TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

Huyu kukujibu lazima akuombe vyote au kimojawapo ya vifuatavyo
1. Uende PM
2. Umpe meter number
3. Utaje jina lako

Yaani utafikiri bila kumpa hayo makitu hatakumbuka majibu vizuri..
Na siyo tatizo la mtu mmoja au sehemu moja tuu.
Ni tatizo la nchi nzima.
Ikiwa Dodoma makao makuu ya nchi hali ni hiyo, je mikoa ya pembezoni huku hali ikoje?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Huu Ni zaidi ya urasimu, unataka taarifa za mtu mmoja badala ya kutoa maelezo ya pamoja.
Malalamiko yako mengi, au hali hamuioni?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Huu Ni zaidi ya urasimu, unataka taarifa za mtu mmoja badala ya kutoa maelezo ya pamoja.
Malalamiko yako mengi, au hali hamuioni?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
ELIMU KUTOKA TANESCO

TOA TAARIFA SAHIHI NA KAMILI ILI KUPATIWA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI

Mpendwa mteja wetu unapotoa taarifa kupitia njia zetu mbadala za Mitandao ya Kijamii Whatsapp, Facebook, Twitter Instagram Jamii forum, Barua pepe nk unashauriwa kutoa taarifa kamili zitakazowawezesha wataalamu wetu na viongozi kukupatia Huduma bora na za haraka. Tunakuomba uzingatia yafuatayo[emoji116][emoji116]

1. Jina la mtoa taarifa
Hii inatusaidia kumtambua mtoa taarifa kwenye mifumo yetu. Hakikisha unapewa namba ya Taarifa maarufu kama (TB namba) Ili mafundi wakiagizwa kuja kukuhudumia isije kutokea (wakagongana). Kama usipotoa taarifa ukapewa namba ya taarifa, mafundi wawili au watatu wanaweza kuja kwako kwa wakati mmoja.

2. Eneo, Wilaya, kijiji Mtaa Hii inatusaidia kujua kazi fulani inafanyiwa kazi na ofisi ipi na kujua kama tatizo la eneo husika limeshatolewa taarifa na wateja wengine.
Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti

2. Alama au mtu au kitu maarufu kilichopo eneo lako
Taja, Mfano nyuma ya ofisi ya Mbunge, karibu na Msikiti/Kanisa la eneo X, Ofisi za Serikali, Ofisi za watu binafsi , watu mashuhuri mfano kulia mwa Nyumba ya Msanii X iliyopo eneo la Madale nk.

3. Namba ya simu
Namba ya simu ya mteja aliiyetoa taarifa au inayopatikana. Namba hii inatusaidia kumfikia mteja aliyetoa taarifa kwa wakati, na pia kumpigia mteja aliyetoa taarifa kujua kama alihudumiwa au bado.

4. Jinsi ya kufika eneo husika
Toa maelezo ya ziada ya jinsi ya kufika nyumbani kwako ili hata wataalamu wetu wakifika na simu zako hazipatikani iwe rahisi kukupata au kuulizia kwa majirani zako.

5. Elezea kwa ufasafa unachohitaji, unacholalamika, au unachoomba
Ni muhimu sana kutaja nini unakitolea taarifa ili wataalamu wa TANESCO wajue na kujiandaa kabla ya kufika kwako.

6. Muda wa kutokea kwa tatizo
Kama ni hitilafu au tatizo linalohitaji ufumbuzi wetu tafadhali onesha tatizo limetokea tangu lini au hutokea muda gani.

6. Namba ya mita
Kama ni tatizo la mita au taarifa zinazohusu manunuzi ya umeme uwe na namba ya mita na ni changamoto gani unaipata mfano: __Nikiingiza umeme mita namba xxx inaandika connect au error 77, FF1, Sleep, au nikinunua umeme wa shilingi kadhaa napata ujumbe fulani mfano Insuffient balance nk_

7. Namba ya taarifa
Kama mteja ulishatoa taarifa TANESCO kwa kupiga simu, au kufika TANESCO, anashauriwa kuonesha namba ya taarifa uliyopatiwa wakati wa kutoa taarifa na Ofisi Husika mfano NMR042021TB-0008

Zingatia

Huduma bora inaanza na utoaji wa taarifa kamili na fasaha

TANESCO Tunayaangaza Maisha Yako
 
Ni kweli mkuu, kuna kaka yangu nimemlipia hiyo elfu 27 lakini mpaka leo hajaunganishwa ,

