Tamko la kamati kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba

Akiongea baada ya wabunge wa chadema kutoka nje alisema Rais wetu mpendwa "Mtatoka mtaenda mtarudi kwani mimi ndio Rais wenu hamna mwingine wa kumpelekea matatizo yenu ila ni mimi" alisema Rais kikwete. je kwa chama cha demokrasia na maendeleo kuunda kamati ndogo ili kwenda kumuona Rais kikwete je kwanza wamemtambua? je wataacha mchezo wao wa kitoto kutoka bungeni Rais anapohutubia utakoma? je watakubali maneno ya Rais kuwa mtakwenda mtarudi Rais wenu ni mimi?

habri hiyo wewe umeitoa wapi?
 
LINI?! Ni baada ya General Election 2010, WAPI?! mbele ya waandishi wa habari including BBC Swahili service!!!! Hata hivyo, Dr. baadae alikula matapishi yake kwa kutangaza kumtambua rais kwavile eti "ni rais kwa mujibu wa sheria", sasa sijui kuna rais kwa mujibu wa nini cjui!!!!

waliimanisha matatizo yako kwenye sheria zetu hatuna budi kuzibadilisha bahati mbaya zinataka kubadilishwa kisanii..
 
Hehe ... if you can't fight them join them .. wamegundua hata wakisusa katika mpya mchakato utaendelea tu ,
 
Ok,

Kwahiyo CDM wanaenda kumwomba JK awashirikishe kwenye uundaji wa katiba mpya?

Mapendekezo yao JK hajayaona ama wanadhani labda presence yao itasaidia?

Ama wanadhani hajapewa taarifa za kutosha kuhusiana na msimamo wao?

Lets wait and c...

Ni kweli anazo taarifa pengine za kutosha kuhusiana na msimamo wao, nafikiri uamuzi wa kwenda kuonana naye si lazima awasikilize lakini ni moja ya hatua ya watu wastaarabu kujaribu kila namna nzuri isiyokuwa na gharama kubwa kabla ya kuchukua maamuzi mengine amabayo pengine ni ya gharama kubwa.
 
Tamko is very mild and conditional. I was expecting a total rejection of the proposed bill. Kwa kusema wako tayari kuona mswada unafanyiwa marekebisho wanarudisha nguvu kwa CCM. CDM wametoa ofa kwa CCM kuwa "mkibadili sheria tutashiriki".. I believe its a bad offer. Au hata wangeifunga katika kifungo cha muda. Oh well.

It IS a total rejection. Wasipota suluhu kwenye mazungumzo na muswada ukawa sheria wanarudi kwenye mikutano ya hadhara na maandamano yaliyopigwa marufuku na polisi. Hata kitendo cha CDM kwenda kuhubiria wananchi kuukata mchakato wa kupata katiba mpya ni kuvunja sheria na adhabu yake ni jela miaka mitatu na/ faini ya milioni 5. These are bold statements ukizingatia CDM wanajua jk atakataa "ofa" yao kwa kuwa yuko adamant kusaini.
 
MKJJ mimi nafikiri offer ya kukutana na rais si mbaya kama Mzito kabwela alivyosema hapo juu ni kuonyesha kwa wananchi na mataifa ushiriki wao katika kutafuta suluhu, na endapo mambo yatashindikana na kuamua kuchukua option ya mwisho watakuwa na cha kusema tulimshauri hakutusikiliza. Elewa Chadema si wajinga wameona wakitumia nguvu ya umma leo (ambayo CCM walikuwa wanategemea) CCM wanaweza kupata kisingizio na kwenda kwa wananchi kuwashitaki. Kitu kingine kama alivyosema MKabwela Donors kina Cameron wanaweza kuwauliza Chadema walikuwa na alternative gani nyingine iliyoshindwa. Ila mimi kama mimi hata Chadema wenyewe wanajua kuwa wanakwenda kukutana na rais kama ushahidi tu hakuna tangible solution yeyote itakayopatikana.


ni kweli lakini twende mbele kidogo; hii ofa inatarajia kuwa Rais Kikwete atakuwa tayari kuonana nao - kitu ambacho kinahitaji ujasiri mkubwa sana kwa Kikwete maana yeye ndio kiongozi alitakiwa kuonesha njia- sasa kama hawataweza kumuona kwa wakati huu itakuwaje? Lakini pia inatarajia kuwa Rais asiutie sahihi mswada kuwa sheria sasa akiweka na ukawa sheria kabla hawajakutana naye watakuwa wameenda kumbembeleza ufanyiwe marekebisho?

Na wakati wanasubiri marekebisho Rais akateua tume ya kukusanya maoni, bado wataendelea kuombea Rais awasikilize. Ni wakati gani wanachora mstari usiovukika?
 
Ni rais kwa sababu ametangazwa na kuapishwa kuwa rais lakini kafikishwa hapo baada ya matokeo kuchakachuliwa! Hiyo hata mbishe kiasi gani ndio ukweli wenyewe! Kumalizia tu nakurudishia kuwa wewe sio tu kuwa ni kiazi bali ni gimbi kabisa! Ubongo wako umekauka kama gamba la kobe!

Na wale ma observer wooote wa ndani na nje ya nchi waliwadanganya dunia kuwa kura zilikuwa halali?
 
