TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

Kiuhalisia n nguzo moja tuu hyo ya pili inakuwa mwenye ndani ya compound.

Nguzo waliweka wakang'oa huu n mwaka watatu unaisha nguzo hazifiki Ila mwingine zipo.

Nipe gharama ya kushea nguzo pili nipe mawasiliano ya wahusika wa nguzo mkoa wa kilimanjaro kwa utatuzi wa hili
Gharama inatolewa mara baada ya mteja kufanya maombi ya umeme akapimiwa na kupatiwa gharama kwa maeneo ambayo miundombinu ya umeme imefika.Hakuna gharama ya nguzo wala vifaa vinavyotumika kukufungia umeme
 
Na siyo tatizo la mtu mmoja au sehemu moja tuu.
Ni tatizo la nchi nzima.
Ikiwa Dodoma makao makuu ya nchi hali ni hiyo, je mikoa ya pembezoni huku hali ikoje?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Sasa wao badala ya kulichukua kama tatizo wanataka nchi nzima tuwape majina na namba za simu na tulipo..!! kesho na kesho kutwa tukutwe na ugaidi..!!
 
Sasa wao badala ya kulichukua kama tatizo wanataka nchi nzima tuwape majina na namba za simu na tulipo..!! kesho na kesho kutwa tukutwe na ugaidi..!!
Unaweza kutumia njia nyingine kutoa taarifa kwa kuwa hakuna taarifa la nchi nzima linaweza kuwa tatizo la mtu au eneo fulani
 
Unaweza kutumia njia nyingine kutoa taarifa kwa kuwa hakuna taarifa la nchi nzima linaweza kuwa tatizo la mtu au eneo fulani
Ukishaambiwa na mtu kwamba hata huku ni hivyo hivyo hata kule ni vile vile m,aana yake ukusanye taarifa za maeneo yaliyotajwa, ACHANA NA KUTAKA KUJUA REAL IDENTITY ZA WATU..!! Unless otherwise nia yako si kujua matatizo ya TANESCO na kuyatatua, bali una nia nyingine..
 
Kwa maeneo yanayohitaji kusogeza miundombinu wateja wanashauriwa kusubiri huduma isogezwe ili waweze kulipia 27000 tu na kufungiwa umeme.
Hapo mpaka tusogeze miundombinu ndio uweze kulipia gharama halisi
Huu ni urasimu usio na msingi wowote. Mtu anahitaji umeme mmekaa mpaka siku mkijisikia kusogeza nguzo moja ndio apate umeme? Mnakera kwa kweli
 
ELIMU KUTOKA TANESCO

TOA TAARIFA SAHIHI NA KAMILI ILI KUPATIWA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI

Mpendwa mteja wetu unapotoa taarifa kupitia njia zetu mbadala za Mitandao ya Kijamii Whatsapp, Facebook, Twitter Instagram Jamii forum, Barua pepe nk unashauriwa kutoa taarifa kamili zitakazowawezesha wataalamu wetu na viongozi kukupatia Huduma bora na za haraka. Tunakuomba uzingatia yafuatayo

1. Jina la mtoa taarifa
Hii inatusaidia kumtambua mtoa taarifa kwenye mifumo yetu. Hakikisha unapewa namba ya Taarifa maarufu kama (TB namba) Ili mafundi wakiagizwa kuja kukuhudumia isije kutokea (wakagongana). Kama usipotoa taarifa ukapewa namba ya taarifa, mafundi wawili au watatu wanaweza kuja kwako kwa wakati mmoja.

2. Eneo, Wilaya, kijiji Mtaa Hii inatusaidia kujua kazi fulani inafanyiwa kazi na ofisi ipi na kujua kama tatizo la eneo husika limeshatolewa taarifa na wateja wengine.
Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti

2. Alama au mtu au kitu maarufu kilichopo eneo lako
Taja, Mfano nyuma ya ofisi ya Mbunge, karibu na Msikiti/Kanisa la eneo X, Ofisi za Serikali, Ofisi za watu binafsi , watu mashuhuri mfano kulia mwa Nyumba ya Msanii X iliyopo eneo la Madale nk.

3. Namba ya simu
Namba ya simu ya mteja aliiyetoa taarifa au inayopatikana. Namba hii inatusaidia kumfikia mteja aliyetoa taarifa kwa wakati, na pia kumpigia mteja aliyetoa taarifa kujua kama alihudumiwa au bado.

4. Jinsi ya kufika eneo husika
Toa maelezo ya ziada ya jinsi ya kufika nyumbani kwako ili hata wataalamu wetu wakifika na simu zako hazipatikani iwe rahisi kukupata au kuulizia kwa majirani zako.

5. Elezea kwa ufasafa unachohitaji, unacholalamika, au unachoomba
Ni muhimu sana kutaja nini unakitolea taarifa ili wataalamu wa TANESCO wajue na kujiandaa kabla ya kufika kwako.

