TANESCO tunataka majibu ya tuhuma kuhusu udini

TANESCO tunataka majibu ya tuhuma kuhusu udini

Sasa hivi mtu anaweza kupita
Mtaani kwake akauliza majirani
Zake dini zao akiona kuwa
Waislamu ni wengi au wakristu
ni wengi basi ataleta mada hapa
Kuwa kuwa Kuna udini mtaani
Kwake.

Iweje watu wa dini moja wawe
Wengi kuliko dini nyingine mtaani
Kwao? Hapo atakuwa kamaliza
Utafiti wake na kutupa matokeo

Huko ndiko tunako elekea
Watanzania wa leo. Ni aibu
na hatari kwa taifa letu changa.
 
Angalia hata idadi wa wahitimu wa fani za umeme wengi ni wakristo..sasa kama ukwel ndio huo ulitaka hao waislamu wachukuliwe kutoka madrasa ili kukidhi unachokitaka...fikiria kwa mapana...fikiria shule za kiislamu zinatoa product gan ndio uje ulalamike...basi waambien vyuon wasiwe wanadahili wakristo ili mwisho wa siku idadi itimie na waislamu wapate upendeleo...badala yakufikiria chanzo cha tatizo unajadili matokeo
 
Na watamaliza hadi misitu yetu, wameagiza mtu awatengenezee ALUTARE.


What is service charge?

A type of fee charged to cover services related to the primary product or service being purchased. For example, a concert venue may charge a service fee in addition to the initial price of a ticket in order to cover the cost of security or for allowing electronic purchases. Another example would be a fee for using the ATM of a competing bank.
Mimi nadhani Service charge ni muhimu kwa shirika hila la uma kwa sababu zifuatazo

  1. Gharama kubwa za uwekezaji kuanzia kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme,Gharama hizi kubwa zinapelekea wawekezaji kuona kuwa kuwekeza kwenye umeme kunachelewa sana kulipa (Long payback period),Hivyo shirika hili la uma limejitahidi kufikisha umeme hata maeneo yasiyo na faida hivyo kulichangia service charge ni kulipa nguvu Zaidi
  2. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka,nyaya kukatika,meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bura kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili
  3. Service charge mimi naiona kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme.
  4. Sio wateja wote wanaolipa service charge bali na kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku mimi nikiwepo mmoja wao naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.
 
Mkuu uko sahihi lkn ujue kwamba kwa hali hii naamin hata waajiriwa ktk sekta husika wengi watakuwa ni ndg za viongoz ambapo itakuwa ni muendelezo wa imani flani ndani ya idara.
 
Hii nchi daah Tanesco imekuwa kama Kigango wagalatia watu bwana Yesu asifiwe.

KUDHIBITI WIZI WA UMEME
Shirika linaendelea na Kampeni maalum katika mikoa yote ya kuwakamata wezi wa umeme na kuwachukulia hatua kali. Pamoja na hatua nyingine zitakazochukuliwa, wezi wa umeme watakuwa wanatangazwa hadharani na kufunguliwa mashtaka. Hivyo ninatoa rai kwa ye yote ambaye amekuwa akijihususha na wizi wa umeme ajisalimishe mwenyewe kwa kwenda kwa Meneja wa Mkoa anakopatia huduma. Kama hawatajisalimisha kwa hiari hatua zilizokusudiwa dhidi yao zitachukuliwa pasipo huruma yo yote. Tunatoa siku saba kwa wateja wanaojua kwamba mita zao zimechezewa kujisalimisha wao
 
Mkuu uko sahihi lkn ujue kwamba kwa hali hii naamin hata waajiriwa ktk sekta husika wengi watakuwa ni ndg za viongoz ambapo itakuwa ni muendelezo wa imani flani ndani ya idara.

KERO ZA HUDUMA KWA WATEJA
Ukiacha kero zinazosababishwa na Miundombinu, TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadibisha wafanyakazi
wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja. Baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa ni pamoja na lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma, kucheleweshewa huduma, ubadhirifu nk.
Shirika linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeshaanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo. Kwa mfano katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo wizi na ubadhirifu. Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana. Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, Wahandisi na Wahasibu.
Shirika litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi ye yote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa, anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakabobainika kuachishwa kazi.
Tumeanza maandalizi ya kutoa namba maalum za simu kwa wateja wetu ambazo zitatumika kutoa taarifa ya vitendo kama hivyo vinavyofanywa na wafanyakazi wetu ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
 
Ramadhani Dau aliitwa mdini/mujahidina kisa ni kuonyesha mapenzi kwa dini yake waziwazi.Laiti dau angekuwa mlevi na mla nguruwe angezeekea NSSF tena bila kelele.Sikuwahi kusikia mtumishi wowote wa NSSF kwamba alishawahi kunyanyaswa kwa dini yake.Hii nchi inahitaji uvumilivu wa kiwango cha mwisho.

