcome siyo output. Siyo akina nchimbi.
..inabidi tuwe macho kidogo hapa.
..waziri amesema kuna mikataba 26 na baadhi yake ni mibovu. halafu anawataka wajumbe wa bodi waipitie.
..sasa what happens kama wajumbe wa bodi watatofautiana na mtizamo wa waziri na kumrudishia majibu kwamba mikataba yote ni mizuri??
..kama waziri tayari ameona kuna mikataba mibovu, kwanini asitoe amri mara moja kwamba irekebishwe??
..tusiwe na haraka ya kushangilia ushindi. tusubiri miezi mitatu tuone kama kuna mikataba itarekebishwa, na zaidi ni mikataba mingapi.
nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na ngeleja.
ashughulikie basi na issue ya symbion!
Pole sana ndugu, usipoteze sana na muda na watu kama hawa, kwa kifupi ni kwamba kuna baadhi ya watu wamezi-set akili zao kwamba maadamu kitu fulani hakijafanywa au kusemwa na CHADEMA basi ni takataka, na wewe ukisema kitu chochote kukosoa CHADEMA hata kama mwisho wa siku una nia ya dhati kabisa ya kusaidia kuijenga CHADEMA bado utaambulia matusi tu na mimi nasema hawa ndio watu ambao wataiangusha CHADEMA hiyo hiyo wanayopiga kelele humu kila siku kwamba wanaipenda, sote tunapenda mabadiliko nchini mwetu na haijalishi nani anayaleta! Mh. Waziri ameongea vizuri sana na tunapata matuamaini kwamba atajaribu!
Nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na Ngeleja.
Andiko moja kwenye Biblia Linaesema tusiwe na haraka ya kuweka mikono ya baraka kwenye kichwa cha mtu, Binafsi nachelea kusema nimapema sana kuamini na kutekeleza ayasemayo pamoja na nia nzuru aliyonayo haijui rangi halisi ya chama chake cha CCM.
Acha kufuka mapovu kama kifutu. Mwaga mapoint tuyaone. vinginevyo tusubiri, muda ndio utaamua.Look this shuleless opening ur mouth empty minded....
U know nothing & u won't know anything in ur entire life....
how u come with such F****ing words.... Sie tunamjua huyu Prof. Muhongo, si jana, au leo..... shut..up... go to ur haemophrodite manji....
JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:22 NA ARODIA METER DAR ES SALAAM
*Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ulaji tu
*Asema shirika hilo hivi sasa lina kesi 200 zisizoisha.
*Aitaka TPDC kupitia upya mikataba 26 ya gesi
*Akataa fedha ya mafuta na gesi kuingizwa Hazina
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kesi mbalimbali zinazokabili mashirika yaliyo chini ya wizara yake likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni kichaka cha ulaji wa watu.
Profesa Muhongo pia ameonya kuwa mtumishi atakayeingia mkataba mbovu na kampuni yoyote ya kigeni au ya ndani atafukuzwa kazi na kushtakiwa.
Aliyasema hayo wakati wa akizindua bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency Dar es Salaam jana.
Fedha nyingi katika Tanzania zinapotea kwa njia ya mikataba mibovu na kesi nyingi zisizoisha mahakamani.
Alisema kwa mfano Tanesco peke yake kuna kesi zaidi ya 200 ambazo nyingi ni miradi ya watu wachache.
Waziri alisema baadhi ya watumishi wanashirikiana na makampuni ya sheria kuyaibia mashirika kwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka.
Fedha nyingi katika nchi yetu zinapotea kwa kesi zisizoisha na mikataba mibovu kesi hizo zinaifikisha bili zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka na kusababisha taifa kubaki katika ufukara.
Nimekwisha kusema ni marufuku kampuni moja kurundikiwa kesi nyingine na kampuni itakayopewa kazi hiyo lazima ishinde kesi nane kati ya 10, tofauti na hayo inyanganywe mara moja na tabia hii ife, alisema Profesa Muhongo.
Kuhusu Bodi ya TPDC
Akizindua boda ya TPDC, Profesa Muhongo aliwasimamisha wajumbe wapya wa bodi kila mmoja kwa dakika mbili akiwataka waeleze uzoefu wako na jinsi watakavyosaidia kuliinua shirika hilo.
Baada ya kujielekeza waziri aliwakabidhi wajumbe hao mkoba wenye mikataba 26 ya TPDC ili waipitie na kutoa mapendekezo yao ndani ya miezi mitatu.
Alisema Novemba 30 mwaka huu atakaa pamoja nao kujadili mkataba moja baada ya mwingine.
Hapa tuna mikataba 26 baadhi yake ni mibovu, kazi yenu ni kuipitia upya ni lazima kila mkataba ufanyiwe auditing (ukaguzi).
Nimeambiwa kisima kimoja kinalindwa kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 100 mpaka 150, kwa hiyo lazima bodi ipitie kwa makini suala hili ikiwezekana ulinzi huo ufanywe na jeshi letu ili fedha zibaki nchini.
Tusije tukafanya tena mkosa kama tulivyofanya kwenye sekta ya Madani. Kampuni nyingi ni wajanja msiwaamini hata kidogo, haiwezekani mtu anachimba kwa miaka 10 bila kulipa kwa kisingizio cha fedha alizotumia.
Azuia mikataba mipya
Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo amepiga marufuku mikataba mipya hadi ya sasa itakapopitiwa upya na kujiridhisha kwamba ipo kwa manufaa ya Watanzania.
Kuanzia sasa sitasaini mkataba wowote hadi hii iliyopo tutakapojiridhisha kuwa iko salama kwa manufaa ya watanzania. Alisema.
