Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Hilo TANESCO na serikali yao ya Sisiem, wanaloliita ni punguzo la bei ya umeme, ni changa la macho la hali ya juu, lenye lengo la kuingia kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, wakijinadi kwa wananchi kuwa, hamuoni jinsi chama chenu kilivyotekeleza ilani yake ya kuwaletea maisha bora kwa kila Mtanzania?Gharama za kuzalisha umeme zimeshuka kwa 50% lakini inashangaza kwamba TANESCO bado hawajashusha bei za umeme kwa kiwango cha kuridhisha.
Zamani wateja wa kikabwela (KCC) tulikuwa twapata unit 2.7 kwa gharama ya Tsh 1000. Baada ya hili punguzo feki (linalopigiwa kelele sana na serikali kwa sababu ya kukaribia uchaguzi mkuu wa Oktoba), sasa mlaji hupata unit 2.8 kwa thamani ya Tsh 1000! Maana yake ni kwamba kwa kila Tsh 10,000 unapata unit 1 ya umeme! Hii ni dharau, kebehi na kejeli kwa wavuja jasho wa nchi hii.
Badala haya mafisadi yashushe bei ya umeme kwa walalahoi, wamefanya hivyo kwa wafanyabiashara na mapapa wakubwa ambao wana uwezo mkubwa wa kulipia umeme. Ni bora hili punguzo la kipuuzi liondolewe badala ya serikali kujitapa kwamba wameshusha bei ya umeme wakati hawajashusha chochote.
Ndugu zangu, nyie wote ni mashahidi mnapolipia ankara za umeme mahali mlipo. Ifike wakati tufunguke akili na kuing'olea mbali hii serikali ya wachumia tumbo mwezi Oktoba. Tusikubali kudanganywa tena na haya mafisadi.
Ukichunguza punguzo hilo,halina tofauti na la mzazi aliyemuahidi mwanae kumnunulia nguo mpya, lakini badala yake anarejea nyumbani na pipi ya ivory ya Jero na kumzawadia mwanae huyo ili 'kumnyamazisha' asiendelee kupiga kelele.
Hata hivyo waTZ mwaka huu tumeapa kuwa hatudanganyiki tena, na hata wakitugawia na khanga na mafulana yao ya bure, tutatekeleza ile slogan yetu mpya inayosema KULA SISIEM, lakini KURA kwa UKAWA.