MIUNDOMBINU YA TANESCO
Miongoni mwa kero kubwa inayolalamikiwa sana na wateja wetu ni kukatika umeme kunakosababishwa na uchakavu wa miundombinu. Ukweli ni kwamba baadhi ya miundombinu tuliyo nayo ni ya siku nyingi wakati matumizi ya umeme
yameendelea kuongezeka kwa kasi sana. Kwa mfano nyingi ya Substations katika jiji la Dar es Salaam zimejengwa katika miaka ya 80 na 90. Wakati huo wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa chini ya milioni 3. Sasa hivi wakazi wa jiji ni zaidi ya milioni 5 na hivyo miundombinu iliyopo inaelemewa sana.
Jitihada za kurekebisha hali hii zilikwishaanza ambapo sasa kuna miradi mikubwa inaendelea katika jiji la Dar es Salaam na itakapokamilika itasaidia sana kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme. Kwa kiasi fulani kukatika huko kwa umeme hasa katika jiji la Dar es Salaam kunatokana pia na utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi inayotekelezwa ni pamoja na ule unaojengwa kusini mwa Dar es Salaam kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambao utaboresha umeme maeneo ya Kigamboni, Kurasini, Mbagala, Mkuranga, Kisarawe, Gongolamboto, Ukonga, Kitunda, Vingunguti na Tabata
Mradi mwingine ni unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan ambao utasaidia kuondoa matatizo yaliyo katika maeneo ya Muhimbili na Upanga, Mwananyamala na Kinondoni, Oysterbay na Masaki, Jangwani Beach, Bahari Beach na Mbezi Beach.
Mradi mwingine ni ule unaotekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ambao unaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Shinyanga, na Geita.
Mradi mwingine ni ule unaofadhiliwa na Serikali ya Finland ambao utasaidia sana kuimarisha umeme kati kati ya jiji la Dar es Salaam na kusaidia kuimarisha umeme katika eneo lenye majengo mengi marefu la Samora, Azikiwe, Kariakoo na Sea view.
Sambamba na miradi hiyo inayotekelezwa Dar es Salaam, mradi mkubwa wa kupeleka umeme wa 400KV kutoka Iringa kupitia Mtera, Dodoma, Singida hadi Shinyanga uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika na hivyo kutuhakikishia umeme wa uhakika katika kanda ya ziwa hasa jiji la Mwanza.
Kazi ya kuunga Songea na Gridi ya Taifa kutokea Makambako kwa 220KV inaendelea na Makandarasi wako kazini.
Kazi za kuunga Tanzania na Kenya kwa umeme wa 400KV inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani zabuni za kuwapata Makandarasi ziko katika hatua za mwisho. Ujenzi unategemewa kuanza mwakani.
Kazi nyingine ambazo hazijaanza lakini zitaanza hivi karibuni ni pamoja na Dar es Salaam – Somanga (400KV), Bulyankhulu – Geita – Nyakanazi – Rusumo (220KV)
Miradi hii ya kuimarisha miundombinu ikikamilika itasaidia kulipunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme kutokana na mfumo wa Usambazaji.
Nawaomba wateja wetu, wakati kazi hii kubwa inapoendelea, wawe na subira na uvumilivu kwa usumbufu wa hapa na pale utakaokuwa unatokea. Hata hivyo TANESCO itajitahidi kurekebisha kasoro zinazoweza kurekebishwa katika miundombinu ya sasa ili kupunguza usumbufu huo wakati marekebisho makubwa yakiendelea
 
Mkuu naona umeenda direct kwenye maboresho yenu hebu sasa rudi kwenye agenda kuu
 
KUDHIBITI WIZI WA UMEME
Shirika linaendelea na Kampeni maalum katika mikoa yote ya kuwakamata wezi wa umeme na kuwachukulia hatua kali. Pamoja na hatua nyingine zitakazochukuliwa, wezi wa umeme watakuwa wanatangazwa hadharani na kufunguliwa mashtaka. Hivyo ninatoa rai kwa ye yote ambaye amekuwa akijihususha na wizi wa umeme ajisalimishe mwenyewe kwa kwenda kwa Meneja wa Mkoa anakopatia huduma. Kama hawatajisalimisha kwa hiari hatua zilizokusudiwa dhidi yao zitachukuliwa pasipo huruma yo yote. Tunatoa siku saba kwa wateja wanaojua kwamba mita zao zimechezewa kujisalimisha wao
Naona unatetea mkate wako Tanesco.
 
Unataka kuniambia pale Tanesco kwenye interview lazima uvae msalaba?

