Ongezeko la watu Duniani na yanayoendelea

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Nani alaumiwe kwa vitendo vya laana vinavyoendelea kwenye hiki kizazi, je , serikali kwenye nchi zenye nguvu na ushawishi Duniani Wana msimamo gani juu ya haya?vipi kuhusu nchi yetu?

Nimesikia kuwa Kuna watuhumiwa kadhaa wanaojihusisha na ushoga, wamekamatwa sehemu mbalimbali nchini Tanzania, iwe kwa kukiri au kuhisiwa tu, looh nasikitika sana na kuumia sana juu ya watu kufanya wenzao kama kiburudisho.(mabasha adhabu yao ni kunyongwa tu)na hao wanaokamatwa ni wale wanaofanywa, vipi wale wanaowafanya,hali ni mbaya mtaani hata ukamate watu 1000 kwa siku ni sawa na 0.001% ya wahanga na hawalazimishwi kwamba ni ukatili wengi wao wanataka wenyewe.

Zipo sababu kadhaa ambazo hupelekea haya kwenye Dunia ya Sasa

1. Ukosefu wa ajira
Leo hii ili upate nafasi au ajira kunahitaji marefa na watu ambao kwa masharti maalumu utagawana nao asilimia fulani za mshahara kwa kipindi fulani, huku njia mpya na chafu ambayo ni rushwa ya ngono ikishika nafasi kubwa na mbaya zaidi kwasasa mabazazi, au washika dau hawachagui jinsia, hivyo vijana wakike na wakiume,wadogo zetu wanajikuta hawana la kufanya anaamua kukubali kishingo upande kusudi atimiziwe haja zake.

2. Kuchagua kazi za kufanya
Vijana wengi kwasasa hawataki kusikia hizi physical work, kukoroga zege, saidia fundi na zingine zinazofanana na hizo, badala yake wengi wamekimbilia kuendesha bodaboda, kufungua vijistudio uchwara na viji library, yaani zile kazi soft soft huku wakiwa wanapendeza kupitiliza kuwashinda hata dada zao ,
Je,nani wanatoa mitaji wezeshi kwa Hawa vijana? (Napata mashaka)

3. Kupenda maisha mazuri
Kwasasa Kila mtu anahitaji kuishi maisha fulani ya kisasa hata kama siyo kivile lakini angalau aendane na wakati, neno gari si anasa kama zamani wengi wanasema hivyo, lakini je kwa mazingira na vipato vyetu Kila mmoja anamudu? Hapa ndipo tatizo linapokuwa kubwa.

Vijana wanasukuma IST, Brevis , altezza , Subaru n.k huku wengi wao wakiwa hawana ajira Wala kazi za uhakika, vijana wanamiliki matoleo mapya ya simu, pamba Kali na ni watanashati mno (napata mashaka)

4. Michezo ya kubashiri {betting}
Uraibu mbaya Duniani kushinda hata madawa ya kulevya, ndiyo unawamaliza vijana, na kujikuta wanaangukia kwenye kukata tamaa ya maisha mapema.

Wakati unafanya kibarua na kulipwa TSH 7000/=per day, ambapo haizidi laki mbili kwa mwezi, Kuna jamaa yeye anaweka mikeka yake mitano ya miatano miatano , huku yule shetani anayeangamiza Hawa vijana akifanya mkeka mmoja uwin, basi matineja na wavivu hufurahia hali hii yaani miatano kwa laki na nusu, wakati mikeka yote iliyochanika alibet kwa pesa isiyo zaidi elfu tano, na umfamnyishe kazi ngumu?

Kimbembe kinakuja pale ambapo inakatika wiki nzima hajala mkeka mraibu huyu, huwa anachangangikiwa yupo tayari kufanya lolote na kufanywa lolote ili mradi mkono uende kinywani na apate mtaji wa kuendeleza uraibu wake,nasisitiza Yupo tayari KUFANYWA chochote kijana huyu mraibu (kazi ipo)

5. Kupenda starehe {za muda mfupi) kuliko uwezo
Leo hii neno kidimbwi na sehemu zingine za starehe si geni kwa baadhi ya watu, na Kila mpenda starehe yeyote anatamani kufika, haijalishi ana mawe (pesa) au la, yeye hujichanganya kwa watu wanaoitwa madon na maboss,huku , kazi yake ikiwa ni kuwaita wanaume wenzie maboss, siku hizi wanaitwa wapambe, machawa, n.k

