Tanesco yazidi kubanwa; Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu; lina Kesi 200 zisizoisha

Ni kweli Prof Muhongo, walau unatupa matumaini, tatizo ni kwamba wewe ni NJIWA katika kundi la KUNGURU,.ufisadi wa nchi hii unapaliliwa na WAZEE,wakiona unagusa sana madili yao WATAKUTOA,.ushauri wangu kwako ni kwamba wakianza tu UPUUZI wao,jiuzulu.rudi zako UDSM,ili kulinda hadhi na heshima yako
 
Hivi W.E.H.U kama ninyi mnaomzodoa Mh. waziri mnataka afanye nini? Akiwa kama Ngeleja mnakuja juu, akiwa Muhongo halisi mnasema nguvu ya soda. Mnataka mpatiwe waziri wa aina gani? Au hadi muwe na waziri kama Nchimbi ndio mnafurahi? wabhongo bhana!

Pole sana ndugu, usipoteze sana na muda na watu kama hawa, kwa kifupi ni kwamba kuna baadhi ya watu wamezi-set akili zao kwamba maadamu kitu fulani hakijafanywa au kusemwa na CHADEMA basi ni takataka, na wewe ukisema kitu chochote kukosoa CHADEMA hata kama mwisho wa siku una nia ya dhati kabisa ya kusaidia kuijenga CHADEMA bado utaambulia matusi tu na mimi nasema hawa ndio watu ambao wataiangusha CHADEMA hiyo hiyo wanayopiga kelele humu kila siku kwamba wanaipenda, sote tunapenda mabadiliko nchini mwetu na haijalishi nani anayaleta! Mh. Waziri ameongea vizuri sana na tunapata matuamaini kwamba atajaribu!
 
Kweli nami nakubali Mawaziri wasiwe wabunge / wanasiasa. Dr.Muhongo tunakuombea. Kuna vitu viwili so far vinanifurahisha kwa huyu msomi.

1. Kuwashirikisha zaidi Manaibu wake, Wizara na Taasisi zilizo chini ya wizara na kuwapa nguvu ya kutenda
2. Uwazi katika vitendo na si kukimbilia TV na vyombo vya habari tu

Sasa Wataalam na Bodi wakisha pitia Mikataba mibovu hapo ndio tunaomba Dr. utoke adharani utueleze maazimio yenu nini kitafanyika na pia namna ya kuelekea kumpatia Mtanzania faida kutoka rasilimali za nchi yake.
 
Watu kama wewe ni wa kuogopa kama ukoma! unagopa kupambana kwa sababu ya kuwekewa sumu, pigana kidume!
Tahadhari ni sehemu ya maisha, hakuna sehemu nimesema naogopa kupambana, tatizo lako wewe ni kukurupuka.
 
Hivi W.E.H.U kama ninyi mnaomzodoa Mh. waziri mnataka afanye nini? Akiwa kama Ngeleja mnakuja juu, akiwa Muhongo halisi mnasema nguvu ya soda. Mnataka mpatiwe waziri wa aina gani? Au hadi muwe na waziri kama Nchimbi ndio mnafurahi? wabhongo bhana!
Naunga hoja kwa mikono miwili,
 
Nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na Ngeleja.

lazma tubadilike na kumpongeza mtu anapofanya vizuri sio kila kitu ubishi usio na maana,kwa hili unaonesha jinsi ulivyo maskini wa fikra!
kaza buti muhongo!
 
Hata kesi ya Dowans ni chaka la ulaji wa DHAIFU, Rostam, Al Adawi na mafisadi wengine ndani ya Serikali na magamba.

Dowans waliposhitaki ICC tukasema Tukubali yaishe hatushindi, kwani kila kitu kiko wazi, hao wameleta mitambo na inafanya kazi, watu wakatuona sisi wajinga> Leo imekuwa ni ulaji? Vipi Symbion? ni ulaji wa nani?
 
Wale wanaompinga prof watakuwa watoto wa mafisadi, mm kama mzalendo nampa big up na watz tuko nyuma yako, wakikupindua nasi tutawapindua, peoples power
 
Ashughulikie basi na issue ya Symbion!
Jina lako lingeendana kidogo na comment na tabia yako. Jamaa ameingia juzi tu na ndio kwanza Wizara husika inapitia mikataba yote kuangalia wapi kuna matobo. Tunaweza kuwa na "Patience" kidogo!? TIME WILL TELL.
Huyu jamaa ni mchapa kazi na sio MwanaSiasa. Issue ya Symbion wa kuishughulikia ni WEWE, MIMI NA WATANZANIA WOTE.
 
Mimi nilishasema humu kwenye Jf, kuwa Prof. Muhongo ni aina ya watu wanaofaa kuwa Rais wa nchi yetu, katibu kiongozi awe Maswi (katibu nishati na madini), Magufuli awe Waziri mkuu......! Dr. Ulimboka apewe waziri wa afya, Tanzania lazima iwe mahali pazuri pakuishi...!

Kibanga Msese
 
Prof Mungu akupe afya na Uzima tele nina iman umeme utashuka bei kwa mara ya kwanza ktk histor of Tz.
 
