TANESCO Morogoro mbona kila siku umeme hakuna kwa muda mrefu?

KITEKSORO

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
346
425
TANESCO Morogoro kwa kukatika huku umeme kila siku kwa masaa mengi mjitafakari. Nadhani Mh. Rais Magufuli hajagundua upuuzi huu ila soon atagundua na mtalia na kusaga meno pale mtakapotumbuliwa!

Kila siku umeme lazima ukatike na hakuna taarifa yoyote inayotolewa kwa umma. Wananchi wanateseka tu, biashara zinakufa!

Hata muda huu naandika msg hii hapa nilipo umeme hakuna zaidi ya four hours!! BADILIKENI. MENEJA WA TANESCO MKOA WA MOROGORO AMKA TATUA KADHIA HII. VERY SOON UTAKUMBUKA HUU UZI WANGU, IT WILL BE TOO LATE!
 
Kote hata huku tangu asubuhi ndiyo umerudi sasa.... kwingine nako giza sasa hivi kwa jirani. Mgao wa kisirisiri
 
Morogoro Wamezidi Yaani Kila Leo Utasikia Transformer Tunaifanyia Matengenezo.

Mara Sijui Nini!

Kazi Yao Kubwa Kuzurura Hasa Hao Kitengo Cha Emergency, Ukiwapigia Customer Care Kupokea Shida! Wajitafakari Upya Ila Hao Wagumu Mno!

Umeme Unakatwa Saa Zaidi Ya Nne Bila Taarifa.

Radio Zilivyojaa Tele!!
 
Nadhani ni nchi nzima naambiwa Moro, Arusha, mbeya kote Giza. Tanesco wame shindwa kazi.@5 tena
 
Kote hata huku tangu asubuhi ndiyo umerudi sasa.... kwingine nako giza sasa hivi kwa jirani. Mgao wa kisirisiri
Hivi nyinyi mnaishi wapi huko ambako umeme unakatika kiasi kwamba hadi mnalalamika namna hii?

Mimi binafsi sioni umeme ukikatika upo 24hrs
 
Huku chanika week hii yote ukifika saa 12 jioni wnakata hadi 6 usiku
 
Nadhani ni nchi nzima naambiwa Moro, Arusha, Mbeya kote Giza. Tanesco wame shindwa kazi.@5 tena
Ondoa sasa hiyo dhana maana Tanzania ni zaidi ya hiyo mikoa uliyoitaja na hata ndani ya hiyo mikoa uliyoitaja kuna mawilaya, tarafa, kata na mavijiji kiiiiiibao.

Ninakoishi umeme haukatiki kabisa hadi tunatamani ukatike angalau makelele yapungue
 
Sio Morogoro tu, baadhi ya maeneo hasa Chanika umeme unakatwa kila siku wakati wowote na kwa masaa mengi tu bila hata kutoa taarifa kwa nini unakatwa. Kwa ushahidi kabisa, umeme umekatwa leo mchana na kurudishwa kwa masaa machache, saa moja usiku huu umekatwa tena na kwa vyovyote vile watawasha saa 6 au 7 usiku.

Kwa ushahidi jana kwa masaa tofauti kuanzia saa moja jioni umeme ulikatwa, Mwanza Morogoro Arusha na Mbeya kwa wakati tofauti tena kwa masaa mengi tu, hata umeme ukiwashwa hauna nguvu hata ya kuamsha feni achilia mbali friji.

Narudia kusema tena kuwa TANESCO kuna kikundi kimejipanga kuihujumu Serikali na Kalemani anadanganywa tu, na anadanganyika kirahisi sana....Leo anaaminisha watu eti SGR haitakosa umeme pale itakapokamilika, hivi kweli umeme huu wa majumbani unakosekana kwa masaa, mtu anaibuka na tamko la hovyo namna hiyo?
 
Hivi nyinyi mnaishi wapi huko ambako umeme unakatika kiasi kwamba hadi mnalalamika namna hii?

Mimi binafsi sioni umeme ukikatika upo 24hrs
Nilikuambia juzi kuhusu mgao wa umeme morogoro ukabisha Sana Sasa huyo nae anadanganya halafu mbona unaitetea tanesco unamslahi nayo Sasa muda huu ninavyoandika hii msg kule turiani kwenye kiwanda Cha mtibwa hakuna umeme toka saa moja mechi ya Simba na jkt wameiangalia na majenereta piga simu muda huu huko mtibwa turiani usibishe ujinga mgao wa umeme upo hasa morogoro.
 
Kumbe upo Morogoro na si nchi nzima eeeh?
JF haina feature ya kwenda live ningewaonyesheni mahala nilipo na kinachoendelea then niwahoji watu kuhusu kukatika umeme.

Nadhani mngehisi nyinyi sio watanzania na shida zenu za umeme
 
Back
Top Bottom