Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023: Tulikubaliana kwa pamoja na tuliamua kitita kianze kutumika

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware amesema maamuzi ya ujio wa Kitita hicho ni matokeo ya makubaliano ya pande zote ambazo ni watoa huduma binafsi za Afya na BAKWATA kwa maslahi ya serikali na sekta binafsi.

Akizungumza na vyombo vya habari leo February 29,2024 Jijini Dar es Salaam, Dkt Saqware amesema kuwa hakuna atakayekosa huduma ya matibabu kwa kuwa mkataba baina ya mfuko na watoa huduma za afya wa sekta binafsi (APHFTA) haujavunjwa.

“Kamati ilikuwa huru kumsikiliza kila mtu, tulikubaliana kwa pamoja na tuliamua kitita kianze kutumika kwa faida ya nchi na taasisi zetu."amesema Dk Saqware.

Ambapo ameongeza kuwa “Kwahiyo tunapenda kutoa msimamo wa kitaalam kwamba Wizara kupitia NHIF iendelee na utekelezaji wa kitita cha mafao kilichoboreshwa cha NHIF cha mwaka 2023 kama ilivyoshauriwa na kamati,”

Pia amesema kuwa mapendekezo ya kamati ya wataalam ni pamoja na kuanza kutumika kwa kitita cha mafao cha mwaka 2023 pamoja na maboresho yaliyopendekezwa na kamati katika sehemu ya ada ya ushauri na kumuona daktari, huduma za dawa, upasuaji na vipimo.

Ameongeza kuwa kitita kinachotumika hivi sasa kilifanyiwa maboresho kwa mara ya mwisho mwaka 2016 hivyo Mfuko umelazimika kufanya mapitio katika Kitita hicho ili kwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na hali halisi ya utoaji wa huduma za afya nchini.

Itakumbukwa kauli hiyo imetolewa kipindi ambacho kumekuwepo na taarifa inayohusu vituo vya afya kuweka wazi kuwa vitasitisha kutoa huduma kwa Wagonjwa wanaotumia Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia Machi 1, 2024 hali ambayo inaendelea kuibua mijadala mbalimbali.

9655.jpg


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom