TANESCO watenge eneo kwa umeme usiokatika sasa

TANESCO watenge eneo kwa umeme usiokatika sasa

rashidisa

Member
Joined
Nov 15, 2023
Posts
13
Reaction score
11
Tanesco mnachofanya mnashusha elimu yenu ya mambo ya umeme ,hivi mnakata kata umeme bila taarifa na bila kutuandaa hii SI kuua uchumi wa Taifa letu?

Kumbuka watu wamewekeza Kila Kona ya Nchi wakijua umeme ni wauhakika sasa Kila wakati mnakatakata umeme Kwa elimu Gani mliyosoma? Mfike mahali muone heshima ya ujuzi wenu mliyosoma acheni kukata umeme.

Kazi ya umeme kubwa ni kuzalisha bidhaa mbali mbali popote pale,Nchi hii Kila siku ni sababu tu mnazotuambia kwanini lakin? Kama mnashindwa kutenga eneo litakalokuwa na umeme imara Kwa uzalishaji

Nakushauri Rais wangu SAMIA binafsisha Tanesco TU Ili tupate uhakika wa umeme siyo hii wanayofanya Tanesco hata tukiwapa miaka elfu Moja hawatatatua changamoto ya kukatika Kwa umeme Nchini

Ushauri wangu ni huu tengeni eneo maalum basi ambalo mtafunga umeme usiokatika Ili liwe eneo la viwanda vikubwa na vidogo TU Ili hapo Nchi akusanye Kodi kwingine basi chezeeni mnavyotaka. Asante Kwa kunielewa
 
Back
Top Bottom