Kinachonichekesha kuhusu mashabiki wa CCM badala ya kutekeleza sera za chama chao wanazoimba kila siku kwamba ndiyo msingi wa kukubalika kwao wako bize to paint CHADEMA bad. Sera kuu ya CCM sasa hivi ni kuwaambia wananchi CHADEMA ni chama cha vurugu, NGO, chama cha kikabila, cha kidini, cha ukoo etc. What a joke??????????? Huko ndiyo kunaitwa kufilisika kisiasa how come kuanzia mwenyekiti wa CCM, viongozi waandamizi, na mashabiki badala ya kuelezea na kutekeleza sera za chama chao wako bize na mambo ya chama pinzani? Bahati nzuri wananchi wanaona na kudigest vizuuri kuhusu nini kinaendelea.They can see kwamba ile so called "jeuri ya chama" imeshapotea kabisa. Ndiyo maana viongozi wa CCM hata hawajiamini tena kusimama ndani ya public square kudebate muelekeo na mustakabali wa nchi yetu.

Jambo jingine ambalo naona wengi hawalielewi na pengine hawalijui kabisa ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya political activism na siasa ukweli. Ndiyo maana wanashindwa kuelewa ni kwa nini CHADEMA wameunda hiyo kamati ya kumuona raisi na si mwenyekiti wa CCM.
 
As I can remember, its more or less than a year ago since Slaa refused to concede electoral defeat calling it fraud and I am not sure if he had eventually came to publicly accept it. I am astonished that he is now becoming part of a team appointed to meet the president whom he does not even recognise! I don't want to believe that he can do such unthinkable decision as to be viewed as the most irresolute politician this country has ever seen.
 
MUSWADA WA MAKINDA NI SAWA NA JUMBA LA DHAHABU ILIOJENGWA KATIKA MSINGI WA BISKUTI USWAHILINI

Sheria ya Makinda iliopitishwa majuzi bungeni Dodoma ni sawa na jumba kuuuuubwa la kifahari liliojengwa kwa matofali ya dhahabu lakini chini yake likisimama juu ya MSINGI MARIDADI LAKINI ILIOJENGA KWA VIJIPANDE VYA BISKUTI.

Kwa uelekeo huo, maana yake ni kwamba gharika la Umma wa Tanzania pindi tu utakapopiga basi tujue kwamba hakuna tena jumba hapo. Safari ndio hiyo inaendelea.

Utaifa mbeeeeele kama tai, KATIBA MPYA kamwe hatutoiacha ianguke kama mane mane toka angani; KATIBA MPYA ni jukumu letu sisi wenyewe (unalienate right) kulitunga wenyewe TUKIWA TUMEUSHIKA USHUKANI SISI WENYEWE na wengine woote ikiwa ni pamoja na Rais, Ikulu, Bunge, Mwanasheria Mkuu na Serikali ya CCM kwa ujumla wake wakiwa ni sehemu ya ABIRIA WETU MUHIMU sana katika zoezi zima hili.

As I can remember, its more or less than a year ago since Slaa refused to concede electoral defeat calling it fraud and I am not sure if he had eventually came to publicly accept it.

I am astonished that he is now becoming part of a team appointed to meet the president whom he does not even recognise! I don't want to believe that he can do such unthinkable decision as to be viewed as the most irresolute politician this country has ever seen.
 
Hii iko vizuri. kumuona rais na kuzungumza naye. Iko kiungwana zaidi,bila shaka naye atawapokea na kuwasiliza.
 
Hii move ni nzuri na ni ya kuungwa mkono kwa wapenda maendeleo wote.

CHADEMA niwape hongera kwa kutambua kuwa at any one time kunakua na rais mmoja, hivyo ni vizuri wamemtambua.

Pili kuonesha kutokubaliana kwa dhati kabisa na muswada uliopita bungeni, tena kwa step ya kwanza ikiwa ni ya majadiliano. Hapa naona wamemtega JK,... Kwa kuwa hata wakirudi kwa wananchi watakua na cha kusema kwamba mbinu mbadala zimeshindikana.

Tatu, JK chondechonde kaa meza moja na CHADEMA uwasikilize ukiwa na open mind, sio guarded mind. In that way utaweza kujifunza kitu ama kuona point wanayoona CDM haiko sawa.

Nne, timu nzito wa viongozi waandamizi wa CHADEMA muwe tayari kucompromise pale mtapoona ni pana cosmetic effect rather than structural effect ya huo mswada, ili uchaguzi wa 2015 tuingie na katiba mpya. In other words muwe na list ya absolutely unacceptable items, items to be revised, na desired changes.

Mi najua piga ua galagaza hakuna seating head of state wa CCM, hataweza kusimamia uundawaji wa katiba mpya utakaoruhusu yeye mwenyewe kushtakiwa pindi atakapoachia madaraka. Kama atakubali mabadiliko ya structure ya mchakato wenyewe, na wakati wa mchakato kukawa na mabadiliko ya msingi na kuweka proper checks and balances. Basi kubalini ili asign tuwe na katiba mpya kwenye next election 2015. Baada ya kupewa madaraka Rais kutoka CDM anaweza kuweka amendment za kuruhusu rais aliyestaafu kushtakiwa.

Ni mawazo yangu tu!
 
Back
Top Bottom