Utasikia maneno kama Vipi mshua, vipi mwamba, oyaa niaje boss wangu, huku akirembua macho yake na kutikisa dredi zake alizoosha vizuri zikatakata, huku akiwa mcheshi na muongeaji mzuri kupitiliza,anaujua mpira vizuri, anaujua muziki vizuri, hata siasa pia, yeye kazi yake nikukusoma wewe boss kipi una interest nacho basi atapita humo humo na hakika utafurahi uwasilishaji waje na pombe nzuri utanunua. Je , unadhani jasho la Kila mtu huenda bure kwenye Dunia ya leo? (watu hawaachi kitu)

6. Kukata tamaa ya maisha
Katika makosa yote mtu hutakiwi kufanya ni hili la kukata tamaa na kuhisi huwezi fanya chochote tena, ukiona liwalo na liwe. Hapa lazima ushushe thamani yako na kujikuta unawapa mianya mabazazi na mamende kutumia nafasi hiyo kulaghai na kutimiza azma zao mbaya, mwisho wa siku mtoto wa kiume unazoeshwa michezo isiyostahili (kufr laana)

7. Kuzamia kwenye nchi za watu
Siyo kosa kwenye ughaibuni kuharibu zali , lakini lazima kujipanga na kujua A, b, c kadhaa kabla ya kuchukua uamuzi. Vijana wengi hujikuta wanapelekwa huko ng'ambo na kukuta kazi aliyoahidiwa ni tofauti na aliyoikuta, pia unaweza usiikute kazi yoyote ukajikuta unaishi maisha magumu , mwisho wa siku unaangukia mikononi mwa watu wabaya ambao, aidha wanalipa kisasi kwakuwa walifanyiwa hivyo, au ni tabia zao za kupenda migongo (kufr laana)

8. Haiba na muonekano wa kike kwa mtoto wa kiume {sura ya mama}
Si lazima kwenye kundi hili mtu awe na hormones za kike hapana, ila hapa vijana hulazimishwa, kwa kutongozwa kabisa ,si lazima akutamkie Bali anaanzia mbali kwa kukutafutua ajira nzuri, au kuuza duka,au uwe dereva wake, mtoto wa kiume anazungukwa bila kujua, atakataaa weeee lakini mwisho wa siku dau likiwa kubwa, hujikuta anaelemewa na kujikuta anaingia mzima mzima kwenye huo mkumbo,mwisho wa siku anaona ni kawaida kwani kama ni mademu naye si anao. basi anapiga naye anapigiwa.

9. Malezi {hasa single mother)
Hapa Sina haja ya kupaelezea sana, ila ni hatari sana mtoto kulelewa na mzazi mmoja hasa wa kike (samahani dada na mama zangu sisemi hamuwezi kulea). Utandawazi, mzazi kubadilisha nguo mbele ya watoto akidhani ni watoto hawaelewi, kuleta mabwana ndani kwako yaani chumba kimoja unacholala na mwanao huku ukifanya mapenzi kwa kujiachia ukidhani amelala kumbe miguno na kelele zote akisikia. Nini madhara yake kwa mtoto, tambua kuwa hisia anazovuta hapo siyo za kufanya bali kufanywa anakuwa huku akiharibika kisaikolojia akiwaza kujaribu kusukumiwa nyama kama alivyosikia toka kwa mama yake, tatizo ndipo linapoanzia.

10. Umasikini, umasikini, umasikini
Moja ya maadui watatu aliowahi kuongelea mwalimu ni umasikini,najua itakuwa ngumu msomaji kuelewa hii point lakini ukweli ndiyo huu.

Umasikini ndiyo unabeba yote yanayosababisha kushamiri na kukua kwa matendo yasiyofaa na chukizo mbele za Mungu.
 
Umepindisha kichwa cha habari ili uzi wako usiunganishwe na ule
Kwa hiyo hayo ndio mambo yanayofanya ongezeko la watu duniani ama ndio mambo yanayoleta ushoga?
 
Back
Top Bottom