Tanesco kukata umeme; watoto wafa temeke kwenye disco toto wakishehereka idd! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco kukata umeme; watoto wafa temeke kwenye disco toto wakishehereka idd!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Phillemon Mikael, Sep 12, 2010.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  Yale machungu yaliyojitokeza mwaka juzi Tabora kwa watoto kufa kwenye disco kwa kukosa hewa ....safari hii yamejitokeza tena safari hii wilayani TEMEKE ambapo watoto zaidi ya watatu wamekufa na wengine kujeruhiwa ...mara baada ya umeme wa TANESCO kukatika ghafla kwenye eneo/mtaa ulipo ukumbi wa DISCO waliokuwa wakicheza..............huu ni mfululizo wa uzembe unaoendelea nchini!!!....magazeti ya leo yatakuwa na habari zaidi...
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tusubiri taarifa zaidi,
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  sitaki hata kulizungumzia hili.. nimelisikia toka jana.. na ninayo video ya ITV.. lakini tunazungumza ili kiwe nini? Kama hawakushtuka walipokufa 19 siku ya Idi katika mazingira yale yale.. kwanini mnafikiria watashtuka leo? Ni mapenzi ya Mungu.
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  ..kweli nchi hii kila kitu ni mapenzi ya mungu MJJ...TBC wameirusha wanasema...kuna wengine 11 wamelazwa hospitali wapo kwenye hali mbaya ......na kuna ambao wametibiwa na kuruhusiwa...

  kipindi kile iliundwa tume na waziri ....ikaishia kusema ni mapenzi ya Mungu na rais akatoa laki 5 kwa kila familia nadhani safari hii watafanya hivyo hivyo.
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni kweli MKJJ,
  mpiganaji thabiti hachoki na akichoka mapigano yamekwisha,
  Mungu yawezekana kweli ni jamvi la uozo? hata wa uzembe wa kiutawala? kwa nini yasiwe mapenzi ya uongozi mbovu!
   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Cha kujiuliza ni kwa nini vitendo hivi HAVITOKEI x-mas au pasaka..?

  Ujumbe utafika tuu.
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wewe sasa umeamua kuwatibua ngoja, waje sasa tehe tehe tehe,
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Pole wafiwa na watoto walioumia.

  Hili wenda halitokei kwa sababu krismas na pasaka, watoto haweindi kucheza disco usiku. Hili tatizo wakulaumiwa ni wazazi wanaoruhusu watoto kwenda kucheza DISCO tena usiku.

  Na tena labda sielewi, hili ni disco la aina gani? labda niulize ili nipate kwenda sambamba. Je ni disco wakimaanisha zile ngoma wanazopiga waislam mara nyingi wakati wa sherehe, ama ni lile disco la akina LUCKY DUBE?
   
 9. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Tulizungumzie lipi sasa?..au Terry Jones na uchomaji wa Koran..
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yaani mkuu nimecheka sana na haya mawazo yako, eee kweli bora ujuzwe, maana hata madrassa ni chuo!
   
 11. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kwa nini?
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Pamoja nimetoa lawama kwa wazazi harakaharaka, lakini naomba kufahamu ni DISCO lipi watoto wanaloenda kucheza? maana nakumbuka huwa kuna zile ngoma sijui (DAFU kama nimekosea nirekebishe), ama ni DISCO la akina TID?

  Na bado hizi lawama siwezi kuzielekeza kwa SERIKALI ama TANESCO, tatizo bado liko palepale kwa wanaoandaa hayo matukio na wazazi pia.
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Sijui labda ndo maadili ama tamaduni za siku hizo zinavyowaelekeza. Sina uhakika hapa
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  mkamap nadhani you were right na reason uliyotoa .....serikali ina lawama kwa sehemu kubwa kwa kuruhusu kumbi zisizokuwa na emergency exit za kutosha ...ambazo kwa kawaida hata umeme ukikatika maandishi yake yanatakiwa yareflect kuelekeza exit points.....maana suala la kukatakika umeme kwa Tanzania ni la kawaida...

