TANESCO bado hawajashusha bei ya umeme kwa mlaji

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,195
Reaction score
27,810
Gharama za kuzalisha umeme zimeshuka kwa 50% lakini inashangaza kwamba TANESCO bado hawajashusha bei za umeme kwa kiwango cha kuridhisha.

Zamani wateja wa kikabwela (KCC) tulikuwa twapata unit 2.7 kwa gharama ya Tsh 1000. Baada ya hili punguzo feki (linalopigiwa kelele sana na serikali kwa sababu ya kukaribia uchaguzi mkuu wa Oktoba), sasa mlaji hupata unit 2.8 kwa thamani ya Tsh 1000! Maana yake ni kwamba kwa kila Tsh 10,000 unapata unit 1 ya umeme! Hii ni dharau, kebehi na kejeli kwa wavuja jasho wa nchi hii.

Badala haya mafisadi yashushe bei ya umeme kwa walalahoi, wamefanya hivyo kwa wafanyabiashara na mapapa wakubwa ambao wana uwezo mkubwa wa kulipia umeme. Ni bora hili punguzo la kipuuzi liondolewe badala ya serikali kujitapa kwamba wameshusha bei ya umeme wakati hawajashusha chochote.

Ndugu zangu, nyie wote ni mashahidi mnapolipia ankara za umeme mahali mlipo. Ifike wakati tufunguke akili na kuing'olea mbali hii serikali ya wachumia tumbo mwezi Oktoba. Tusikubali kudanganywa tena na haya mafisadi.
 
Tanesco ni kijiwe cha kupigia hela kwa ccm,huduma mbovu,umeme miradi inasuasua nchi nzima,hadi hela za rea wamezingilia kinyume na maumbile.
 
mimi kwa elfu kumi zimeongezeka 0.8 units

ndugu mompome yaani hii nchi ni ya ajabu sana. na wakati tunateseka hv na ugumu wa maisha kuna mifisadi inamiliki hela nyingi sana za wizi ambazo imezibatiza majina ya ajabu kama HELA YA UGOLO/MBOGA, VIJISENTI, nk.

Na pamoja na udhalimu tunaofanyiwa na serikali hii ya kifisadi, kuna mijitu itakuja hapa kama laki si pesa, ifweero, MUSSA ALLAN (MSALANI), Ritz FaizaFoxy, MwanaDiwani, thatha, TataMadiba, gsu, mjepo, Agogwe, Simiyu Yetu, Cybercrime, Queen P, et al itakuja hapa na kuanza kutetea ufisadi huu unaofanywa na TANESCO kwa maelekezo ya CCM.
 
Last edited by a moderator:
TANESCO hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika TANESCO katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.
Mmaaey swadakta ni ya kweli hayo na mungu akujalei uwe na upeo zaidi wa elimu
 
Nakushukuru sana bi mkubwa kwa kuonyesha ukomavu huu na kuukubali ukweli. Wapwa zangu Elli, lusungo, Mamndenyi, BAK na mjepo hebu piteni pande hizi tumpongeze huyu bi mkubwa. Naona mabadiliko yanakaribia.
 
Last edited by a moderator:
TANESCO hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika TANESCO katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.
Suluhu haiwezi kuwa kubinafsisha TANESCO, mifano hai ipo mingi. Kama tumeshindwa kulisimamia likiwa la umma, likibinafsishwa pasipo hata mshindani ndio tutaweza?
 
Libinafsishwe ki kanda na kikazi: ufuaji, usambazaji, usafirishaji viwe vinamilikiwa na kampuni tofauti ki kanda ili kuwe na ushindani. Ukizubaa kwa kutokufua umeme wewe wa Kusini, wa Mashariki anakupiga bao na hali kadhalika.
 
Vema! Umetoa ushauri mujarab sana bi mkubwa. Ndivyo inavyotakiwa kuwa, vingenevyo hakuna ufanisi utakaopatikana kutoka shirika hili lenye matatizo yasiyoisha.
 
TANESCO hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika TANESCO katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.

TANESCO is underperforming kwa sababu ya udhaifu wa serikali ya kikwete

Serikali inayoshindwa kusimamia uwajibikaji na haki

Serikali ya hovyo inayowajali matajiri na kuwapuuza mamilioni ya wananchi wake walio masikini

Mfano mzuri ni wa hili la bei ya umeme
 
Gharama za kuzalisha umeme zimeshuka kwa 50% lakini inashangaza kwamba TANESCO bado hawajashusha bei za umeme kwa kiwango cha kuridhisha.