Huku mnakoelekea iko siku mtamtaka hata moderator atoe idadi ya waislamu na wakristo hapa jf.Ila ukweli ulio wazi kwa wenzetu waisilamu kwenye upande wa maendeleo kwenye taasisi yenu mnakwenda mwendo wa kinyonga na sababu kubwa ni kwakuwa hamchangishani fedha za maendeleo. Kwa wakristo inakuwa tofauti kidogo kwani ni ukweli ulio dhahiri huku makanisani tunachangishana hela za maendeleo mpaka inakuwa kero na huku migogoro ni kitu cha kawaida kabisa. Ila niwaambie ndugu zetu waislamu mtakapoanza kuchangishana hela za maendeleo mjiandae na changamoto za migogoro isiyokwisha kwani fedha mwanaharamu. Hapo Mungu atawekwa pembeni na fedha itakuwa ndio kila kitu.

cc: Faizafox, the big show
 
Ile issue ya Dau NSSF imeanzisha mada nyingine kuhusu TANESCO!!!, kumbe aliyeileta ile mada aligonga Ikulu!!. Dawa ni utafutaji wa elimu kwa udi na uvumba, mambo ya dini sio ya kutumika kama uhalalishaji wa mtu au jamii fulani kushindwa kupambana maishani. Cha kushangaza ni kwamba wadhifa wa Chief Secretary haujawahi kushikwa na muislam tangu tupate uhuru, lakini sijawahi kusikia malalamiko. Waislam wawili wamekaa Ikulu kwa kipindi cha miaka 20 lakini CS ameendelea kuwa mkristo.

Tuachane na hizi mada nyepesi za udini. Matatizo yetu ni makubwa na mengi, tunahitaji kuzalisha watafiti wengi sana. Umeme unawafikia watanzania wasiozidi asilimia 50. Yapo mengi ya maana ambayo bado hayajafanyika, zipo fursa nyingi tu ambazo bado hazijatumika vizuri. Huu uislam na ukristo ni sababu tu ya kuhalalisha kutopiga hatua kwetu. Waungwana tubadilike, maendeleo ya dunia hii wala hayatusubiri.

Ushauri wako huutoa pale tu upande fulani unapohitaji ufafanuzi, ilipohojiwa NSSF bila ya ushahidi kama ulioletwa hukuonekana. Tatizo la unafiki kwny nchi yetu ni kubwa kuliko ufisadi na udini na ndio sababu wanasiasa wanatuchezea kama tako la baamedi.
 
Ushauri wako huutoa pale tu upande fulani unapohitaji ufafanuzi, ilipohojiwa NSSF bila ya ushahidi kama ulioletwa hukuonekana. Tatizo la unafiki kwny nchi yetu ni kubwa kuliko ufisadi na udini na ndio sababu wanasiasa wanatuchezea kama tako la baamedi.

HALI YA UZALISHAJI UMEME NCHINI
Hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbali mbali tunazokabiliana nazo kwa sasa. Kuanzia taerehe 17 Septemba tulipoanza kutumia gesi inayotoka Mtwara tumeweza kuongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi kutoka Megawati 260 zilizokuwepo kabla hadi Megawati 560 ikiwa ni ongezeko la jumla ya Megawati 300 au asilimia 115 ya umeme wa gesi uliokuwa unazalishwa. Hii imechangia sana kuboresha hali ya umeme tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Tunategemea kuongeza umeme wa Megawati 130 zaidi kutokana na vyanzo vya Gesi kati ya sasa na mwishoni mwa mwezi Januari 2016. Hii itafanya jumla ya umeme wote unaotokana na gesi kufikia Megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Haya ni mapinduzi makubwa kwani kwa miaka mingi vyanzo vya maji ndivyo vimekuwa vikichangia zaidi ya asilimia 70 ya umeme nchini na hivyo kusababisha athari za mara kwa mara kila unapotokea ukame.
Pamoja na hayo yaliyokwishafanyika, Mkandarasi wa mradi wa pili wa Kinyerezi (KII) wa Megawati 240 anatarajia kuanza kazi wakati wo wote kuanzia sasa baada ya kuwa amekwishalipwa sehemu ya fedha za awali za kuanza kazi hiyo.
 
Ushauri wako huutoa pale tu upande fulani unapohitaji ufafanuzi, ilipohojiwa NSSF bila ya ushahidi kama ulioletwa hukuonekana. Tatizo la unafiki kwny nchi yetu ni kubwa kuliko ufisadi na udini na ndio sababu wanasiasa wanatuchezea kama tako la baamedi.
Hao ni watoto wa uchochoroni, wasikusumbue sana Mkuu kwa kuonekana kwao wakati kama huu.
 
ashki majununi ati..
mnapiga mikelele isio na tija humu, huku mnajua daawa ni msalaba? hahahahaa...

wee ulitaka wazikiri? kale kapambio ka jehannam...harjununu fununu..ha ha..
harjununu ha haa(kichaa ni taaluma) Muhammad saw alisema hakuna mbora kama Mkristo..na mtawafuata shibrin shibrin dhirin dhirin hata kama wataingia shimoni na shimo lenyewe lina nge...
 
Back
Top Bottom