6. Muda wa kutokea kwa tatizo
Kama ni hitilafu au tatizo linalohitaji ufumbuzi wetu tafadhali onesha tatizo limetokea tangu lini au hutokea muda gani.

6. Namba ya mita
Kama ni tatizo la mita au taarifa zinazohusu manunuzi ya umeme uwe na namba ya mita na ni changamoto gani unaipata mfano: __Nikiingiza umeme mita namba xxx inaandika connect au error 77, FF1, Sleep, au nikinunua umeme wa shilingi kadhaa napata ujumbe fulani mfano Insuffient balance nk_

7. Namba ya taarifa
Kama mteja ulishatoa taarifa TANESCO kwa kupiga simu, au kufika TANESCO, anashauriwa kuonesha namba ya taarifa uliyopatiwa wakati wa kutoa taarifa na Ofisi Husika mfano NMR042021TB-0008

Zingatia

Huduma bora inaanza na utoaji wa taarifa kamili na fasaha

TANESCO Tunayaangaza Maisha Yako
Yaani nyie watu utendaji wenu unakera sana. Mtu anawaletea form eneo lake limepimwa anawatajia hadi namba ya kiwanja na block lakini bado kwenye form zenu hamjazi taarifa sahihi. Kwanini msiwe mnachukua ramani za mipango miji ili kuwafikia wateja kwenye maeneo yaliyopimwa kirahisi. Sasa mimi niko eneo lililopimwa na linajulikana bado mnataka eti nisema nakaa karibu na kitu gani sijui.

Tanesco inabidi mbadilike mnachangia kurudisha nyuma taifa kwa huu ujinga ujinga. Mtua anaporudisha form kwanini kusiwe na register ya kusaini ili kutrack uhalali wa kucheleweshewa huduma. Hili hamlifanyi makusudi ili kukwepa lawama zinazotokana na uzembe wa makusudi mnayofanya ili mpatiwe rushwa.

Kwanini msifanye kama Kenya kuwe na makampuni yanayowapelekea watu umeme au kama mlivyofanya vijijini kwenye miradi ya REA. Yaani mimi nikianza tu ujenzi makampuni yanakuja kunishawishi kama mteja niunganishiwe umeme na nyie kama Tanesco mnamalizana na hayo makampuni ( yaani sub contractors). Sasa mnajirundikia kazi zote wenyewe then mnasema eti wateja wamekua wengi mnashindwa kuwahudumia.

Huku ni kutokuwajibika kwa makusudi kabisa na kuhujumu nchi. Wateja wanapokua wengi basala ya kuongeza alternative za kuwahudumia mnaanza blabla za ajabu ajabu. Mnahujumu nchi nyie watu sijui kwanini hamtumbuliwi hapo.
 
Tafadhali onesha uungwana kwa kutoa taarifa tunazoomba hata kwa PM au hapa badala ya kulalamika bila kutusaidia sisi kukuhudumia
 
Tafadhali onesha uungwana kwa kutoa taarifa tunazoomba hata kwa PM au hapa badala ya kulalamika bila kutusaidia sisi kukuhudumia
Kwenye uzi huu nimetaja maeneo ambayo mmetelekeza nguzo na watu hawana umeme nendeni mkaanze huko. Unataka taarifa zangu za nini wakati nimekutajia maeneo yenye kero.
 
Mimi hapa nimeshavuja zaidi ya laki mbili na elfu nane......!.kuna hela ya ramani, kuna hela ya mhuri, kugongea mhuri, hela ya survey hela ya makolokocho gani sijui.
 
Watanzania mmejaa ujinga Sana , Takukuru ipo , unashindwa vipi kwenda kuchukua hela za takukuru uwape.

Kila Kitu mnataka msaidiwe na serikali mna akili Nyie kweli.
 
Ukishaambiwa na mtu kwamba hata huku ni hivyo hivyo hata kule ni vile vile m,aana yake ukusanye taarifa za maeneo yaliyotajwa, ACHANA NA KUTAKA KUJUA REAL IDENTITY ZA WATU..!! Unless otherwise nia yako si kujua matatizo ya TANESCO na kuyatatua, bali una nia nyingine..
Mjinga Huyo kapewa kazi kwa kushusha sketi anajibu hovyo hovyo.
 
Gharama inatolewa mara baada ya mteja kufanya maombi ya umeme akapimiwa na kupatiwa gharama kwa maeneo ambayo miundombinu ya umeme imefika.Hakuna gharama ya nguzo wala vifaa vinavyotumika kukufungia umeme
Naomba utatatuzi mmenihamisha kutoka matumizi yakawaida na kuniweka katika matumizi makubwa baada yakuingiza key changed luku ,token hazingii na simu yenu haipokelewi
 
Mzee ukifuata mambo ya tanesco utakufa na corona dirisha la 3
Hawa jamaa tuliamua kuachana nao hela tumewapa tukasema basi
 
Back
Top Bottom