Fedha za gesi na mafuta kutoingizwa Hazina
Profesa Muhongo vilevile alisema fedha zote zitakazotokana na gesi na mafuta hazitaingizwa Hazina.
Alisema hatua hiyo itaepusha fedha hizo kuchangwa na nyingine na baadaye kuchakachuliwa na hivyo kushindwa kuonekana zimefanya jambo gani.
Waziri alisema fedha hizo zinapaswa kuonekana zimefanya kitu ambacho Watanzania watajivunia kuwapo kwa raslimali hiyo.
Fedha za gesi na mafuta hazitakwenda Hazina kwa sababu huko kuna matobo mengi. Sitaki zikachanganywe na nyingine ambazo zikienda kwenye halmashauri mwishowe tutasikia dawati moja limenunuliwa kwa Sh milioni 10, alisema.
Azungumzia malipo ya huduma (capacity charge)
Waziri Muhongo pia amepiga marufuku mashirika yote yaliyo chini ya Tanesco kuingia mkataba na kampuni unaotaka malipo ya huma (capacity charge).
Alisema malipo hayo ni bandia na wizi wa wazi, na mtumishi yeyote atakayeingia mkataba wa aina hiyo atafukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa.
Ni marufuku kwa kampuni inayotaka kufanya biashara na sisi kuweka kipengele cha capacity charge, kampuni itakayotaka capacity charge ni ya kipuuzi.
Katika sekta ya umeme kuna kampuni zinazolipwa hadi Sh bilioni mbili hadi saba kwa mwezi kutokana na malipo ya capacity charge.
Yeyote atakayeingia na kusaini mkataba wa aina hiyo akaufute mara moja kabla haujanifikia, tutamfukuza kazi na atashtakiwa kwa sababu ni mwizi, alisema.
Sera ya gesi na mafuta
Waziri alisema ili sera ya gesi na mafuta iweze kuandaliwa wananchi wanaoishi mikoa inayotoa raslimali hiyo wajulishwe waweze kutoa maoni yao nini kiingizwe kwenye sera hiyo.
Tena nyinyi wataalam msiende na kuwabwagia tu hiyo draft na kuondoka, muipeleke wiki mbili kabla na baadaye mkutane nao ili waseme ni kitu gani wanataka kiingizwe kwenye sera hiyo, alisema.
Mchango katika bajeti ya serikali
Waziri Muhongo aliyaagiza mashirika yote yaliyo chini ya wizara yake kujiandaa kuchangia bajeti ya serikali mwakani.
Alisema serikali kama mbia mkuu wa mashirika hayo lazima apatiwe gawio lake kila mwaka.
Hata wale wanaopata hasara lazima waonyeshe kwamba katika kipindi fulani watakuwa wanatengeneza faida kwa hiyo gawio lake lazima lionekane, hatuwezi kuendelea kukusanya kodi katika viberti, bia, soda huku nyinyi mkiendelea kupokea fedha za serikali bila kurejesha gawio, alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda alisema pamoja na mambo mengine wanatambua umuhimu wa kukamilika kwa Sera ya Gesi Asili na umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya utafutaji na uzalishaji mafuta ya mwaka 1980 kuondoa upungufu uliopo
Many thanks. But time will tell who is right-between me and you stupid self.wewe ni msaliti mkubwa! Mnakatisha tamaa watu wazalendo wa kweli, huyo manji kama anakudanganya siku zake zimekwisha zakutufanya sisi wajinga watu wenye bongo kama wewe ndiyo manasababisha nchi hii kuwa masikini kwa mawazo yenu ya kibinafsi.
A Conclusion based on a few data is as invalid as the person making such conclusionlazma tubadilike na kumpongeza mtu anapofanya vizuri sio kila kitu ubishi usio na maana,kwa hili unaonesha jinsi ulivyo maskini wa fikra!
kaza buti muhongo!
Katiba mpya inakuja, mawaziri watoje nje ya bunge (wasiwe wabunge) au wajumbe wa kamati za vyama vya siasa i.e NEC or CC. Anaweza kuwa mwanachama lakini asiwe mbunge or m-NEC. Pia kama wanasema wamesoma lazima kuwa na evidence ya elimu yao from a credible institution. Huu muda uliobakia hadi 2015 uwe ni ndio mwisho wa kuwa na cabinet ya magumashi.
Andiko moja kwenye Biblia Linaesema tusiwe na haraka ya kuweka mikono ya baraka kwenye kichwa cha mtu, Binafsi nachelea kusema nimapema sana kuamini na kutekeleza ayasemayo pamoja na nia nzuru aliyonayo haijui rangi halisi ya chama chake cha CCM.
Wewe humfahamu Muhongo. Huyu ni calibre ya Julius Nyerere. Hawezi kukubali hongo ya Manji au yeyote yule.Nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na Ngeleja.
jokaKuu,..inabidi tuwe macho kidogo hapa.
..waziri amesema kuna mikataba 26 na baadhi yake ni mibovu. halafu anawataka wajumbe wa bodi waipitie.
..sasa what happens kama wajumbe wa bodi watatofautiana na mtizamo wa waziri na kumrudishia majibu kwamba mikataba yote ni mizuri??
..kama waziri tayari ameona kuna mikataba mibovu, kwanini asitoe amri mara moja kwamba irekebishwe??
..tusiwe na haraka ya kushangilia ushindi. tusubiri miezi mitatu tuone kama kuna mikataba itarekebishwa, na zaidi ni mikataba mingapi.