Tamko la NEMC litasaidia "Jobless" kupata Mtaji wa Biashara na Kuuaga Umasikini, hivyo tunawashukuru mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Kama nilivyomsikia Afisa wao Mmoja ( NEMC ) ni sahihi GENTAMYCINE nichukue tu nafasi hii mapema kabisa Kuuaga Umasikini niliokuwa nao sasa mwaka wa Kumi ( 10 ) kwani naenda kuwa Tajiri wa Kutukuka.

"Tunajipanga kuja na Tangazo la kumtaka Raia yoyote akiona tu Dereva wa Lori, Gari Dogo au Basi la Mikoani limepaki Msituni barabarani ( Barabara Kuu ) halafu Dereva au Abiria wanakojoa na hata Kunya ( Kuukweka ) upesi sana Piga Picha kisha tuletee NEMC kama Ushahidi na tutakupa Zawadi ya Shilingi Milioni Moja yako taslimu" alisema Afisa huyo wa NEMC.

NEMC nawaombeni toeni Tamko ( Tangazo ) hili mapema kwani kuna Malori fulani kama Matano huwa yanatoka Bandarini na Usiku wa Saa 4 huwa wanapaki maeneo ya Ruvu ambapo baadhi huwa Wanashuka kukojoa Porini na baadhi Kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) na hapa nikiwapiga Picha wote najua nitakuwa na Shilingi Milioni Tano zangu za haraka.

Pia NEMC fanyeni haraka kuja na Tangazo ( Tamko ) lenu kwani kuna Gari fulani za IT kama 15 hivi Usiku kati ya Saa 3 hadi Saa 5 huwa zinapaki Kuchimba Dawa ( Kukojoa ) maeneo ya mbele pale Msolwa hivyo najua GENTAMYCINE nikiwavizia hawa Wote na Kuwapiga Picha zangu Kumi na Tano ( 15 ) na kuwaleteeni Ofisini Kwenu mtanipa Zawadi yangu ya Shilingi Milioni Kumi na Tano hivyo nikichanganya na ile Shilingi Milioni Tano nitakuwa tayari nina kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini Kibindoni ambacho kitanitosha kabisa Kujiajiri kwa kuanzisha Mradi / Miradi.

Gari pekee ambazo hata nione zimepaki huko Njiani ( Barabara Kuu ) na Wahusika wameshuka na Kukojoa au Kuukweka ( Kunya ) kwa muda Vichakani / Maporini sitopoteza muda wangu Kuyapiga Picha na Kuwapiga Picha ni ya JWTZ kwani najua Wakinikamata nitajuta kwanini Wimbo wa Taifa hauna Kolabo au Nyoka hana Ugoko au Simba hajambi kama Binadamu Kudadadeki....!!

Haya 'Jobless' tuchangamkie Bingo.
 
Back
Top Bottom