Utendaji hatutaki Maneno ..wala Operation Zimamoto

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Prof ana dhamira ya kweli ya kuonyesha tofauti. Ila aangalie maana wanaofaidika sana na ulaji si watu wadogo kama kina sie...wengine ni wakubwa kuliko hata yeye kwenye nafasi aliyonayo.
 
Mimi nilishasema humu kwenye Jf, kuwa Prof. Muhongo ni aina ya watu wanaofaa kuwa Rais wa nchi yetu, katibu kiongozi awe Maswi (katibu nishati na madini), Magufuli awe Waziri mkuu......! Dr. Ulimboka apewe waziri wa afya, Tanzania lazima iwe mahali pazuri pakuishi...!

Kibanga Msese

Mkuu, hiyo hatari na haifai kabisa kwani wengine hawatapenda.

Profesa Muhongo katibu mkuu wake Maswi na waziri wa Ujenzi Magufuli ni Sokoine no 2 na wanatakiwa waachwe wachape kazi. Maana baada ya hayati Sokoine sijaona waziri jembe ambae haogopi kuchapa kazi isipokuwa hawa watu watatu.

Kila nchi iliyoendelea ina watu wa aina hii na hakuna magarasa. Naunga mkono kabisa baraza la mawaziri lijumuishe wabunge wa kuteuliwa wa aina ya hawa jamaa kwani wanaleta tija kubwa sana.
 
..inabidi tuwe macho kidogo hapa.

..waziri amesema kuna mikataba 26 na baadhi yake ni mibovu. halafu anawataka wajumbe wa bodi waipitie.

..sasa what happens kama wajumbe wa bodi watatofautiana na mtizamo wa waziri na kumrudishia majibu kwamba mikataba yote ni mizuri??

..kama waziri tayari ameona kuna mikataba mibovu, kwanini asitoe amri mara moja kwamba irekebishwe??

..tusiwe na haraka ya kushangilia ushindi. tusubiri miezi mitatu tuone kama kuna mikataba itarekebishwa, na zaidi ni mikataba mingapi.
 

JokaKuu

Kitendo cha waziri kusema mikataba ipitiwe ni ishara tosha kuwa amegundua kasoro na nimzalendo, kwani ni mawaziri wangapi hawajafanya alichokifanya ukizingatia muda mfupi aliokaa wizarani....? Hata wajumbe wa bodi wakija na majibu kuwa mikataba 26 haina shida, yet tatizo sio waziri bali ni wajumbe.

Anatakiwa apongezwe kwa kila hatua moja anayopiga, na sio kumkatisha tamaa.....au kum'sumu, kwakua wachache maslahi yao yanaondolewa kwa manufaa ya umma.

Kuna mahali JK huwa simkubali, lakini kitendo cha kumchagua huyu bwana nampa big up sana yani.

Kibanga Msese
 
“Yeyote atakayeingia na kusaini mkataba wa aina hiyo akaufute mara moja kabla haujanifikia, tutamfukuza kazi na atashtakiwa kwa sababu ni mwizi,” alisema.
Serikali ikishaingia mkataba mbovu wa mabilioni ya hela halafu ukamfukuza kazi na kumfunga aliyeingia mkataba hiyo itatusaidia nini? Mbona concept nzima ya kuingia mikataba inatusumbua namna hii? Kwa nini mchakato wa mikataba uruhusu busara ya mtu fulani mmoja ambae ukikuta kauza nchi unamfukuza kazi na kumfunga, then what? That is enormously ridiculous mheshimiwa Waziri!
 

JokaKuu

Kitendo cha waziri kusema mikataba ipitiwe ni ishara tosha kuwa amegundua kasoro na nimzalendo, kwani ni mawaziri wangapi hawajafanya alichokifanya ukizingatia muda mfupi aliokaa wizarani....? Hata wajumbe wa bodi wakija na majibu kuwa mikataba 26 haina shida, yet tatizo sio waziri bali ni wajumbe.

Anatakiwa apongezwe kwa kila hatua moja anayopiga, na sio kumkatisha tamaa.....au kum'sumu, kwakua wachache maslahi yao yanaondolewa kwa manufaa ya umma.

Kuna mahali JK huwa simkubali, lakini kitendo cha kumchagua huyu bwana nampa big up sana yani.

Kibanga Msese
K.Msese,

..nasubiri hiyo miezi 3 kuona kama atafuta mkataba wowote ule.

..Prof.Muhongo akifuta mkataba hata mmoja mimi nitakuwa mstari wa mbele kumpongeza.

..mbona inajulikana kwamba mikataba ya uchimbaji dhahabu ina kasoro/matatizo na ni hasara tupu lakini Waziri hapendekezi ipitiwe upya??
 
Last edited by a moderator:
Huyu profesa kweli amenissuza roho!tatizo ni ile doubtfulness tuliyonayo ya chochote kinachotokea kwenye utawala wa ccm,thats it!Lakini otherwise,huu ni utendaji adimu kabisa kwenye serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom