Tanesco na Dawasa sitisheni kupeleka huduma maeneo ya mabondeni

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,044
2,566
Mheshimiwa Rais wetu mpendwa tunakuomba uwaagize Tanesco na Dawasco waache mara moja kutoa huduma kwenye maeneo ambayo ni hatarishi(mabondeni). Kwa kufanya hivyo itapunguza kasi ya wananchi kujenga maeneo hatarishi.
 
Kama ili mtu ajenge inabidi apewe kibali na 'wizara' ambayo simply ni Serikali je inakuwaje watu wanapata vibali vya kujenga maeneo hayo hatarishi.
 
Wanaume wa dasmlam Kwa kulialia.......! Kanda ya ziwa Kuna nyumba zilimeswa ziwa lakini hakuna kelele. Tulijipanga upya tukaanza tena.

Dar vimafuriko vya nusu saa kelele Kila muda.

Je na ushuani yamewafika mafuriko au ushenzini tu?
 
Kama serikali itaweza kutafuta kwa haraka bajeti kujenga kingo za mito na vijito vya mjini Dar es Salaam mchanga unaokusanyika Jangwani itakuwa historia pia makaazi ya watu yaacha kubomoka


Picha hapa chini kingo za mto mkubwa wa usiokauka mto Siene katika jiji la Paris unaopitisha meli za cruise
1705813065607.png


Picha hapa chini za kingo za mto mdogo tena wa msimu wa mto Gide kitongoji cha Ubungo jijini Dar es Salaam

1705813098083.png

Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi chuo kikuu tajwa kongwe UDSM kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo TAMISEMI wangeweza kutumia kodi za wananchi vizuri na wanafunzi wa UDSM kujifunza kwa vitendo kujenga kingo hatimaye majina yao kuingia ktk rekodi kumbukizi tukuka kuwa elimu imewezesha kutatua changamoto katika jamii .

Picha hapo chini toka maktaba mchanga ukiondolewa kutoka mto Msimbazi uliokokotwa na maji toka kingo za mito na vijito vya maeneo ya mkoa wa DSM
1705813196136.png
 
Back
Top Bottom