TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Akili iliyotumika kutengeneza Corolla na IST, ndio hiyo hiyo iliyotumika kutengeneza Landcruiser V8.
Waliotengeneza GePG hawawezi shindwa erps
🤣 Haya pigeni marufuku software zote za nje ili zote ziandikwe na eGA. Microsoft, Android, Apple pigeni marufuku fanyeni kila kitu wenyewe. Software za kuongoza ndege airport tengenezeni wenyewe. Za mashine za hospitali tengenezeni wenyewe. Software ni software tuu ukitengeneza moja utaweza kutengeneza zote. 🤣
 
Kipindi cha kula hiki... wacha watu wale...hii nchi ni ya kuliwa liwa na wajanja...JPM alipowabana kwa pamoja walimuandama kwa matusi na dhihaka...
 
Mbona huulizi wakati serikali inanunua software za Microsoft Windows? Kwa nini eGA hawaandiki OS itumike serikalini?
We ungenyamaza tu mkuu. La sivyo unaweza ukahoji kwanini maisha yana ngazi tofauti. Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kila kitu ni msukumo tu. Serikali ikiwa na dira ya kwamba Tanzania itengeneze OS yake na computer zake inawezekana kabisa.

Ila kulinganisha ERP na OS ni ngazi tofauti.
 
Inawezekana kabisa. Ila itachukua muda kukamilisha miradi yote hiyo. Watu wenye akili kama zako wangeenda nje ya nchi kutafuta GePG.
eGa tayari software ya ERP wanayo, kama kuna mahitaji mahsusi ya Tanesco ingefanyiwa marekebisho, ili pesa zibaki hapahapa nchini mikononi mwa waTanzania.
 
Najua taasisi zetu,TRA,NIDA,Zina mifumo kama hii,lakini Haina ubora kabisa,lakini kuchukua hayo mapesa ukawapa watu wa nje,badara ya kuzipa Taasisi zetu za ICT zitengeneze hiyo software,ni matumizi mabaya sana ya pesa ya umma,hapo haitaishia kununua software tu,itabidi tukodishe na hardware ambazo ni compatible na hiyo software,na hata kama kulikuwa na haja ya kukodisha software,kwanini hatukwenda South Afrika?au Misri?kwanini twende nje ya Afrika.
 
TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
hujaona dollar hapo,
ni usd 30 million sawa na 69,000,002,280.00 Tanzania shillings {69 Billion }

Jaribu kuangalia source zako za habari sidhani kama ni mill 30
tupeni source mkuu, tujihakiki.
 
Hiyo software hatuwezi kutengeneza? Mbona serikali inatoa mamilioni ya fedha kusomesha wataalamu wa IT kila mwaka?
 
Kama wanayo si wangerekebisha halafu wangewapa Tanesco wanasubiri nini? Tena ERP software yetu tuanze kufanya export nayo kama biashara tuuze au tukodishe nchi zingine ituingizie hela. Tuendelee na kutengeneza hizo zingine tushindane na Microsoft, Android, Apple na makampunzi mengine tunazonunua software zao unaonaje bosi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…