TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

Mkuranga pwani ni zaidi ya matatizo.
Unajaza fomu lakini saveya kuja kwako bila maalifa ni ndoto. Hiyo ni savey, kuungwa ni Jambo jingine. Watu wanamaliza miezi bila kutembele, ukipiga simu unajisumbua. Meneja ndo hapokeagi simu kabisa labda za wakezake.
tanesco ni Jipu tena lisiloiva
 
Gharama inatolewa mara baada ya mteja kufanya maombi ya umeme akapimiwa na kupatiwa gharama kwa maeneo ambayo miundombinu ya umeme imefika.Hakuna gharama ya nguzo wala vifaa vinavyotumika kukufungia umeme
Tuambie zile nguzo bure nchi nzima ziko wapi
Na kwanini malalamiko ya wananchi watendaji wenu hawayatatui
 
Tuambie zile nguzo bure nchi nzima ziko wapi
Na kwanini malalamiko ya wananchi watendaji wenu hawayatatui
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Hizo taarifa zote unazotaka ni za nini hasa jibu hayo maswali Kwa faida ya wote hapa hapa
 
Alisema"mtanikumbuka kwa mema"! Hao wafanyakazi wa Tanesco wanaoweka mgomo baridi kwa nini wasitimuliwe wote iwe fundisho kwa wengine! Wakirudi mtaani na wao wawe wanapanga foleni ya kuunganishiwa umeme ili wajifunze! Dr. JPM, we really miss you! May your precious soul rest in eternal peace and power our great African hero, amen !
Anakumbukwa na genge

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Malipo ya 27,000 yanalipwa kwenye nyumba yenye sifa ambayo ipo ndani ya mita 30,
Nyumba yako ikiwa mbali zaidi ya mita 30 na panahitaji nguzo inabidi usubirie mpaka Tenesco walete miundombinu yao Nguzo na waya ziwe karibu ndani ya mita 30 utalipa hiyo elf 27.

kama Nyumba yako iko mbali zaidi ya mita 30 sehemu yenyewe Nguzo basi tambuwa kuwa hauna vigezo na sifa ya Kulipa 27,000
Waziri ameleta shida, alisema nguzo ni bure. kazi sana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kama nilivyoandika hapo juu ni bora waziri wa nishati ukatengue kauli ya kuunganisha umeme kwa 27,000. Maana wanachi wengi hasa wenye umbali wa kuhitaji nguzo moja ama mbili sasa hivi hawahudumiwi kabisa. Ukitaka kupata control number unaambiwa ulipie angalau laki moja kwa kila nguzo na hiyo laki moja kwa kila nguzo haiingii serikalini.

Bei elekezi ya 27,000 imegeuka mwanya mpya wa kuomba rushwa kwenye ofisi za Tanesco. Hata nguzo walizosambaza mitaani wameziacha chini zinaliwa na mchwa mara baada ya kupewa bei hiyo elekezi.

Nashauri waziri wa nishati utembelee kule Dodoma mathalani maeneo ya Chidachi, Makulu, Mkonze, Miganga n.k. Kule utakuta nyumba nyingi zimekamilika lakini hazijaunganishwa na umeme wa Tanesco. Wenye kuweza wameamua kuweka Solar ili maisha yaendelee.
Sidhani kama hii ni kweli mimi nimewekewa kwa bei hiyohiyo ya 27,000 nadhani zipo sababu zingine tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Ili tanesco ifanye kazi sawasawa inatakiwa iwekwe chini ya usimamizi maalumu. Serikali iingie gharama lakinu itasaidia kumaliza haya makandokando.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Anakumbukwa na genge

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Tujijkumbushe. Mwaka 2016 EWURA waliidhinishia TANESCO kupandisha gharama za utumiaji umeme kwa karibu asilimia 15. Baada ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA kutangaza ongezeko hilo mara moja Rais alitengua uteuzi wake. Tangu wakati huo karibu miaka mitano sasa, si TANESCO wala EWURA walidhubutu kuongeza gharama tofauti na yaliyokuwa mazoea yao. Tujikumbushe tu.
 
Hii nchi ukisikia tamko lolote kutoka kwa viongozi usilitilie maanani, maana maneno siku zote yanaenda na upepo tu, na hao tanesco huwa hawamsikilizi yeyote ni wao na maamuzi yao tu
 
Back
Top Bottom