Zamani wateja wa kikabwela (KCC) tulikuwa twapata unit 2.7 kwa gharama ya Tsh 1000. Baada ya hili punguzo feki (linalopigiwa kelele sana na serikali kwa sababu ya kukaribia uchaguzi mkuu wa Oktoba), sasa mlaji hupata unit 2.8 kwa thamani ya Tsh 1000! Maana yake ni kwamba kwa kila Tsh 10,000 unapata unit 1 ya umeme! Hii ni dharau, kebehi na kejeli kwa wavuja jasho wa nchi hii.

Badala haya mafisadi yashushe bei ya umeme kwa walalahoi, wamefanya hivyo kwa wafanyabiashara na mapapa wakubwa ambao wana uwezo mkubwa wa kulipia umeme. Ni bora hili punguzo la kipuuzi liondolewe badala ya serikali kujitapa kwamba wameshusha bei ya umeme wakati hawajashusha chochote.

Ndugu zangu, nyie wote ni mashahidi mnapolipia ankara za umeme mahali mlipo. Ifike wakati tufunguke akili na kuing'olea mbali hii serikali ya wachumia tumbo mwezi Oktoba. Tusikubali kudanganywa tena na haya mafisadi.
tpaul ungehimiza Tanesco wafanye juu chini kuhakikisha wanathibiti tatizo la kukatikakatika umeme kila siku. Hapa Arusha kila siku si chini ya lisaa umeme unakuwa umekatika; mbaya zaidi umeme wao unaogopa mawingo kukiwepo tuu dalili za mvua lazima umeme ukatike
 
Last edited by a moderator:
TANESCO is underperforming kwa sababu ya udhaifu wa serikali ya kikwete

Serikali inayoshindwa kusimamia uwajibikaji na haki

Serikali ya hovyo inayowajali matajiri na kuwapuuza mamilioni ya wananchi wake walio masikini

Mfano mzuri ni wa hili la bei ya umeme

Hapana ni "wasomi" wetu hao wanaoiendesha TANESCO.

Hapo ndipo mtapojuwa maana ya kuviondoa vichwa madarasani mkaweka mapakacha kuyasomesha. Hayo ndiyo matokeo yake.
 
tanesco hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika tanesco katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.

liuliwe tena,,,,kwani serikali imeshindwa kulisimamia,,,,,,
 
Hapana ni "wasomi" wetu hao wanaoiendesha TANESCO.

Hapo ndipo mtapojuwa maana ya kuviondoa vichwa madarasani mkaweka mapakacha kuyasomesha. Hayo ndiyo matokeo yake.

na hii yote ni kwa sababu ya serikali ya CCM kusiasisha elimu yetu. haya ndio matokeo ya divishen 5 za CCM na wala hawaoni haya kushuka kwa elimu yetu kwa kuwa lengo ni kuwadunisha watanzania kielimu ili waendelee kuiba rasilimali za nchi hii na kuficha fedha uswisi.

mimi nasema TANESCO haitaperform hadi CCM watakapong'oka madarakani mwezi wa Oktoba. hakuna mkato wala muujiza mwingine zaidi ya huu. get me?
 
TANESCO hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika TANESCO katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.

sawa mama,ila mimi nafikiri ubinafsishaji hautashusha gharama,ila at least ubora wa huduma utaongezeka unless iwe unazungumzia ubinafsishaji wenye kutoa nafasi ya ushindani mkubwa wa kibiashara ndani yake na sio ubinafsishaji huu tuliozowea hapa nchini kwetu ambao tender zinadhibitiwa ili wale wale wanaoua mashirika ya umma wapewe biashara yake.
 
TANESCO hawajashusha na wala hawatoshusha daima mpaka hilo shirika liwe la kibinafsi.

Kuna wizi wa kila aina unafanyika TANESCO katika ngazi zote.

Sitegemei kama watashusha.

Inabidi hilo shirika lote liuliwe kabla ya kuanza kushusha.

mashallah!nakuomba bibie,niko chini ya migu..i mean on bended knee leo hii iwe post yako ya mwisho ili JF tupumuwee!usiendelee usijeharibu tena lol!
 
Back
Top Bottom