Wafanyakazi wengi Tanesco hawajapenda kauli ya waziri vile hawana pa kulalamika wanatutesa sisi wananchi
 
Tusaidie

Jina

Simu

Wilaya

Tuangalie na kukupatia taarifa kamili
 
Hujajibu bado, je 27000 ndiyo bei ya kufungiwa umeme au lah? Au hiyo bei inazo conditions?
Eneo nililopo mwananzengo katakiwa kulipa laki8, panahitajika nguzo2 kufikishiwa umeme, je hii Ni sahihi? Tupe majibu kwanza

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Hujajibu bado, je 27000 ndiyo bei ya kufungiwa umeme au lah? Au hiyo bei inazo conditions?
Eneo nililopo mwananzengo katakiwa kulipa laki8, panahitajika nguzo2 kufikishiwa umeme, je hii Ni sahihi? Tupe majibu kwanza

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Kwa maeneo yanayohitaji kusogeza miundombinu wateja wanashauriwa kusubiri huduma isogezwe ili waweze kulipia 27000 tu na kufungiwa umeme.
 
Hii elf 27 waziri alianza kuiongea zamani sana tangu kipindi cha kampeni za 2020, mimi kipindi hicho nilikuwa sijaweka umeme......nilivyoenda kulipia walinitoza laki tatu wakadai elf 27 ni umeme wa vijijini. Inavyooneka waziri anaiongea hiyo buku 27 kisiasa zaidi............
 
Mimi nilitozwa laki tatu kipindi waziri alishasema elf 27 na sikuhitaji nguzo hata moja zaidi ya mita na waya....hapo unasemaje?
 
Hii elf 27 waziri alianza kuiongea zamani sana tangu kipindi cha kampeni za 2020, mimi kipindi hicho nilikuwa sijaweka umeme......nilivyoenda kulipia walinitoza laki tatu wakadai elf 27 ni umeme wa vijijini. Inavyooneka waziri anaiongea hiyo buku 27 kisiasa zaidi............
Hakuna siasa na Nia ya Serikali kupitia TANESCO ni kuhakikisha wateja wote wanafungiwa umeme kwa bei elekezi ya 27000 tu
 
Je, kwenye ile laki tatu niliyotoa, mtanirudishia chenji ili niitumie kuendelea kulipia LUKU?
 
Kalemani, ndalichako wangebadilishwa kwny hizo wizara au watolewe kabisa.

Hao Wapo kimazoea mno mpaka wanadharaulika.
wamekalia wizara hizo 6 years in vain.

Awekwe waziri mpya mwingne aggressive.

Uprofesa wa ndalichako kwny ualimu na mazao ya utendaji wake nao ni questionable hana tofauti na dr kawambwa.
 
Hakuna siasa na Nia ya Serikali kupitia TANESCO ni kuhakikisha wateja wote wanafungiwa umeme kwa bei elekezi ya 27000 tu
Zinatakiwa nguzo mbili ili umeme ufike kwenye nyumba hapo mtu anatakiwa alipe sh ngap za nguzo na gharama za mita pamoja na kufungiwa umeme.

Sehemu n hadhi ya Kijiji katika mkoa wa kilimanjaro.

Naomba full gharama tafadhali wiring inamiaka miwili Sasa toka ikamilike
 
Hapo mpaka tusogeze miundombinu ndio uweze kulipia gharama halisi
 
Mkuranga pwani ni zaidi ya matatizo.
Unajaza fomu lakini saveya kuja kwako bila maalifa ni ndoto. Hiyo ni savey, kuungwa ni Jambo jingine. Watu wanamaliza miezi bila kutembele, ukipiga simu unajisumbua. Meneja ndo hapokeagi simu kabisa labda za wakezake.
Amekuja Meneja Mpya hapo. Yuko Poa sana na msikivu. Mfuate ofisini.
 
Hapo mpaka tusogeze miundombinu ndio uweze kulipia gharama halisi

Kiuhalisia n nguzo moja tuu hyo ya pili inakuwa mwenye ndani ya compound.

Nguzo waliweka wakang'oa huu n mwaka watatu unaisha nguzo hazifiki Ila mwingine zipo.

Nipe gharama ya kushea nguzo pili nipe mawasiliano ya wahusika wa nguzo mkoa wa kilimanjaro kwa utatuzi wa hili
 
Back
Top Bottom