TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
4,510
Reaction score
6,607
Kama nilivyoandika hapo juu ni bora waziri wa nishati ukatengue kauli ya kuunganisha umeme kwa 27,000. Maana wanachi wengi hasa wenye umbali wa kuhitaji nguzo moja ama mbili sasa hivi hawahudumiwi kabisa. Ukitaka kupata control number unaambiwa ulipie angalau laki moja kwa kila nguzo na hiyo laki moja kwa kila nguzo haiingii serikalini.

Bei elekezi ya 27,000 imegeuka mwanya mpya wa kuomba rushwa kwenye ofisi za Tanesco. Hata nguzo walizosambaza mitaani wameziacha chini zinaliwa na mchwa mara baada ya kupewa bei hiyo elekezi.

Nashauri waziri wa nishati utembelee kule Dodoma mathalani maeneo ya Chidachi, Makulu, Mkonze, Miganga n.k. Kule utakuta nyumba nyingi zimekamilika lakini hazijaunganishwa na umeme wa Tanesco. Wenye kuweza wameamua kuweka Solar ili maisha yaendelee.
 
Naungana na mtoa mada nilienda ofisi moja ya Tanesco kuulizia mbona nimelipia tokea November na sijafungiwa na jirani kalipia April na kashafungiwa na wote tulikua na uhitaji wa nguzo nilichojibiwa ni kwamba huyo jirani kalipia full amount ni bora tuwekwe wazi ni kiasi gani kinatakiwa kulipwa
 
mkuu jiongeze, iyo 27k yote inaenda tra kama kodi, tanesco hawana chao hapo
alaf ufungiwe umeme bure?
utakaa sanaaaaaa
Hiyo 27,000/- iende yote TRA kama kodi, kwa 18% ya hela ipi? Wakati wanaitamka hiyo 27,000/- walijua kuna hayo makitu ya kodi na hela ya kubaki TANESCO
 
Back
Top Bottom