  PILI NI UTAMADUNI WA KUSHEHEREKA....wengi..siku za sherehe hupenda kuwaachia watoto wakatembee kama mbuzi wasiokuwa na mchungaji....tena mbali kabisa na nyumbani...

  Mimi kwenye jamii yetu utamaduni wa sherehe tuliozoea ni kuwa sikukuu ni siku ya FAMILIA...hata kwa wale wanaume wakware lazima siku hiyo ukae nyumbani na familia..yako....hata wale wanaokaa mbali husafiri kujumuika na familia .na hata ukienda kutembea lazima uongozane na watoto....sio kawaida kabisa sikukuu kuwaacha watoto watoke peke yao....ITS TIME FOR FAMILY RE-UNION!!

  Nadhani hata nchi za ulaya wana utamaduni wa aina hiyo....siku ya sikuu kuu watu wote huwa majumbani mwao...wakitafakari na kusherekea.....
   
 15. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #15
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Poleni sana wafiwa, na walio mahospitali Mungu awajalie afya.
  Hapa nimeshindwa kuelewa, ni kwamba Tanesco walikata umeme ghafla au umeme ulikatika ghafla? maana hayo ni mambo mawili tofauti. kwa ninavyojua miundombinu ya umeme Tanzania ni mibovu sana hivyo kupelekea umeme kukatika ghafla mara kwa mara.
  statement yako bwana Phillemon imenifanya nijiulize, kwa nini Tanesco wakate umeme ghafla?
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Licha ya umeme kukatika lakini na miundombinu yenyewe ya kumbi nyingi za starehe haijatulia, ukumbi mdogo lakini unajaza watoto wengi kupita uwezo wake. Nadhani serikali ndio ya kulaumiwa kwa kuruhusu kila nyumba kuwa ukumbi wa starehe!
   
 17. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Umeuliza swali swali zuri sana. Nijuavyo mimi sio kwamba TANESCO huwa wanakata umeme ila miuondo mbinu yao ni mibovu na hata sometimes mteja wao huwa na wiring mbovu/zilizochoka hivyo kusababisha faults za mara kwa mara. Sidhani kama kuna haja ya kuilaumu TANESCO pekee, koz haiingii akilini kama TANESCO walienda katika huo ukumbi usiku na kukata umeme...na kama ni kweli basi mwenye ukumbi anapaswa kuwashitaki Tanesco na ma sure atashinda koz sheria za ukataji umeme za TANESCO zainasema ili mtu akatiwe umeme ni lazima kuwe na muda wa kwenda ofisi yoyote ya TANESCO iliyo karibu yake ili mara atakapolipia ankara zake aweze kurudishiwa huduma ya umeme. Kama Tanesco watakuja Nyumbani kwako Usiku kukata umeme then unatakiwa Uwatimue ni lazima waje ndani ya muda ambao wewe unaweza kufanya malipo katika ofisi zao.

  Pili tujenge utamaduni wa kufanya maintanance ya wiring katika majumba yetu tunayoishi na maofisi tunayofanyia kazi. Hakuna kitu kisicho na half life. maintanance ya Nyumba isiishie kwenye kupaaka Rangi, kubadili tiles na paa....kwa hili tutaepukana na faults zinazoweza kuepukika...
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sio mapenzi ya mungu ni uzembe na hulka ya kutaka hela kwa wanaoendesha shughuli za burudani kama hii ya temeke na ile ya tabora. Serikali yetu inaangalia mwisho wa pua, baada ya lile tukio( la tabora ) hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuhakikisha tukio kama lile halitokei tena.
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kweli kuna vibali hasa vinatolewa na serikali vya kuendesha disco kwa ajili ya watoto? :confused2:
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280

  kaka noted..siunajuwa tena kiswahili wengine ni lugha ya pili au tatu...i meant to say..."baada ya umeme kakatika ghafla".....naomba isomeke na kueleweka hivyo....,nadhani miundombinu na hali ya TANESCO inajulikana.........
  kule TABORA Mwaka juzi ni viyoyozi vilizidiwa nguvu watu wakaanza ku suffocate taratibu..bila kujijuwa wakawa wanaishiwa nguvu.........
   
Loading...